Balozi wa Marekani nchini Tanzania atembelea Ofisi za JamiiForums

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
0EC152D9-CEEC-48AC-866B-FE2FA5A05D9A.jpeg


Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mhe. Donald Wright leo Februari 4, 2022 ametembelea Ofisi za JamiiForums na kukutana na watendaji na mwakilishi wa Bodi ya Wakurugenzi

Balozi Wright na timu yake wamepata kuelezwa namna Jamii Forums ambayo ni Asasi ya Kiraia inavyoendesha shughuli zake katika kufanya uchechemuzi wa Haki za Kidijitali, Uwajibikaji, Demokrasia na Utawala Bora nchini Tanzania

46489A6B-59E1-4D7E-A7A3-72AD056C048E.jpeg
A7570D9C-A1FD-4BCD-AE50-79259076966F.jpeg
47336557-43C4-42EC-AA6F-E2CE1D761468.jpeg


28D3BC60-38D1-4EE4-9B0B-F6B4BABBD704.jpeg
 
Haya ndo mambo yanayonipigishaga ban sasa,hapa tu kanafsi kanarukaruka niseme kuhusu mod mpiga ban..🤣

Kwa leo naacha fujo wacha nizungumzie swala kubwa niachane na maswala madogomadogo!.
Jf juu lazima tutoboe kimataifa au mnasemaje mods..?
 
Mh Balozi amekutana na viongozi wa Jf na kubadilishana nao mawili matatu , japo mpaka sasa hatukuambiwa yaliyozungumzwa .

JF Imejipatia heshima kubwa ndani ya Nchi na kwenye Jumuiya ya Kimataifa kutokana na Uhuru mpana wa kujieleza inaoutoa kwa wanachama wake , ikiwemo jambo kubwa sana lililowashinda Wengi la KULINDA FARAGHA ZA WATEJA WAKE

Mungu ibariki JF

instagram_image.jpg
 
Hakuna mzungu anaefanya jambo lake Kwa bahati mbaya.

Jf ni nzito sana na kama kumbukumbu zangu ziko sahihi kipindi cha uongozi wa Hayati Magufuli Melo alikuwa akisumbuliwa sana juu ya JF nafikiri ni Kwa sababu ya uzito wa Jf na watu wake.

Mambo ni mengi😄😄huwezi jua labda ndio baraka zenyewe.
👊🏿👊🏿👊🏿
 
Ni wazi JF inaheshimika na kutambulika zaidi ya media nyingi hapa Tanzania, sasa JF waangalie uwezekano wa kuanzisha magazeti, luninga, na radio station yao.

Hizi ziara za hawa mabalozi zinaonesha vile kizuri kinavyojiuza...
 
Nyani Ngabu, Ni mawazo yako yaliyopitwa na wakati

Unafikiri ule ubalozi wa Marekani Tanzania ulijengwa na pesa za Babu yako?

Kama Balozi hatambuliki zile chanjo za korona zilitolewa kwa msaada zilitoka Marekani au kwenye Familia yako hapo Mbezi ya Tangi bovu

Unafahamu maana ya Balozi, Balozi ni muwakilishi wa Rais Katika nchi husika

Huyo Balozi ndiye muwakilishi wa Biden hapa Tanzania, Raia wa Marekani kufahamu au kutokufahamu inategemea kama wana lengo la kuja Tanzania au kuna tukio kubwa sana Tanzania

Obama alivyofika Tanzania, alifikia nyumbani kwenu hapo Tangi bovu au alielekea kwenye ubalozi wake kwanza

Kuna watu wazima humu jamii forum lakini wana mawazo ya kipuuzi na kipumbavu sana

Mimi mtanzania sina lengo la kwenda Iraq, Syria, Somalia, Au Cambodia,. Nianze kuulizia mabalozi wa huko kwa faida gani?

Balozi ana kazi zake maalum na hapo kwenda jamii forum ana mambo anayotaka kujifunza na kuyaona ili ajiongezee maarifa na uzoefu Katika maisha yake

Wewe Nyani ngabu una mfahamu Balozi wa Tanzania huko uzebakstan? au nchi ya Tajikstan?

Sasa Mimi nimeishia huko uzebakstan na Balozi anayesimamia huko namfahamu vizuri toka Tanzania, Watu ambao hawana mpango wa kwenda huko uzebakstan wamtafute Balozi wa kazi gani?
 
Back
Top Bottom