Balozi wa Libya Tanzania akaidi kushusha bendera ya NTC!

Balozi wa Libya Tanzania akaidi kushusha bendera ya NTC!

Iwapo ataamua kupuuzia "concern" hiyo basi hakuna kinachobaki zaidi ya kumpa AMRI ya kuondoka nchini.

Acha blah blah nyingi ... la msingi ni hilo la mwisho tu. Kikwete afanye kama alivyofanya Mugabe kama ana ujasiri, ampe huyo balozi amri ya kuondoka nchini. Tukumbuke kwamba Libya ilikuwa na bendera yake na wimbo wake wa taifa toka ilipopata uhuru wake mwaka 1951 hadi 1969 Gadafi alipoongoza mapinduzi ya kijeshi dhidi ya serikali halali. Kwa miaka 42 (1969 - 2011) huyu Gadafi amekuwa Supreme Leader wa Libya na viongozi wote serikalini hawana kauli zozote zile. Alitwaa madaraka kwa upanga na sasa ameondolewa kwa upanga.
 
wandugu, naona mjadala umejaa emotions lakini turudi ktk ukweli. Sheria za Tanzania zinasema nini juu ya kubadili bendera na hasa utawala unaoingia kwa staili hii ya uasi?

Mkuu SlidingRoof ametuambia anazijua sheria lakini mpaka sasa hajatupa hivyo vipengele. Kwa kufupi balozi huwa anawakilisha taifa nasio nchi. Kama nilivyotosema kwenye post yangu hapo huu Article 3(1)(a) of the Geneva Convention ambayo tumesaini inasema kuwa "The functions of a diplomatic mission consist of representing the sending State in the receiving State." Lakini kuna watu hapa wanadhani kuwa balozi huwa anawakilisha serikali. Siwalaumu kwa vile ndio tumefundishwa hiyo dhana. Lakini sheria inasema wazi kuwa kazi za balozi ni kuiwakilisha nchi. Kwa maana hiyo serikali ikibadilika haina maana kuwa mabalozi nao wanakuwa batili.

Kuhusu bendera ni moja ya nembo za taifa. Bendera sio nembo ya serilaki. Taifa ni watu, na watu ndio wanaoamua kubadilisha nembo zao. Sasa watu wa taifa la Libya wameamua kubadilisha bendera ya taifa lao, kinachotuuma ni nini. Kwanza hata huyo balozi hajapandisha bendera mpya. Kwa matakwa ya taifa la Libya, balozi amerudisha bendara iliyokuwa inatumika zamani.

 
............. rebels must demonstrate actual independence of outside authority such as NATO, EU, etc, not the supremacy of one town over others but the independence of one state from its peers and that's why some of us argue a sovereign state is said to be in fact politically and juridically independent of any superior............

No they don't! kipimo hicho tunaweza kukitumia dhidi ya taasisi kama PLO? Kusema kuwa "sovereign state is said to be in fact politically and juridically independent of any superior" haina maana nzito kama unavyotaka kuashiria. Sovereignty exist with the people above whom there are no other superior authority. Wakati wewe unaangalia "state" as "sovereign" hoja yangu ni kuwa "wananchi ndio sovereign". Na hivi ndivyo hata Katiba yetu imeweka. The state only embeds the sovereignty of its people. The state becomes sovereign only because its people are sovereign. Ndio maana ya wananchi kudai uhuru ili wa exercise their sovereignty in their own state. Lakini hata bila kuwa na state watu bado wako sovereign mfano kama Wapalestina au hata wale wa Western Sahara.

Lakini kwenye suala la Libya, nchi ya Libya imekuwepo as a sovereign state kwa maana ya kwamba watu wake wamejipatia uhuru wa kuweza kujiamualia mambo yao. Bahati mbaya sana mapinduzi ya Libya yaliyomuingiza Gaddafi na kuung'oa utawala wa Mfalme Idris hayakuleta utawala wa kidemokrasia bali ulijaribu kumuondoa mfalme mmoja na kumuingiza mwingine kwa madai ya utawala wa Jamhuri. Lakini pamoja na utawala wa miaka zaidi ya 40 ambapo Gaddafi was the state kama yule mfalme wa Ufaransa aliyewahi kudai kuwa "The State, I am the State" wananchi wa LIbya bado walikuwa wana sovereignty yao na wakati ulipofika baada ya kutumia muda mrefu kudai haki ya kuitumia wakajikuta wanalazimika kuchukua silaha na kuwaondoa watawala dhalimu.

