Balali apewe Kinga!

Status
Not open for further replies.

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,395
39,531
Nimejenga hoja kuwa kama kweli wanataka kukomesha mtandao wa wahalifu katika ngazi mbalimbali za serikali na utumishi wa umma, hususan kuanzia na BoT, wampe kinga aliyekuwa Gavana wa Benki hiyo Bw. Daud Balali.

Ni hoja ndefu, unaweza kuisoma kwenye Tanzania Daima. Je, serikali watakuwa tayari kumpa kinga Balali?
 
Hilo ni swali gumu sana sasa hivi kwa serikali ambayo ina wasiwasi kuwa yote waliyofanya sirini yatawekwa hadharani kesi ya Balali ikianza.

Kwa sasa nitakuwa cautious kidogo.
 
Mimi sitaki Libalali lipewe kinga kwa sababu mijizi mingine nayo itaona sawa tu kuiba ikijua kwamba itapewa kinga kuwasemea mijizi myenzie. Mimi nasema lifungwe huko Ukonga ili liwe fundisho kwa mijizi na mifisadi mingine
 
Nadhani ni wazo zuri sana kumpa kinga lakini iwe na masharti kusudi asiishie mitini na kinga hiyo huku tukiambulia patupu kuhusu fedha zetu. Kinga hiyo apewe kwa masharti kuwa atoe ukweli wote kuhusu upotevu wa pesa hizo bila kuacha neno, na atusaidie kwa kutupatia taarifa zitakazotuwezeksha kuwakamata washirika wake na kuweza kurudisha fedha hizo kutoka huko zilikopelekwa. Ingawa yeye ni mmoja wao, mimi ninaweza kumsamehe kama chambo cha kushikia mafisadi wengine 10 na kumwacha yeye mmoja. Bila kinga tunaweza kuambulia kumkamata yeye tu na kuwaacha mafisadi waliokubuhu wakiendelea kufisadi mitaani.
 
...sioni kama itasaidia chochote kwa nchi kukomesha ufisadi kwa sababu watuhumiwa wengi ni hao hao mafisadi wanaoweza kumpa kinga,mimi ninavyojua mtu anapewa kinga kama anaweza kutoa info ambayo ni critical(which is true in this case),lakini tatizo kuanzia mwizi,investigator,prosecutor ni hao hao mafisadi walioiba na wanajua kila kitu kuanzia A to Z,sasa info gani critical hapo wanahitaji zaidi ya kumuondoa huyu Balali(get out my way) ili kujisafisha...hivi mwanakiji kwa akili yako unafikiri kina JK hawajui kinachoendelea? hii issue haiendi popote na ishaisha,what happened na radar maana British katufanyia kila kitu na ushahidi katuwekea mezani tushtaki wahusika lakini tulichopata toka kwa yule fisadi mkuu wa kura na kulinda rushwa mungu anajua.
 
Unajua, tukitaka hili jambo liende vizuri ni kutaka serikali impe kingi, maana sasa hivi wametufanya yeye ndio mbaya wetu pekee na wengi tumechukizwa naye zaidi. Lakini naamini tukibadili mwelekeo na kusema Balali apewe kinga na maelezo niliyoyatoa kwenye makala hiyo utaona kuwa hawatakuwa na wa kumlaumu.

a. Wakikubali wampe kinga, watakuwa wamempa yeye kamba wakati wao watakuwa wameweka vichwa vyao kwenye vitanzi

b. Wakikataa kumpa kinga watajikuta wanaulizwa wataweza vipi kumlazimisha aseme ukweli wote.

Binafsi naamini kama fedha zilizoibiwa ni karibi trilioni moja, I'm willing to give him immunity for his involvement in the 133mln scandal in exchange for testimony on.

- EPA
-Twin Towers
-Mwananchi
- Meremeta
- Mkapa
- Mgonja
- Mramba
- Deep Green
- Meremeta
- Helikopta za Jeshi
- Rada
- n.k n.k

I think its a price we can pay. Hata FBI walipotaka kuwasambaratisha Mafia wa hapa ilibidi watoe kinga kwa baadhi ya mafioso kama kina Gotti na Selamme.

