Balozi wa Korea Kusini Nchini, Ahutubia kwa Kiswahili!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,498
113,602
Wanabodi,

Leo nimeshuhudia jambo kubwa la kuitukuza lugha yetu adhimu ya Kiswahili, pale Balozi wa Korea hapa nchini, H.E Young Ho Kim, alipopanda jukwaani na kuhutubia kwa lugha ya Kiswahili!.

Kitendo hiki sio tuu ni cha ukuzaji wa Kiswahili, bali baadhi ya wenzetu, hawako tayari kuendelea kuukumbatia ukoloni mamboleo kwa kuendeleza colonial legacy ya kuzungumza lugha ya mkoni Mwingereza!.

Kule nyuma niliwahi kuandika humu, wakoloni Waingereza wametufanya vibaya!, kwani mpaka leo ni aghlabu sana kuwasikia viongozi wetu wakizungumza lugha yetu wakiwa ugenini popote!.

Tena hutokea tukio ambalo mfadhili ni mzungu, basi hotuba zote zitasomwa kwa lugha ya mkoloni eti tuu ili mfadhili asikie, wakati huyo mfadhili angeweza kuwekewa mkalimani na waliowengi ndio wakahutubiwa kwa lugha yao!

Tuupunguze uzungu kwab kitukuza kizungu, huku ni kuendeleza ukoloni mambo leo!.

Asanteni.

Pasco
 
Mnaweza kuninukuu....Hilo haliwezekani ng'o!!

Narudia tena, Hilo haliwezekani ng'o.

Bila kuongea Kizungu hatutajulikana kama tumesoma. Hatutajulikana kama tumestaarabika. Hatutajulikana kama ni "vichwa".

Tayari tumeshaathiriwa na kuathirika vibaya kiasi cha kutoweza kujirudi.
 
Ushauri wako ni mzuri sana sana lakini ... mwafrika (hasa mtanzania) kujikomboa kwenye hili suala la lugha itahitajika nguvu ya ziada. Na kuongeza chumvi kwenye kidonda ni kuwa wasomi (ambao ndio walitakiwa wawe mashujaa wa kiswahili) ndio wanaoongoza kukidharau. Tumefikia hatua ya watu kuongea kiswahili kibovu ili tuonekane hatukijui vizuri. Hapa jamvini ukichapia kiswahili watu hawashtuki sana lakini kiingereza... mh utachekwa mpaka ujione wewe ni juha
 
Ni sera tu mkuu!! Kama tukiamua yote yanawezekana! lakini kwa sababu kila kitu tunaiga, basi hadi matumizi holela ya dola ndani ya nchi yetu ni halali wakati ukiwa nchi zingine ni kwa nadra unaweza kutumia dola bila kuibadili.
 
Mimi nasema hilo haliwezekani hadi hapo nitakapothibitishwa visivyo!!
 
Ni sera tu mkuu!! Kama tukiamua yote yanawezekana! lakini kwa sababu kila kitu tunaiga, basi hadi matumizi holela ya dola ndani ya nchi yetu ni halali wakati ukiwa nchi zingine ni kwa nadra unaweza kutumia dola bila kuibadili.

Wakoloni hawataki kusikia hii kitu mkuu. Kwao lugha ni silaha kubwa ya kuendeleza utawala wao.
Back in time, wakati Mwalimu Nyerere (PBUH) alipotangaza kuwa Kiswahili ni lugha ya taifa, wao (Waingereza) wakaenda kuimarisha viwango vya elimu kule Kenya, na kuifanya Kenya kuwa kituo cha lugha yao katika ukanda huu. Wanajua kuwa tukifanya tabadili katika sera ya lugha, itakuwa ndio mwanzo wa kuacha utegemezi katika elimu, kwa kuwa itatulazimu kuandaa wenyewe vitabu vyetu na sio kutegemea hivi vya India.
 
Wanabodi,

Leo nimeshuhudia jambo kubwa la kuitukuza lugha yetu adhimu ya Kiswahili, pale Balozi wa Korea hapa nchini, H.E Young Ho Kim, alipopanda jukwaani na kuhutubia kwa lugha ya Kiswahili!.

Kitendo hiki sio tuu ni cha ukuzaji wa Kiswahili, bali baadhi ya wenzetu, hawako tayari kuendelea kuukumbatia ukoloni mamboleo kwa kuendeleza colonial legacy ya kuzungumza lugha ya mkoni Mwingereza!.

Kule nyuma niliwahi kuandika humu, wakoloni Waingereza wametufanya vibaya!, kwani mpaka leo ni aghlabu sana kuwasikia viongozi wetu wakizungumza lugha yetu wakiwa ugenini popote!.

Tena hutokea tukio ambalo mfadhili ni mzungu, basi hotuba zote zitasomwa kwa lugha ya mkoloni eti tuu ili mfadhili asikie, wakati huyo mfadhili angeweza kuwekewa mkalimani na waliowengi ndio wakahutubiwa kwa lugha yao!

Tuupunguze uzungu kwab kitukuza kizungu, huku ni kuendeleza ukoloni mambo leo!.

Asanteni.

Pasco

Jemedari hata mimi nimefarijika kwa wewe kutoa taarifa hizi
 
pasco... mkorea kuhutubia kiswahili yaweza kuendana na mtanzania kuhutubia kizungu au kikorea

angehutubia kikorea ndio ningefananisha na sisi kuongea kiswahili

mawazo tu
 
Back
Top Bottom