Sasa hii ya kusaidiwa na watu wa nje si jambo geni hata kidogo. Na wala halipunguzi uhalali wa kile kinachofanywa na NTC. Iraq imesaidiwa na mataifa ya nje, Comoro ilisaidiwa na mataifa ya nje, Bosnia vivyo hivyo hata Uganda hivyo hivyo.. as long as kwamba wanaounda NTC ni wananchi wa Libya na wamekubali kubeba madaraka ya kulirudisha taifa lao mikononi mwao hilo ni mwisho, sisi wengine tunaweza tusipende au tunaweza tungependa iwe tofauti lakini ukweli unabakia kuwa wananchi wa Libya kama wale wa Tunisia na Misri kabla yao wameamua kutumia sovereignty yao kuondoa utawala wa Gaddafi na kuanza kujenga utawala mpya. Wananchi wa Syria nao wanatumia sovereignty hiyo hiyo kwa kutumia maandamano na sijasikia watu wakiseam wale wanaouawa Syria ni Wamarekani na Wafaransa lakini ni wananchi wa Syria. Sasa wakiamua hatimaye kuchukua silaha na kuamua kumuondoa Bashir well.. tunaweza tusipende lakiniw atakuwa wameamua kutumia haki yao ya kutumia sovereignty yao kujinasua kutoka katika mikono ya utawala wa familia ya Assad.

Jamani Demokrasia ni nini kwani? Wengine wanafikiria demokrasia ni uchaguzi!!!! au vyama vingi.. its not..
 
wandugu, naona mjadala umejaa emotions lakini turudi ktk ukweli. Sheria za Tanzania zinasema nini juu ya kubadili bendera na hasa utawala unaoingia kwa staili hii ya uasi?

hazisemi chochote. Na hiyo Vienna convention (imeshaoneshwa hapo juu) haisemi balozi anamuwakilishi rais wa nchi husika au chama tawala cha nchi husika; Balozi ni mwakilishi wa nchi. Ndio maana wanaitwa "balozi wa tanzania nchini marekani au Umoja wa mataifa" haitwi "Balozi wa Rais Kikwete nchini Marekani" au "Balozi wa Gaddafi nchini Tanzania"

Na kuhusu bendera Vienna convention inasema hivi:

The mission and its head shall have the right to use the flag and emblem of the sending State on the premises of the mission, including the residence of the head of the mission, and on his means of transport.
Article 20.

Sasa sisi tunakataa vipi wakati State kule Libya chini ya NTC imeshabadilisha bendera yake? sisi tunang'ang'ania ati ooh tunatakiwa ifuate protokali.. ya kufanya nini? Hakukuwa na uchaguzi Libya kumefanyika Mapinduzi, guess what? Mapinduzi yana matokeo na matokeo yake ni mabadiliko ya ghafla ya watawala! Thats what a revolution is.. we need to catch up with it!
 
1. Rebels

Kwa hiyo you meant rebels that have attained the status of sovereign statehood? To you what is a State? Kama rebels waki attain the status of sovereign statehood, nchi ya Libya yenyewe itakuwa na status ipi? Unachanganya kati ya serikali na nchi. What should have the status of a State? The rebels or Libya?

2. The English word sovereignty originally derived from the French term souverain: a supreme ruler not accountable to anyone, except
perhaps to God.....Tazama kitabu kilichoandikwa na Ivo D. Duchacek, Nations and Men: International Politics Today ( New York: Holt,
Rinehart and Winston, 1966), p. 47.