Vinginevyo goli la JK litaendelea kusimama.
 
Nadhani ni wazo zuri sana kumpa kinga lakini iwe na masharti kusudi asiishie mitini na kinga hiyo huku tukiambulia patupu kuhusu fedha zetu. Kinga hiyo apewe kwa masharti kuwa atoe ukweli wote kuhusu upotezu wa pesa hizo bila kuacha neno, na atusaidie kwa kutupatia taarifa zitakazotuwezeksha kuwakamata washirika wake na kuweza kurudihs fedha hizo kutoka huko zilikopelekwa. Ingawa yeye ni mmoja wao, mimi ninaweza kumsamehe yeye kama chambo cha kushikia mafisadi wengine 10 na kumwacha yeye mmoja. Bila kinga tunaweza kuambulia kumkamata yeye tu na kuwaacha mafisadi walikubuhu wakiendelea kufisadi mitaani.

...good point,lakini swali nani wa kumpa kinga(not theoritical)?
 
Unajua, tukitaka hili jambo liende vizuri ni kutaka serikali impe kingi, maana sasa hivi wametufanya yeye ndio mbaya wetu pekee na wengi tumechukizwa naye zaidi. Lakini naamini tukibadili mwelekeo na kusema Balali apewe kinga na maelezo niliyoyatoa kwenye makala hiyo utaona kuwa hawatakuwa na wa kumlaumu.

a. Wakikubali wampe kinga, watakuwa wamempa yeye kamba wakati wao watakuwa wameweka vichwa vyao kwenye vitanzi

b. Wakikataa kumpa kinga watajikuta wanaulizwa wataweza vipi kumlazimisha aseme ukweli wote.

Binafsi naamini kama fedha zilizoibiwa ni karibi trilioni moja, I'm willing to give him immunity for his involvement in the 133mln scandal in exchange for testimony on.

- EPA
-Twin Towers
-Mwananchi
- Meremeta
- Mkapa
- Mgonja
- Mramba
- Deep Green
- Meremeta
- Helikopta za Jeshi
- Rada
- n.k n.k

I think its a price we can pay. Hata FBI walipotaka kuwasambaratisha Mafia wa hapa ilibidi watoe kinga kwa baadhi ya mafioso kama kina Gotti na Selamme.

Vinginevyo goli la JK litaendelea kusimama.

....mwanakijiji safi sana na umefikiria kama Bob kennedy alipokuwa anawamaliza mafia,na ninakubaliana na wewe kwa hiyo exchange ya 133bn ili kujua ukweli kuhusu trillion,sure it does make sense lakini still naona JK kwa kumuweka juzi Mgonja tena BOT board huoni kama hiyo ni message sent...tumekwisha labda next president sio huyu mmachinga!
 
Kujibu swali lako, Mwanasheria Mkuu na IGP wanaweza kutoa kinga kwa Balali kwa kutumia sheria ya Uhujumu Uchumi na Organized Crime ya 1984...
 
Mimi sitaki Libalali lipewe kinga kwa sababu mijizi mingine nayo itaona sawa tu kuiba ikijua kwamba itapewa kinga kuwasemea mijizi myenzie. Mimi nasema lifungwe huko Ukonga ili liwe fundisho kwa mijizi na mifisadi mingine

Mkuu wangu MMJ,

Wossap mkuu? Huko kuna nini kinaendelea mpaka umekuwa apaologist wa Balali kiasi hiki? Kinga gani anapewa mwizi aliyetuibia na kusababisha vifo vya watoto, wazee, vilema kwa kukosa dawa kutokana na mihela aliyochota? I do not care kuhusu wengine arudi yeye kwanza bongo kujibu mashitaka yake, ama sivyo abaki huko huko asituletee balaa bure!

