Hapa tulipofika siamini tena kwamba suluhisho la matatizo yetu ya ufisadi yatapatikana katika mfumo wetu wa sheria zaidi ya njia ya siasa. Haya matatizo ya BoT na mengine mengi ambayo akina Slaa hawajayafunua, hayakufanyika kwa bahati mbaya; ni mambo ambayo yalipangwa ili kufanikisha malengo mahsusi ya kisiasa. Hao waliopo katika mamlaka ya kisiasa ambao ndio wanaopaswa kuwafikisha akina Balali mahakamani wanajua jinsi hizo pesa zilivyopotea na zilivyotumika. Ni haohao ndio waliomsindikiza na pengine kumficha Balali huko aliko ili kuepusha aibu, sasa leo unaposema hawahawa ndio wampe kinga Balali ili awataje mahakamani, tunasoma vitabu au tunaongelea uhalisia?
Mimi nasema hawa wataweza tu kushughulikiana kama watagundua kwamba kusuasua kwao kutawanyima kura (kula) 2010. Vinginevyo, kama wananchi vijijini wataendelea kuwachekea na kutokuona uhusiano uliopo kati ya umaskini wao na wizi wa Bot na kwingineko, basi tujue haya majamaa yatasuasua tu hivihivi mpaka tusahau! Mbona tumeshasahau Richmond na mazira mengine kibao, kwa nini unafikiri hatutasahau hili?
Mimi tena sisemi tena "miafrika ndivyo tulivyo", sasa nasema miCCM ndivyo ilivyo. Hii mijamaa haiogopi sheria, inaogopa kunyang'anywa madaraka, henceforce the supremacy of political solution over a legal one.
Mwanakijiji,
Nadhani uko influenced sana na mfumo wa Marekani kiasi kwamba unasahu jinsi Tanzania ilivyo na inavyoendeshwa. Hayo yote unayoyasema yanafanyika na yamefanyika Marekani.
Halafu rafiki yako Kwame vipi tena? Nimezisoma txt mgsg nikacheka hadi mbavi zinauma...
Mwanakijiji,
Nadhani uko influenced sana na mfumo wa Marekani kiasi kwamba unasahu jinsi Tanzania ilivyo na inavyoendeshwa. Hayo yote unayoyasema yanafanyika na yamefanyika Marekani.
Halafu rafiki yako Kwame vipi tena? Nimezisoma txt mgsg nikacheka hadi mbavi zinauma...
Nyani, you might be right.. lakini nani hajawa influenced na dominant culture
- Tunaimba kama wamarekani (nina mifano mia moja na moja)
- Tunazungumza kama wamarekani
- TUnacheza kama wamarekani (leo ukicheza Sindimba watu wanakushangaa)
- Tunakula kama Wamarekani (nasikia siku hizi kuna hadi McD bongo, na sijui kama wanauza ugali na maharage)
- Tunavaa kama wamarekani
- Lafudhi yetu imekuwa kama Wamarekani (we angalia watangazaji wakitamka neno Dar-es-Salaam)
- Tunajenga na kutaka vitu vikubwa kama Wamarekani (siku hizi watu hawashindani uzuri wa nyumba bali ukubwa wake)
- Tumefikia mahali pa kutukana kama Wamarekani
Ila ikija kwenye kuiga mambo ya msingi tunajifanya sisi ni waafrika.
- Tenganisheni nguzo za Serikali - "hayo ni mambo ya Marekani"
- Fuateni utawala wa demokrasia - "sisi tuna demokrasia yetu ya kiafrika"
- Punguzeni nguvu za Rais - "hapana, hii ya kwetu ndiyo nzuri"
- Tumieni sheria kupambana na ufisadi - "hayo ni mambo ya kimarekani"
- Msiibe fedha za umma - "mbona hata Marekani wanaiba"
Sasa, nakubali niko influenced na Wamarekani because it works.. kwanini tusiige vitu vya msingi na vinavyofaa? Hatuona aibu kuvaa kama Wamarekani na wengine hadi vilemba vina bendera ya Wamarekani lakini ikija kwenye sheria tunang'aka!
Kama mmoja alivyosema hapa "only in Tanzania..."
labda itakuwa mara ya kwanza kwa Rais wa zamani kufunguliwa mashtaka na pengine kuswekwa lupango!!
Ben alisema "wavivu wa kufikiri", inawezekana yeye alifikiri sana na kufikia kufanya aliyofanya kwa hiyo sisi tuliochoka kufikiri anaona kama hatuwezi kumfanya kitu, labda anaota. maji ya kichemka atakuja jua tumefikiria vibaya!
Ballali angepewa Kinga..!!!