Tupe sources za kisheria ulizodai unazo. Not books or dictionaries. Wewe mwenyewe umesema tutoe legal sources, wakati wewe unatupa secondary sources? Achana na textbook arguments ambazo nyingi ni very theoretical na hazi apply in practice. Tupe vifungu vya sheria. Under what legal basis we should not recgonise the NTC as the representative of the people of Libya?
 
LEO WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UINGEREZA AMEWASIHI WAFUASI WA GADDAFI
WAWEKE SIRAHA CHINI KABLA HAWAJACHUSHIWA MVUA YA MABOMU NA NTC
yakwamba kama NCT watawashushia mambo baada ya muda wa kujisalimisha kuisha hakuna wa kulaumiwa wa kuwazuia
maana wanaomtetea GADDAFI ni CRIMINAL kwa kuipinga serikali/mamlaka yaani NTC
hii ina ujumbe gani kwa membe.
Mimi bado na beza huu msimamo wa serikali yetu hivi ni kweli watausimamia au wanadhani hii ni issue ya NYAMONGO?
Haya ni mambo ya kimataifa na wenye VETO wakisema imepita BANA tusizuge kwamba hatujui ili na kuacha kusimamia mambo ya msingi kwa taifa
 
Swali lako ni sawa na kusema mbunge anawakilisha chama au wananchi wa jimbo. Jibu ni kwamba balozi anawakilisha nchi. Lakini nchi huongozwa na serikali. In the case of huyu balozi ndumilakuwili, je tuna uhakika gani kama hao waasi wanamtambua yeye kama mwakilishi wa nchi? Isije ikafika mahala wakaanza kupigana vita hapo ndani wakigombania nani akalie kiti cha balozi. ndio maana kuna taratibu maalum za kutambuana.

Nakubaliana na wewe kuwa balozi anawakilisha nchi lakini nchi huongozwa na serikali. Lakini hii haina maana kuwa serikali ikibadilika then na balozi anakuwa batili. Kisheria, balozi yupo pale kuwakilisha nchi. Kuhusu in case ya balozi kuwa ndumila kuwili, if that was the case then Membe angesema. Asingemtambua hata huyo balozi in the first place. Hata hivyo hataweza kutomtambua kwa vile yuko hapa kuwakilisha taifa la Libya. Kama hamtaki then asilitambue pia taifa la Libya, That will make sense.

Kama anawakilisha taifa la Libya atakuwa tuu ndumilakuwili kama anadai anawakilisha pia taifa lingine. Hatujakataa kuitambua NTC kwa vile tuna wasiwasi huyu balozi nini ndumilakuwili. Rejea sababu alizotoa Membe. Kuhusu kama tuna uhakika gani kama hao waasi wanamtambua yeye kama mwakilishi wa nchi, how come then amepandisha bendera ya waasi bila ridhaa yao? Ina maana yeye kichaa?
 
Labda tuweke pointi hii kwa namna nyingine; kwa mfano CUF au Chadema wangeshinda uchaguzi mkuu mwaka jana na Lipumba au Slaa kuapishwa kuwa Rais ina maana mabalozi wote wa Tanzania waliochaguliwa wanaacha kuwa mabalozi wa Tanzania?
 
hazisemi chochote. Na hiyo Vienna convention (imeshaoneshwa hapo juu) haisemi balozi anamuwakilishi rais wa nchi husika au chama tawala cha nchi husika; Balozi ni mwakilishi wa nchi. Ndio maana wanaitwa "balozi wa tanzania nchini marekani au Umoja wa mataifa" haitwi "Balozi wa Rais Kikwete nchini Marekani" au "Balozi wa Gaddafi nchini Tanzania"

Na kuhusu bendera Vienna convention inasema hivi:

The mission and its head shall have the right to use the flag and emblem of the sending State on the premises of the mission, including the residence of the head of the mission, and on his means of transport.
Article 20.

Sasa sisi tunakataa vipi wakati State kule Libya chini ya NTC imeshabadilisha bendera yake? sisi tunang'ang'ania ati ooh tunatakiwa ifuate protokali.. ya kufanya nini? Hakukuwa na uchaguzi Libya kumefanyika Mapinduzi, guess what? Mapinduzi yana matokeo na matokeo yake ni mabadiliko ya ghafla ya watawala! Thats what a revolution is.. we need to catch up with it!
#

Membe kama angekuwa mzalendo na mwenye kulinda heshima ya taifa letu kiasi hiki ILE NDEGE YA KIJESHI iliyotuha KIA na kuondoka na NEMBO ya taifa TWIGA na wanyama hai wengine isingetokea, au baada ya kutokea hao wanyama wangekuwa wamesharudishwa au tunajua wanarudishwa lini,
mbona hilo limemshinda? hana hta kauli kuhusu muhimu kama hilo kwa taifa lakini la ukombozi wa libya linakuwa kikwazo kwake na serikali?

serikali ya Tanzania haiwezi kuwakubali waasi maana kila siku vijana wanasema waandamane na kuiondoa kama huko libya, kwa hivyo leo wakikiri kwamba NTC ni utawala wa haki na kwa ajiri ya walibya watakua wameamsha shahuku ya vijana kuwaondoa wao pia maana ni madhalimu pia

wanachezo siasa hakuna kitu hapa , hatuzi kupinga na wahisani tena hii serikali inayotukuza wahisa kupingana nao ni ngumu hapa wanashindwa wapi pa kushika,
 
Jamani Membe naye awe anafikilia na kwenda na wakati. Hivi huyu balozi wa Libya anaona kabisa kuwa Serikali iliyomuweka madarakani haipo tena, na wameshika watu wengine na wanatoa maelekezo, sasa yeye akipinga unategemea yatakayomfika ni yapi? Automatically, ni lazima abadilike ili awe salama. Aangalieni mfano mdogo tu tuliousikia siku si nyingi zilizopita wa 'Kujivua Gamba'.

Watu wanaotakiwa kuvuliwa Gamba wengine wanaogopwa hata kuguswa kwasababu moja kubwa, kwamba wakiguswa tu; basi Serikali yote itakuwa imekumbwa na kashfa kwa jinsi hao magamba wanavyoweza kuiweka hadharani. Tusimlaumu Balozi wa Libya, hana ujanja zaid ya kufuata utawala mpya.
Membe yuko sahihi kabisa kusimamia sera zetu za mambo ya nje. Sina charge kwa sababu ya ngeleja nitachangia zaidi baadaye.
 
Nakubaliana na wewe kuwa balozi anawakilisha nchi lakini nchi huongozwa na serikali. Lakini hii haina maana kuwa serikali ikibadilika then na balozi anakuwa batili. Kisheria, balozi yupo pale kuwakilisha nchi. Kuhusu in case ya balozi kuwa ndumila kuwili, if that was the case then Membe angesema. Asingemtambua hata huyo balozi in the first place. Hata hivyo hataweza kutomtambua kwa vile yuko hapa kuwakilisha taifa la Libya. Kama hamtaki then asilitambue pia taifa la Libya, That will make sense.

Kama anawakilisha taifa la Libya atakuwa tuu ndumilakuwili kama anadai anawakilisha pia taifa lingine. Hatujakataa kuitambua NTC kwa vile tuna wasiwasi huyu balozi nini ndumilakuwili. Rejea sababu alizotoa Membe. Kuhusu kama tuna uhakika gani kama hao waasi wanamtambua yeye kama mwakilishi wa nchi, how come then amepandisha bendera ya waasi bila ridhaa yao? Ina maana yeye kichaa?

Hivi wewe una uhakika gani kama WATU WA LIBYA wanawakubali waasi? Maana mpaka sasa kitu kilicho bayana ni kwamba NATO wametumia nguvu zao za kijeshi angani na nchi kavu kuvamia Libya na kuwaingiza NTC. WATU WA LIBYA hawajatoa sauti yao. Soma hapa upate mwanga zaidi juu ya nani anayepindua serikali Libya PressTV - UK, France deploy ground troops to Libya

Chukua mfano huu: Kama mtoto anajifunza kuendesha baiskeli na ameshikiliwa kwa nyuma na yule anayemfundisha, je unaweza kumtambua huyo mtoto kama mwendesha baiskeli? Je, yule aliyemshikia nyuma akibadili mawazo nini kitatokea?

Kitu ambacho unaonyesha kutokukijua kuhusu waasi wa Libya ni kwamba waasi wa ndani hawako chini ya kundi moja. Kuna makundi mengi mbambali na kila kundi lina mtazamo wake wa jinsi ya kumove forward baada ya utawala uliopo kuanguka. Na hicho ndicho kinachofanya waingereza na wafaransa kuingiza majeshi yao ya nchi kavu ili wahakikishe kuwa wale waasi wanaprevail ni wale wanaowataka wao NATO.

Iwapo NTC itafanikiwa kuweza kuongoza Libya tutaitambua, whats the rush? Haraka ya nini?

Kuhusu kukubaliwa kwa balozi, hivi unadhani balozi awezi kufanya usanii wa kuitambua NTC hata kama NTC haimtambui yeye? then kaa karibu na watu wenye uchu wa power ndio utakapoelewa vizuri hili. Swala la yeye kubalidilisha bendera halimfanyi awe anakubaliwa at the position of balozi. Kumbuka kuwa NTC hawawezi kuwa na imani na viongozi wa Ghadaffi.
 
LEO WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA UINGEREZA AMEWASIHI WAFUASI WA GADDAFI
WAWEKE SIRAHA CHINI KABLA HAWAJACHUSHIWA MVUA YA MABOMU NA NTC
yakwamba kama NCT watawashushia mambo baada ya muda wa kujisalimisha kuisha hakuna wa kulaumiwa wa kuwazuia
maana wanaomtetea GADDAFI ni CRIMINAL kwa kuipinga serikali/mamlaka yaani NTC
hii ina ujumbe gani kwa membe.
Mimi bado na beza huu msimamo wa serikali yetu hivi ni kweli watausimamia au wanadhani hii ni issue ya NYAMONGO?
Haya ni mambo ya kimataifa na wenye VETO wakisema imepita BANA tusizuge kwamba hatujui ili na kuacha kusimamia mambo ya msingi kwa taifa

Mkuu ndio maana nimekuwa nikisema kuwa Tanzania, badala ya ku-stick kwenye politics, tungeangalia hili suala kiuchumi zaidi. Russua hawajaitambua NTC, lakini ubalozi wa Libya Moscow wameshapandisha bendera ya mpya. Serikali ya Urusi haijapinga kupinga bendera mpya kupandishwa. Unafikiri Putin ni mjina kiasi. Wachina nao hawajaitambua MTC rasmi lakini wamesema wanaheshimu the choice of the people of Libya. Unafikiri Wachina ni wajinga kiasi hicho. Jirani zetu Kenya na Rwanda wamefanya hivyo hivyo. Unafikiri wao ni wajinga kuitambua NTC? No one can see the future, yet we all must make guesses about it in order to make decisions and be better prepared for what comes our way. The guesses that we make aren't based on seeing the future, but on our knowledge and past experiences, with a little bit of insight mixed in.
 
#

Membe kama angekuwa mzalendo na mwenye kulinda heshima ya taifa letu kiasi hiki ILE NDEGE YA KIJESHI iliyotuha KIA na kuondoka na NEMBO ya taifa TWIGA na wanyama hai wengine isingetokea, au baada ya kutokea hao wanyama wangekuwa wamesharudishwa au tunajua wanarudishwa lini,
mbona hilo limemshinda? hana hta kauli kuhusu muhimu kama hilo kwa taifa lakini la ukombozi wa libya linakuwa kikwazo kwake na serikali?

nimeshangaa waandishi waliokuwepo pale walishindwa kumuuliza hili!

serikali ya Tanzania haiwezi kuwakubali waasi maana kila siku vijana wanasema waandamane na kuiondoa kama huko libya, kwa hivyo leo wakikiri kwamba NTC ni utawala wa haki na kwa ajiri ya walibya watakua wameamsha shahuku ya vijana kuwaondoa wao pia maana ni madhalimu pia

Kuna pointi hapo sana tu.. ni implication ya uamuzi huo ndio inawatisha sana.
 
Labda tuweke pointi hii kwa namna nyingine; kwa mfano CUF au Chadema wangeshinda uchaguzi mkuu mwaka jana na Lipumba au Slaa kuapishwa kuwa Rais ina maana mabalozi wote wa Tanzania waliochaguliwa wanaacha kuwa mabalozi wa Tanzania?

Sasa unachanganya mambo na unafanya hiivyo kwa makusudi. kwani Obama alivyoingia madarakani tulikataa kumtambua balozi wa marekani?

Ishu hapa ni kwamba Libya kuna vita ambayo kwa kiasi kikubwa forces za nje ya Libya yaani NATO ndio inaamua momentum inakoelekea. Mapigano bado hayajaisha. Uongozi bado haujawa stable. Waasi ambao hawako kwenye kundi moja wanadai wameshinda. Sote tunaona momentum iko kwa NTC au more accurately anti Ghadafi, ila hakuna hata mtu mmoja anayeweza kusema for certain kuwa watu wa Libya au Libya kama nchi imechagua nini.

Sisi kama nchi tumeamua kutokutambua vibaraka, ila iwapo watu wa Libya watawa-endorse hao vibaraka na tukiona inafaa kwetu tutawatambua.
 
Membe yuko sahihi kabisa kusimamia sera zetu za mambo ya nje. Sina charge kwa sababu ya ngeleja nitachangia zaidi baadaye.

Unaweza ukatulezea sera zetu za mambo ya nje ni zipi?
 
Trying to think in the other way round "HIVI SAY HUYO BALOZI WA LIBYA ANGESHUSHA HIYO BENDERA YA UTAWALA WA GHADDAFI NA BILA KUWEKA YEYOTE NI KOSA??"
 
Mkuu ambacho sikufurahishwa nacho ni SlidingRoof kumwambia Mbopo akae pembemni ili yeye mwenye uelewa wa sheria za kimataifa atufafanulie juu ya hili suala. Unfortunately, SlidingRoof does not even seem to know the difference between state recognition and government recognition. Anachanganya kati ya nchi na serikali. Kuna wengine humu wanafikiri balozi huwa anawakilisha serikali. Inasikitisha.

I never said that
 
hazisemi chochote. Na hiyo Vienna convention (imeshaoneshwa hapo juu) haisemi balozi anamuwakilishi rais wa nchi husika au chama tawala cha nchi husika; Balozi ni mwakilishi wa nchi. Ndio maana wanaitwa "balozi wa tanzania nchini marekani au Umoja wa mataifa" haitwi "Balozi wa Rais Kikwete nchini Marekani" au "Balozi wa Gaddafi nchini Tanzania"

Na kuhusu bendera Vienna convention inasema hivi:

The mission and its head shall have the right to use the flag and emblem of the sending State on the premises of the mission, including the residence of the head of the mission, and on his means of transport.
Article 20.

Sasa sisi tunakataa vipi wakati State kule Libya chini ya NTC imeshabadilisha bendera yake? sisi tunang'ang'ania ati ooh tunatakiwa ifuate protokali.. ya kufanya nini? Hakukuwa na uchaguzi Libya kumefanyika Mapinduzi, guess what? Mapinduzi yana matokeo na matokeo yake ni mabadiliko ya ghafla ya watawala! Thats what a revolution is.. we need to catch up with it!
Mkuu wangu msitake kubabaisha lugha hapa kwa vitu ambavyo viko wazi kabisa..

Marekani wanapoikataa nchi iwe Iraq au Libya kitu cha kwanza humfukuza balozi hata kama wasiyemtaka au kupingana naye ni rais wa nchi na sio wananchi wake. Vivyo hivyo nchi zote zinapofunga ubalozi hutokana na utawala uliopo na sii wananchi wa Taifa hilo hivyo balozi ambaye huchaguliwa na rais huiwakilisha nchi kulingana na utawala uliopo madarakani..

Katika swala la Libya hata sielewi watu mnataka kuharakisha kipi kama sii kuiga nchi za magharibi ambazo zinaweza vunja sheria hata kama wameziweka wao. Ni rahisi wao kudai kuitambua Libya lakini waulize kama wanaitambua Palestine? na kwa uhakika Palestine wananchi walikichagua chama na wanataka serikali yao lakini mataifa makubwa wamekataa kuitambua..

Hivyo rights walizokuwa nazo wao mataifa makubwa hata sisi na udogo wetu tunayo haki ya kutambua utawala kulingana na jinsi tunavyoona haki imesimama wapi. Na wala sii swala la kuondolewa Ghadafi ndilo liwe kipengelke cha hoja nzima kwa sababu hiki chombo NTC kimeundwa na NATO maalum kwa kuifanya transition ya madaraka nchini humo kwa hiyo tutaweza tu kuitambua Libya itakapo kuwa na utawala kamili lakini sii Mapinduzi ambayo bado hayana picha kamili ya kiutawala.

Ni rahisi sana kusema hapa kwa sababu NATO na mataifa mengine tayari wamekwisha wafuata mabwana zetu lakini sii vibaya pia kusubiri hadi hali halisi imekaa vema kuweza kuitambua serikali iliyopo madarakani. Na penmgine wengi ya wasomaji hapa JF hawafahamu kwamba waliokwenda na kuiteka Tripoli hawakutokea Bangazi bali ni pamoja na majeshi yaliyoasi kutoka magharibi ya mji wa Tripoli maili kama 100. Hawa hawana uhusiano kabisa na chama ama wanaharakati wa Bengazi.

sasa hivi majeshi hayo yameuzingira mji wa Serti na magharibi yake majeshi ya NATO pia yamejiweka tayari ikiwa wafuasi wa Ghadafi watakataa kujisamilisha. Hii ni vita ya wenyewe kwa wenyewe na hadi sasa hivi pamoja na makosa ya Ghadafi kutawala miaka 40 (kosa sijui kulingana na kifungu gani cha sheria za utawala) bado hatuwezi kubeba mzigo kwa sababu tu mapinduzi haya yamefanywa na waasi na sii wananchi wa Libya kama tulivyoona Tunisia, Misri na sasa hivi Syria bado tunasubiri Bahrain na Yemen..Haya ndio mapinduzi ya wananchi haswaaa..

Ni lazima ifahamike wazi kwamba Mapinduzi haya hayakufanywa na wananchi bali waasi ambao wamechoka na utawala dhalimu wa Ghadafi kuitawala nchi hiyo kwa ngumi ya chuma..Lakini niwajuavyo waarabu pasipo utawala wa iron fist mkuu wangu hawawezi kutawalika na nakuhakikishia kabisa kwamba Libya will be another Somalia au Iraq..just stay tuned.

Pamoja na yote hayo bado tunatakiwa kuyatambua mapinduzi haya pindi serikali mpya itakapo undwa kwani mifano yoote uloitoa kuhusu palestine, Comoro, Rwanda, Uganda na kadhalika kote kulikuwepo na chama au utawala tayari unajulikana sio hii NTC iliyoundwa na NATO kama ilivyofanyika Iraq wakati Marekani walipokuja na chombo na mtu wao kisha wakawamwaga mara tu baada ya Saadam kuondolewa... It's always on their interest na sii interest za wananchi wa nchi husika.
 
Trying to think in the other way round "HIVI SAY HUYO BALOZI WA LIBYA ANGESHUSHA HIYO BENDERA YA UTAWALA WA GHADDAFI NA BILA KUWEKA YEYOTE NI KOSA??"

Let me also be a little more realistic and try to look at it another way "kama huyo balozi angeendelea kuipeperusha bendera ya utawala wa Gadafi, Mh. Membe angeona sawa tu ?"
 