Hakuna kinga hapa, hatunayo kwenye sheria zetu, huko US na Kennedy wanayo hiyo kinga kwenye sheria zao, sisi bongo hatuna na hatuihitaji, kwa sababu ripoti iko very clear nani ameiba na nani hakuiba, Idd Simba, Mbilinyi, na Ngasongwa walipoiba walikamatwa na kulazimishwa kujiuzulu hatukutumia kinga yoyote, sasa iweje leo maneno ya Ballali, yalete kinga? The ripoti is very clear kuwa Mgonja, Mramba, Meghji, wanahusika na huo wizi, sasa kinga ya nini? I can understand kilio cha kutolewa full report kwa public, lakini sio maneno ya kinga, mwambieni hakuna kinga hapa, ni yeye kujibu mashitaka yatakayomsibu,

Mkuu Nyani, ahsante kwa mchango mzito hapo juu, hatutaki kinga hapa, kwa sababu wezi wote tunawajua tayari ni kina nani, kamata wote halafu weka pale Sanamu Monument mmoja baada ya mwingine kila siku saa kumi jioni, tangazia wananchi halafu weka risasi 50, ambazo ni lazima zilipiwe na familia zao ili wasituletee hasara zaidi wakiwa wanalipa malipo ya halali ya wizi wao, hiyo ndio the only kinga tunaweza kuwa-offer, ni kuwatwanga shaba tu enough, au abaki huko huko lakini hatuwezi kupangiwa na mwizi what to do!
 
Aisee kwa jinsi bongo inavyoendeshwa hili la kumpa kinga Balali ni njozi tu. Sasa yeye akipewa amtaje kila mtu kuanzia Mkapa, Kikwete, let's say baadhi ya majaji, mwanasheria mkuu, IGP...hivi mnadhani kuna lolote la substance litakalotokea kweli? Bongo watu hawali wenyewe bwana. Tandabui la mafisadi ni kubwa na pana mno. Nyie fikirieni, kama jambo lisilo na utatanishi kama la mgongano wa kimaslahi la Mkono (Mb) kumtetea Ditopile au Balali hamna aliyelipigia kelele mnatarajia nani ampe kinga Balali amwage maharage....tuendeleeni kuota tu kwani wakati mwingine ndoto hutimia.
 
Mkuu wangu MMJ,

Wossap mkuu? Huko kuna nini kinaendelea mpaka umekuwa apaologist wa Balali kiasi hiki? Kinga gani anapewa mwizi aliyetuibia na kusababisha vifo vya watoto, wazee, vilema kwa kukosa dawa kutokana na mihela aliyochota? I do not care kuhusu wengine arudi yeye kwanza bongo kujibu mashitaka yake, ama sivyo abaki huko huko asituletee balaa bure!

Hakuna kinga hapa, hatunayo kwenye sheria zetu, huko US na Kennedy wanayo hiyo kinga kwenye sheria zao, sisi bongo hatuna na hatuihitaji, kwa sababu ripoti iko very clear nani ameiba na nani hakuiba, Idd Simba, Mbilinyi, na Ngasongwa walipoiba walikamatwa na kulazimishwa kujiuzulu hatukutumia kinga yoyote, sasa iweje leo maneno ya Ballali, yalete kinga? The ripoti is very clear kuwa Mgonja, Mramba, Meghji, wanahusika na huo wizi, sasa kinga ya nini? I can understand kilio cha kutolewa full report kwa public, lakini sio maneno ya kinga, mwambieni hakuna kinga hapa, ni yeye kujibu mashitaka yatakayomsibu,

Mkuu Nyani, ahsante kwa mchango mzito hapo juu, hatutaki kinga hapa, kwa sababu wezi wote tunawajua tayari ni kina nani, kamata wote halafu weka pale Sanamu Monument mmoja baada ya mwingine kila siku saa kumi jioni, tangazia wananchi halafu weka risasi 50, ambazo ni lazima zilipiwe na familia zao ili wasituletee hasara zaidi wakiwa wanalipa malipo ya halali ya wizi wao, hiyo ndio the only kinga tunaweza kuwa-offer, ni kuwatwanga shaba tu enough, au abaki huko huko lakini hatuwezi kupangiwa na mwizi what to do!

