BALOZI ZETU NJE YA NCHI: wapi zipo na wapi hazipo?

Je tuna ubalozi irani maana wale wangetufundisha utundu utundu na sisi tukawa tishio kidogo ati!!mafuta pia tungepga mizinga!hata bure tungepata
 
Nurujamii, huo ndiyo utaratibu. Usitie shaka. Kwa maana ya jengo, Israel hawana jengo la ubalozi hapa Tanzania, lakini wanawakilishwa vema na balozi wao anayeishi Nairobi.
 
Kama alivyouliza Mtu wa Pwani, mbona huulizii Nchi za Nordic (isipokuwa Sweden)na nyingine kama hizo ambazo pamoja na kuwa na ubalozi nchini kwetu ni wafadhili wetu wakuu! Kwa nini Sudan tuu?

Kwa Nchi za Nordic ubalozi ni hapo Sweden...
 
Baada ya vita ya 1967 Tanzania tulivunja uhusiano wa kibalozi na Israele ili kuwatetea wapalestina.

Naamini kabisa kabla ya hapo Israele walikuwa na ofisi ya Ubalozi nchini Tanzania.

JKT ilianzisha na Israel na hata sasa wanafufua JKT kwa kuwashirikisha.
UDSM na ilijengwa na kuendeshwa kwa muda na Israel Kilimanjaro Hotel pia ilijengwa na Israel.

Yes, nimeshawahi kusikia kuwa UDSM ilijengwa na Israel na by the time tunavunja uhusiano nao hiyo project ya UDSM ilikuwa haijaisha. Nafikiri miaka hiyo ya 60's na 70;s viongozi wetu walitoa kafara faida nyingi sana za Taifa letu kwa sababu za kisiasa.
Kama ni kweli Israel walitujengea chuo, Hospitali ya Bugando, na miundombinu mingine katika miaka ya mwanzo tu ya uhuru afu then tukawapa talaka kwa sababu za kupata ujiko kisiasa basi tumelogwa. Sababu kwa bongo UDSM mmpaka sasa haina mpinzani na Bugando pia ni moja ya giant healthy facility kwa nchi yetu.

Nafikiri ilikuwa inatosha kutoa tamko la kulaani ukandamizaji wa watu Palestina na kisha kuendelea kuchangia kuwasuluhisha tukiwa na uhusiano na pande zote mbili. Kuvunja uhusiano na misimamo mingine ya kukurupuka itakuwa imetukosesha vitu vingi sana. Mbona Mugabe hatuvunji nae ndoa? Nafikiri vitu vingine ilikuwa ni katika kufuata mkumbo tu!

Ni kweli kuna itikadi za kidini, kisiasa na mambo mengine yanayoleta zengwe katika kuutazama uhusiano wetu na Israel. Lakini inaonekana kuna faida nyingi zaidi kwa maendeleo ya nchi yetu. Kwa mtizamo wangu naona ni muhimu kuboresha uhusiano wetu na nchi zote zenye nia na dhamira njema ya kutujengea uwezo kiuchumi, kielimu, afya, na maeneo mengine ukizingatia hii ni karne nyingine kabisa.
 
Kwa Nchi za Nordic ubalozi ni hapo Sweden...

Sudan ubalozi uko Misri! Kinachodaiwa hapa ni ubalozi ndani ya nchi husika. Hatuna ubalozi Denmark, Norway, Iceland, Finland, Latvia na Estonia. Tunawakilishwa kwenye zote hizi na balozi wetu aishie na kufanya kazi Stockholm, Sweden. Sudan vilevile tunawakilishwa kutoka misri.
 
Sudan ubalozi uko Misri! Kinachodaiwa hapa ni ubalozi ndani ya nchi husika. Hatuna ubalozi Denmark, Norway, Iceland, Finland, Latvia na Estonia. Tunawakilishwa kwenye zote hizi na balozi wetu aishie na kufanya kazi Stockholm, Sweden. Sudan vilevile tunawakilishwa kutoka misri.

Tatizo linaweza kuwa ni la kiuchumi na mazingira kwa kutokuwa na ofisi za balozi katika nchi ambazo zina balozi zao nchini.
 
Tatizo linaweza kuwa ni la kiuchumi na mazingira kwa kutokuwa na ofisi za balozi katika nchi ambazo zina balozi zao nchini.

