Balozi wa Palestina asaidie watanzania 2 waachiwe na Hamas

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,508
19,320
Taarifa toka mitandao ya Israel zinaeleza kwamba, vijana wawili wa Kitanzania waliokuwa wamepelekwa na Serikali Israel kufanya Intenship ya Kilimo, wametekwa na Hamas na hadi sasa wapo mikononi mwao kama mateka, na wao sio Wayahudi,

1. Joshua Loutu Mollel (Masai au Mmeru),

2. Clemence Felix Mtenga (Mchaga)

nakumbuka kama mwaka jana, vijana kama 200 walipelekwa Israel kwa ajili ya kujifunza kilimo. tafadhali, tunaomba Serikali itoe tamko waachiwe. Tayari serikali imeshatia kura UN kulaani mashambulizi Gaza na kutaka yasitishwe, ila kwa hili Balozi wa Palestina yupo hapahapa Tanzania, tunaamini yeye anaweza kuwaomba hamas wawaachie tu hao vijana, hawana hatia yeyote, ni watoto wetu wachamba fulani tu wa hapo Arusha na Kilimanjaro, wala hawajaenda kule kupigana wala kufanya uovu wowote, wanatafuta tu maisha. tuungane kusambaza wito huu tafadhali.

Vilevile Balozi wa Palestina alivyotoa wito Dar es Salaam watu walaani mashambulizi ya Israel, hivyo hivyo na yeye atusaidie kuwaambia Hamas wawaachie Watanzania wenzetu.
 
Nchi hatuna viongozi, hawajui wajibu wao kwa raia.
Pili niwaoga kama kunguru...walipaswa waongee na balozi siku mingi, badala yake wanaahidiwa sijui kuendeleza michezo...pua Makamba, pua Sa100
 
Serikali kama ndio iliwatafutia ufadhili na nafasi kwenda huko, tunahitaji kusikia inasemaje. mbona mataifa yote yenye mateka wametangaza? na watoto wetu wapo kule wanaona mateka wengine wanasumbukiwa ila wao serikali haiwatambui, si ukute wameshajieleza kuwa sisi ni watanzania lakini hamas wakasema hatuwaamini ngoja tusikie kwanza kama serikali yenu itawatangaza kama ninyi ni watanzania, subiri wee serikali kimya. tujifunze mataifa mengine yanavyotetea na kulinda raia wao, ndio kazi ya serikali hiyo tumewachagua kuwaweka madarakani kwa ajili hiyo.
 
problem ya viongozi rangi nyeusi huwa haijali raia wake, ata kusema kuna raia wetu wametekwa watafanya siasa ndo watangaze. serekali inatakiwa iwapiginanie raia wake ata kama ni mmoja ni muhimu sana.
 
msemaji wa serilai ameshalitamkia hilo, anataka watanzania waelewe nini, hasa ikizingatia vijana wenyewe ni wakristo.
 
Huyo Balozi ndiye alikuwa anatutaka tupaze sauti kulaani mashambulizi ya Israel huku yeye hajalaani watanzania wenzetu kuchukuliwa mateka na vijana wake.😁.
 
Huyo Balozi ndiye alikuwa anatutaka tupaze sauti kulaani mashambulizi ya Israel huku yeye hajalaani watanzania wenzetu kuchukuliwa mateka na vijana wake.😁.
miaka yote mabalozi wa palestina huwa wanatuomba watanzania tuwape sapport. nakumbuka nikiwa chuo kikuu udsm miaka ile, balozi wa palestina alikuja na MAKWAIA WA KUHENGA, mzee mmoja hivi mwenye kitambi na biased kwa wagalatia, wakatuomba kweli tuisapoti palestina na kulaani israel. miaka yote wakishambuliwa huwa wanatuomba tufanye hivyo. hata juzi aliongea. sasa, hamas wamekamata vijana wetu wawili, tena ni wakristo, tunataka tuamini kama yeye balozi wakristo kwake wanathamani na kama watanzania kwa ujumla wana thamani. la sivyo tutaamini kuwa hana shukran kwetu na pengine ameona hao ni makafir tu, na asije tena kuomba sapoti kwetu miaka ijayo.
 
mtumeni katibu wa wakatolic tanzania kitime aende israel kuomba hamas wawatoe watoto wa vigogo
 
mtumeni katibu wa wakatolic tanzania kitime aende israel kuomba hamas wawatoe watoto wa vigogo
ndugu wewe kichwa kimejaa maji tena machafu. ubongo huna. mateka wamekamatwa na magaidi na wapo kwenye mashimo ya Gaza, wewe unasema twende Israel? na iyo kauli ya "watoto wa vigogo", ni wivu wa kimasikini, unaona kama watu wakienda kusoma ni watoto wa vigogo, wewe sio wa kigogo ndio maana umepigwa na maisha. kwa taarifa yako, hao ni wanafunzi walipelekwa na serikali kama msaada kwenda kufanya internship kwenye mambo ya kilimo, ni watoto wa masikini kabisa hadi wakahitaji kusaidiw ana serikali kwenda kule.
 
Back
Top Bottom