Asante kwa kunielewa mzee mwenzangu. Kama ulivyosema, ni kweli wezi tunawajua. Hata Balali akiamua leo ayataje hayo majina hatutashangazwa na jina lolote. Sasa kama tunawajua yeye kinga ya nini? Hivi ni jina gani jipya ambalo hatulijui kuwa ni la fisadi?
 
Mwizi umpe kinga for what? Wezi wote wanajulikana kwani hakuna benki inayotoa pesa bila kuwa na kumbukumbu. JK anawafahamu wote pamoja na yeye mwenyewe kukomba pesa ya walipa kodi kwa kutumia mlango wa CCM.

Hakitoki kitu hapa anachotakiwa kufanya rais wa Jamuhuri ni kuwawezesha vyombo vya dola kufungua mashitaka kwa hawa vibaka. Time is coming and very soon even himself won't be safe.
 
Kwenye hii shughuli tutaanza na Mkapa, and the rest wata-follow hakuna haja ya kinga maana wezi wote tunawajua tayari, Balali arudi na kubeba mzigo wake tu, hatutaki ya wengine maana tunawajua na ushahidi upo wa kutosha!

tutaenda kuanzia Mbezi, Kunduchi Beach, Msasani, na Obey!
 
Hoja ya Mzee Mwanakijiji theoreticaly inawezekana lakini practicaly haiwezi kufanya kazi mkuu mwana wa kijiji. Ni nani anayetakiwa kumpa kinga na anayempa kinga anamikono misafi kiasi gani hadi ampe kinga? Hivi akishapewa Kinga na akisema kuwa hakuna uwizi kama msimamo wake ulivyo hadi sasa maana hajatoa statement yeyote kuhusu tuhuma dhidi yake mwenyewe na inawezekana msimamo wake ni kuwa yeye ni clean. Kumbuka hadi sasa Balali hakufukuzwa kazi kwa sababu kaiba bali kwa sababu ya malipo feki ambayo inawezekana ni kweli aliambiwa pesa itoke kwaajili ya usalama wa Taifa (CCM).

Mzee mwanakijiji hii hoja mkuu haitafanya kazi kwa mazingira ya Tanzania. Yaani umpe Kinga balali ili umhukumu Mkapa ambaye mkuu wa nchi alishasema aachwe apumzike kwa amani? Hawawezi kufanya kitu kama hicho kabisa mkuu. Any way ni mawazo yako hayo mkuu lakini hatuwezi linda Fisaidi ili uwakamate mafisadi kwa kutumia mafisadi. Hii ni team moja mkuu na wote wanacheza kama viungo na washambuliaji dhidi ya wanaopinga ufisadi.
 
Mwanakijiji kashashikishwa kitu kidogo na Balali, bado kujiunga na "Mkono Advocates" tu.

Kinga ya nini? Atakayempa kinga anaweza kumpa kinga kwa sababu moja tu.Kuvuruga ushahidi na kuwapata vikambale vidogo visivyohusika wakati mipapa inadunda.

Tena Mwanakiji wala usianze kuwapa ideas bure.
 
Mwanakijiji,
Kwa kweli point unayosema ni nzuri sana. Lakini pia, asemacho Field Marshall ES na wengineo, vinaleta maana (wezi lazima waadhibiwe).

Baada ya kufikiria sana, nimeona kuwa japo Ballali ni fisadi mkubwa, lakini yeye alikuwa conduit ya mafisadi wakubwa zaidi yake kufanya ufisadi. Tunaweza tumfunge naye akakaa kimya huku kina Jeetu, Mgonja etc wakawa wanapeta, wakamwekea kidogodogo chake kwenye USB Bank huko Geneva na by the time anatoka, pesa itakuwa kubwa kiasi cha kumfanya yeye na watoto wake wasifanye kazi tena.

Binafsi, naona Ballali ni samaki mdogo. And we all now, we can let the small fish go to catch the big one. Lakini yeye Ballali, asiwe let go completely, alindwe kisha aende Ukonga for a couple of years! That is, if he cooperates.
 