Kabisa, na hii ndio sababu hasa inayotufanya tukawa na balozi chache sana. Kuziendesha kunahitaji gharama kubwa, na uchumi wa danganyika ndio hivyo unachechemea mno!
 
Kabisa, na hii ndio sababu hasa inayotufanya tukawa na balozi chache sana. Kuziendesha kunahitaji gharama kubwa, na uchumi wa danganyika ndio hivyo unachechemea mno!

Aliyeanzisha mada anajua yote haya. Kuna kitu kimejificha kwenye hoja nzima!!! Ndiyo maana anaulizwa, kwa nini Sudan?
 
Aliyeanzisha mada anajua yote haya. Kuna kitu kimejificha kwenye hoja nzima!!! Ndiyo maana anaulizwa, kwa nini Sudan?

@Fundi
Duh, hii nayo!
Sasa we fundi ni kitu gani unahisi kimefichika hapa? Kwamba jamaa kuna jibu alikuwa anataka nje ya haya tunayojadili ama?
 
Unatakiwa kueleza wazi ni nini hasa uachotaka kujua, ni uhusiano wa Kibalozi au uhusiano wa Kidiplomasia. Tuna uhusiano wa Kidiplomasia na nchi nyingi sana lakini tuna uhusiano wa kibalozi na nchi chache, na hizo ngazi za uhusiano wa kibalozi pia ziko tofauti. What is it that you want to know?
Ukumbuke kuwa most of our diplomatic missions, are mission less. Kwa maana zipo kama symbol of friendship, lakini hazina clear objectives na goals za kuweko huko ziliko, kama nchi nyingine zinavyofanya. Kuhusu uhusiano wa elimu ya Kidini kati ya Tanzania na Sudan, siwezi kusema kwa sababu sijui sera yetu ya mambo ya nje inasemaje kuhusu uhusiano wa elimu ya kidini na ina manufaa gani kwa taifa! Ukiuliza vizuri swali lako utapata majibu!
 
Fahamuni kuweka ubalozi kwenye nchi fulani sio kitu rahisi,unahitaji fedha na gharama nyingine nyingi na ndio maana ili ubalozi uwepo kwenye nchi fulani kuna vigezo vya kuzingatia,ikiwemo umuhimu wa nchi hiyo kidiplomasia,siasa na kiuchumi vilevile uwezo na ndio maana tunaposhindwa tunaweka ubalozi mdogo(consulate) au balozi mmoja anahudumia nchi mbili hadi tatu. Na sio sudan tu sehemu nyingi hatuna ubalozi,ikiwemo chad,mali,afrika ya kati, n.k kwa nini sudan tu?
 
Hizi F**** balozi kazi zake ni nini? hamna maana ya kuwa na balozi zinakuwa picha kwa watanzania.P@$%@#^$ zao wanapeana kula tu.....wanatia hasira sana
 
Balozi ni kiungo kizuri sana kati ya nchi yetu na ile nchi ulipo ubalozi wetu.Balozi ni mtafiti wa maswala mengi sana ya kiuchumi,uongozi,siasa,utamaduni,na mambo mengi,mengi sana kwa ajili ya kuendeleza nchi yetu.Nafasi ya ubalozi ni kitu muhimu sana, ila tatizo ni mtu yule aliyepewa dhamana ya kuwa balozi.Mara nyingi Mabalozi wa Tanzania nchi za nje wamejisahau kabisa kuwa wanawakilisha serikali yetu huko walipo;maana yake wanawawakilisha wanachi wa Tanzania, na badala yake mabalozi wengi wanajinufaisha wenyewe na kujisahau kuwa wao ni macho ya Rais katika kuleta maendeleo hapa nchini.
Namuunga mkono Rais Kikwete kwa kuwaalika nyumbani mabalozi wetu wotenchi za nje ili wapewe namna ya kufanya shughuli zao huko nchi za nje. Waziri Membe alieleza bayana haya yote jana katika mmahojiano na mwandishi wa habari.Mimi naunga mkono, waletwe hawa mabalozi ili waelekezwe namna ya kufanya kazi zao wasilale tu na kuiletea nchi yetu hasara kubea kama ambavyo wengine wamekuwa wakifanya kwa fikra kuwa serikali imelala.Wawajibishwe noja kwa moja pale itakapobainishwa kuwa kumefanyika ubadhirifu fulani katika ubalozi fulani.Au wana JF mnasemaje?
 
Back
Top Bottom