Hivi wewe una uhakika gani kama WATU WA LIBYA wanawakubali waasi? Maana mpaka sasa kitu kilicho bayana ni kwamba NATO wametumia nguvu zao za kijeshi angani na nchi kavu kuvamia Libya na kuwaingiza NTC. WATU WA LIBYA hawajatoa sauti yao. Soma hapa upate mwanga zaidi juu ya nani anayepindua serikali Libya PressTV - UK, France deploy ground troops to Libya

Chukua mfano huu: Kama mtoto anajifunza kuendesha baiskeli na ameshikiliwa kwa nyuma na yule anayemfundisha, je unaweza kumtambua huyo mtoto kama mwendesha baiskeli? Je, yule aliyemshikia nyuma akibadili mawazo nini kitatokea?

Kitu ambacho unaonyesha kutokukijua kuhusu waasi wa Libya ni kwamba waasi wa ndani hawako chini ya kundi moja. Kuna makundi mengi mbambali na kila kundi lina mtazamo wake wa jinsi ya kumove forward baada ya utawala uliopo kuanguka. Na hicho ndicho kinachofanya waingereza na wafaransa kuingiza majeshi yao ya nchi kavu ili wahakikishe kuwa wale waasi wanaprevail ni wale wanaowataka wao NATO.

Iwapo NTC itafanikiwa kuweza kuongoza Libya tutaitambua, whats the rush? Haraka ya nini?

Kuhusu kukubaliwa kwa balozi, hivi unadhani balozi awezi kufanya usanii wa kuitambua NTC hata kama NTC haimtambui yeye? then kaa karibu na watu wenye uchu wa power ndio utakapoelewa vizuri hili. Swala la yeye kubalidilisha bendera halimfanyi awe anakubaliwa at the position of balozi. Kumbuka kuwa NTC hawawezi kuwa na imani na viongozi wa Ghadaffi.

Wakati Nyeyere alivyovamia Uganda tulikuwa na uhakika gani kama watu wa Uganda waliwakubali waasi tuliowaweka madarakani? Kwa sababu kitu kilichokuwa bayana ni kuwa Tanzania walitumia nguvu za kijeshi kwa kuvamia Uganda na kuweka madarakani waasi. Kama kuna makundi mengi mbambali na kila kundi lina mtazamo wake wa jinsi ya kumove forward baada ya utawala uliopo kuanguka, naomba unitajie hayo makundi.

Hata hiyo naona kama unachanganya madesa hapa. Hivi Tumekataa kuitambua NTC kwa sababu wamesaidiwa na NATO? Ina maana kama hao rebels wasingesaidiwa na NATO tungewatambua? Maana Membe kasema hatuwatambui kwa sababu hawajaunda serikali. Sasa vipi kama walikuwa hawajasaidiwa na NATO na hawana serikali. Tungewatambua?

Kuhusu iwapo NTC itafanikiwa kuweza kuongoza Libya, then tutaitambua, so hatuna haraka, then lets wait. Lets not rush kuitambua wakati wenzetu are making deals with the new government. Sisi tusubiri tuu mpaka hizo deals zikishaisha, ndio tuwatambue. Tuji-stick zaidi kwenye siasa za kizamani wakati wenzetu wao wanangalia hili suala kiuchumi zaidi na kwa manufaa ya mataifa yao. Tuendelee kuitambua "serikali" ya shemeji yetu amabye hata hatujui alipo.

But the reality is that the policy of not recognizing governments is of sham and one that is almost impossible to apply in reality.We all know Tanzania wishes to say something about the changes occurring in Libya but not go the whole way and say that the NTC is the government. The middle position of saying something about the situation but not making a formal declaration of recognition undermines our strength and position at the international level. Eti Gaddafi kuongoza Libya imekwishafikia mwisho, lakini hatuwezi kuwatambua waasi wakati bado hawajaunda serikali. What the hell is this? Kama namna gani vipi kwa nini basi tusichukue msimano wa Venezuela? Hapo ndio ningemwona Membe wa maana.
 
Back
Top Bottom