Mwanakijiji kweli hapa una hoja nzito lakini ebu niichambue kidogo kisha nitoe pendekezo:

Assumption 1.
I.Vyombo mbalimbali vya habari, baadhi ya Asasi zisizo za kiserikali na baadhi ya watu tunadhani kuwa Balali hakuhujumu BOT na Taifa yeye pekee. Yaani alishirikiana au alilazimishwa kuchota (kiufundi au hali akijua) toka chunguni na Wakuu fulani wa juu nchini.

Assumption 2.
Balali sasa anataka kuweka rekodi zote katika hali ya ukweli na usahihi ili Watanzania na Walimwengu wajue kilijojili ndani ya BOT.

Assumption 3.
Hao wakuu fulani wa juu nchini kwa kutumia mamlaka na uwezo wao wanaweza kumdhuru ikiwa ni sehemu ya kumkomoa na kumnyamazisha chini ya kanuni ya jino kwa jino endapo watabaini kuwa yuko katika harakati za kuwataja au kueleza hiyo kweli inayowahusu.

Assumption 4.
Kwa vile Balali ana taarifa nyeti zinazotakiwa kutolewa kwa faida ya umma wa watanzania na dunia kwa ujumla, basi anastahili kupewa kinga ya namna moja au nyingine dhidi ya maadui zake ili asidhulike, aweze kuisaidia sheria kurejesha mego la hicho kitumbua cha Taifa na pia kuwafikisha watuhumiwa wote kwenye haki itakayowazawadia wanachopaswa kupata.

Kama assumptions zote hapo juu ni kweli,

1. Basi kinga yake haiwezi kutolewa na hao hao wakuu fulani wa juu nchini maana HAKUNA WATU WANATOA KINGA DHIDI YA ADUI YAO ILI AWAMALIZE ISIPOKUWA KAMA NI WAFUASI WA KANUNI YA UKIPIGWA SHAVU LA KUSHOTO MPE NA LA KULIA NA HIVYO WASINGEKUWA MAADUI ZAKE (in the first place) KWA ANALOTAKA KULIFANYA.

2. HIVYO; KAMA BALALI NI MKWELI BASI KINGA HALISI YA KWANZA ANAYO BALALI MWENYEWE. NAYO NI KUTAMKA ANACHOJUA SASA WAZIWAZI POPOTE ALIPO NA SI KUSUBIRI KESHO NA ASEME AU AANDIKE KUWA YUKO TAYARI KUREJEA NA KUTOA USHAHIDI KATIKA MAHAKAMA KWA MASHARTI YA KUPEWA KINGA PENGINE NA ASASI NYINGINE (INDEPENDENT)YA KIUSALAMA YA NJE ISIYOHUSIKA KABISA KATIKA SAGA HILI.

MPAKA ATAKAPOTOKA HADHARANI WAZIWAZI MIMI BINAFSI NINA MWELEKEO WA DHANIO LIFUATALO:

BALALI NA MAGAVANA WENZAKE WALIOTANGULIA WALISHINDWA WENYEWE KUAJIBIKA IPASWAVYO KAMA WATENDAJI WAKUU WA BOT. HIVYO HANA WA KUMNYOOSHEA KIDOLE ISIPOKUWA KUKAA KIMYA NA KUSUBIRI WATU WASAHAU KAMA WINGU LIPITALO. NA KWA HILI MAADUI ZAKE SASA NI SISI RAIA WOTE WAPENDA AMANI NA HAKI MAANA MTU HUWEZI KUTUHUMIA YA KIZUSHI UKAENDELEA KUKAA KIMYA KIASI HICHO HALAFU UKATEGEMEA WATU WAKUFIKIRIE NAMNA YA KUKUPA KINGA.

Mwanakijiji naheshimu mchango wako lakini hapa naomba ufikirie tena na ikiwezekana umfuate Balali alipo na kumuuliza maswali ya wananchi kupitia International KLH News maana inasikika pande zote za dunia na hapendwi mtu hapo!

[9:4] If the idol worshipers sign a peace treaty with you, and do not violate it, nor band together with others against you, you shall fulfill your treaty with them until the expiration date. GOD loves the righteous.
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom