TEAM 666
JF-Expert Member
- Dec 7, 2017
- 4,330
- 8,421
Rai hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Hamdi Mansour Abuali,wakati akizungumza na waandishi wa habari akizungumzia juu ya machafuko yanaendelea kati ya Israel na Palestina.
Aidha,Balozi Abuali amesema mashambulizi hayo yamekuwa yakitoa roho za watu wasiokuwa na hatia.
Balozi Abuali,amesema mbali na kuondoa roho za watu,machafuko hayo yamewaacha zaidi ya milioni 2.2 ya Palestina wakiwemo watoto kukosa mahali pakukaa.
"Hakuna mafuta,hakuna umeme,hakuna chakula,hakuna maji yaani kila kitu kimefungwa,zaidi ya watu 1300 wamekufa,watoto wakiwemo 344,makazi 790 yameharibiwa huku zaidi ya wapalestina 339,000 wameyakimbia makazi yao"Amesema Abuali.
Hata hivyo,Balozi Abuali amezitaka jumuiya za kimataifa kupinga kile alichokiita ukatili unaofanywa na Israeli kwa wananchi wa Palestina
Naye, Mwenyekiti wa kamati ya mshikamano kati ya Tanzania na Palestina, Abdulaha Athuman, amewataka watanzania waungane kwa pamoja kulisaidia Taifa la Palestina kulaani kile kinachofanywa na Islaeri kwa Taifa la Palestina.
Athumani,Amesema Taifa la Palestina kwa miaka mingi limekuwa likisaidia mataifa ya Afrika ikiwemo ukombozi wa uhuru kwenye baadhi ya nchini za Afrika.