Balozi wa Kiswahili Mama Salma Kikwete!?

Balozi wa Kiswahili Mama Salma Kikwete!?

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
18,344
Reaction score
31,625
Changamoto katika uandishi, mawasiliano na lugha ya Kiswahili zinatarajia kupata mwarobaini kufuatia Chama cha Lugha na Fasihi ya Kiswahili Tanzania (Chalufakita) kuwakutanisha wadau wa ndani na nje ya Tanzania mjini hapa kuzijadili na kuzipatia ufumbuzi.

Mwenyekiti wa Chalufakita, Dk Mussa Hans amesema wadau hao watakutana jijini Tanga Ijumaa wiki hii ambapo pamoja na mambo mengine mtoto wa gwiji wa Kiswahili Shaaban Robert atazungumzia historia ya baba yake.

Amesema kongamano hilo litakaloongozwa na balozi wa kwanza wa heshima wa Kiswahili Afrika na Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (Chaukidu), Salma Kikwete litafunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Othman.

Amesema katika kongamano hilo kutakuwa na makala elekezi za namna ya kuandika kwa ladha yenye kuwavutia wasomaji, wasikilizaji na watazamaji wa vyombo vya habari na machapisho mbalimbali.

"Makala hizo zitazingatia maeneo mbalimbali kama vile uandishi, mawasiliano na lugha katika elimu lakini pia kutakuwa na makala mbili mtambuka," amesema Dk Hans.

Ikbar Shaaban Robert ambaye ni mtoto wa gwiji wa Kiswahili, Shaaban Robert amesema kuwa atatumia kongamano hilo kuwakumbusha wadau jinsi baba yake alivyotoa mchango mkubwa katika kukuza Kiswahili.

"Kiswahili ni bidhaa tukitumie kukuza uchumi wa nchi yetu na kutengeneza ajira katika nchi mbalimbali zilizopania kukitumia kama lugha maalumu nchini kwao," amesema Ikbar.

Source: Mwananchi
 
Haha daah.

Huyu bibi anayesoma kama kindagateni ndio balozi??
 
 
Huyu mama hajui Hata kuzingumza hata neno moja la lugha ya malkia.
 
Amesema kongamano hilo litakaloongozwa na balozi wa kwanza wa heshima wa Kiswahili Afrika na Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini wa Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (Chaukidu), Salma Kikwete litafunguliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, Said Othman.
Ana mchango gani kwenye lugha

Labda wangempa Shibuda hiyo nafasi🤣
 
Back
Top Bottom