Bakwata yataka ustahimilivu viongozi wa dini

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,825
Reaction score
24,481
Bakwata yataka ustahimilivu viongozi wa dini

Mwandishi Wetu

BARAZA Kuu la Waislam (Bakwata), limewataka waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu na madhehebu mengine nchini kuendelea kustahimiliana katika mustakabali mzima wa maendeleo ya taifa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, jana jijini Dar es Salaam, Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban Simba alisema, ustahimilivu ni suala la msingi sana na hasa kwa kuwa tangu nchi imepeta uhuru kumekuwapo tabia njema ya kuvumiliana bila kujali dini ya mtu.

"Watanzania tunatakiwa tuendeleze tabia ya uvumilivu na kuwatazama viongozi hao si kwa dini bali kwa uadilifu na utendaji wa kuwatumikia wananchi,"alisema.
Aliendelea, " tunawaomba Watanzania waendelee kuwa wastahamilivu kwa sababu nchi hii tunaiendesha kwa kuvumiliana."

"Tusiwatazame viongozi kwa dini zao na tunaomba linapotokea jambo linalohitaji kukosoa kiongozi basi busara itumike na wala siyo jazba, kejeli au dharau," alisema.

Katika taarifa hiyo, Mufti Simba alisema kuvumiliana na kustahimiliana kwa madhehebu mbalimbali Tanzania ndiyo nguzo ya amani na utulivu ambao umedumu tangu taifa lipate uhuru wake mwaka 1961.

"Tunaombeni ndugu zetu Watanzania tuendelee ta tabia njema ya kuvumiliana ili tuendeleze mustakabali mwema wan chi yetu,"alisema Mufti.

NOTES: Mufti ameonyesha kuwa mtu mwenye busara sana kuliko Masheikh wotee waliokuwa wakitoa matamko siku za hivi karibuni. Hivi
matamko hayo yaliyotolewa na waislamu siku za nyuma hayakuwa na baraka za BAKWATA? Na kama yalikuwa na baraka za BAKWATA, ujumbe huu wa Mufti unawalenga nani zaidi. Kwa vyovyote hauwalengi maaskofu kwa vile wao walikosoa serikali na wala hawakutamka lolote kuhusu dini ya kiislamu, ila matamko ya mashehe ndiyo yalikuja na kushambulia dini za kikristo hasa katoliki.

Wao tu BAKWATA na rushwa ya pilau ya siku moja kwa Kikwete ikulu na kujichagulia kuweka tintedi kwa kila jambo la msingi kwa maslahi ya taifa.
 
it is confusing!! Cha msingi ni watanzania na utanzania kwanza, haya ya dini baadae!! umoja ni nguvu ndo tutaweza kuondo wazungu weusi na mafisadi-bila hivyo,tanzania na watanzania itaishia kuzama kwenye lindi la umaskini usio mwisho.
 
Utakuwepo ustahimilivu wakati bado wanaendesha mihadhara kupitia radio imaan?
 
Jamani lazima tuheshimu maneno ya hekima ya shekhe mkuu. Alichoongea ni sahihi kabisa. Sisi kama wananchi wa kawaida tunaheshimu na kuiamini BAKWATA tu. Hivyo vikundi vingine vya waislam ndivyo vinavyohongwa plate moja ya pilau na kuanza kubwabwaja kwenye mihadhara isiyo na mbele wala nyuma.

Asante shekhe mkuu kwa hekima zako.
 
Hivi central thing ya mambo ya uisilamu ni nini yaani chombo kikuu? is it BAKWATA ama? kwani nasikia matamko from everywhere sasa sijui chombo kikuu ni kipi
 
UISLAMU umegawanyika kimadhehebu, kwa mfano kuna ANSWAAR, IBAADHI, SUNNI WAL-JAMAA, SHIA, QADIANI, ISMAILI etc. Kifupi ndani ya uislamu umegawanyika madhehebu 73, ndani ya TANGANYIKA chombo cha Bakwata ndicho kinachotambuliwa na serikali katika kusimamia mambo yote halali ya kiislamu, papo hapo kuna chombo kingine kiitwacho BARAZA KUU...hawa nao wananguvu kubwa kuliko bakwata ila hawatambuliwi rasmi na serikali...hawa ndio WANAHARAKATI WAKUU WA UISLAMU NCHINI.
 
Unajua kuna vyombo vingi kwa waislam. BAKWATA ni kimoja na vigine ambavyo viko kwenye level moja na BAKWATA ni BARAZA KUU LA JUMUIYA NA TAASISI ZA KIISLAM. Sasa kwa maelezo ya waislam wanaona kama BAKWATA haipo kwa ajili yao kwani wanasema iliundwa na NYERERE baada ya kuivunja EAST AFRICAN MUSLIM WELFARE SOCIETY miaka ya 1978 au 1979 hivi ambayo wanaamini ilikuwa na msaada mkubwa kwao . Hivyo waislam walio wengi hawataki hata kuisikia BAKWATA.Wanaamini kuwa BAKWATA inaendeshwa na serikali kwa mtaji huo haiwezi kukinzana na boss wake hata mara moja kule kukinzana kwa dhati.
 
Jamani lazima tuheshimu maneno ya hekima ya shekhe mkuu. Alichoongea ni sahihi kabisa. Sisi kama wananchi wa kawaida tunaheshimu na kuiamini BAKWATA tu. Hivyo vikundi vingine vya waislam ndivyo vinavyohongwa plate moja ya pilau na kuanza kubwabwaja kwenye mihadhara isiyo na mbele wala nyuma.

Asante shekhe mkuu kwa hekima zako.
Asante sana mku kwa kunijuza hilo na tangu dakika hii tu ndio na-update data zangu juu ya vikundi gani vinavyohongwa pilau na rais Kikwete pale Magogoni na kuchangia kuwachafua ndugu zetu Waislamu na Uislamu dini ya amani na upendo kutoonekana hivyo nchini.
 
Katika dini ambazo brainwashing ni sehemu ya Ibada zao ni UISLAMU. Nyingine ni hizi "mpya" za kikristo za akina Kakobe, Mwingira, Mzee wa Upako,.....Ni vizuri Viongozi wa dini hizi wakawa makini kwenye kauli na matendo yao.
 
Nadhani sasa ni muda muafaka wa kuandaa tamko la waumini wa dini za asili za kiafrika. Inaonekana hawa waislaam na wakristo wanadhani nwapo wao peke yao nchini.
 
Afadhali wamepatikana viongozi wa kiislam wenye busara kama hawa.
 
[
NOTES: Mufti ameonyesha kuwa mtu mwenye busara sana kuliko Masheikh wotee waliokuwa wakitoa matamko siku za hivi karibuni. Hivi
matamko hayo yaliyotolewa na waislamu siku za nyuma hayakuwa na baraka za BAKWATA? Na kama yalikuwa na baraka za BAKWATA, ujumbe huu wa Mufti unawalenga nani zaidi. Kwa vyovyote hauwalengi maaskofu kwa vile wao walikosoa serikali na wala hawakutamka lolote kuhusu dini ya kiislamu, ila matamko ya mashehe ndiyo yalikuja na kushambulia dini za kikristo hasa katoliki.
[/COLOR][/QUOTE]

Iko wazi kabisa CHADEMA = UKATOLIKI
 
Mbona sijasikia hawa viongozi wa dini ya kiislam
wakitetea maslahi ya taifa mfano
kupinga hadharani malipo ya dowans? Na
na kupiga vita ufisadi?
Wao wako upande wa watawala au wananchi?
 
They don't stand kwa interests kama hizo, kilichopo kwao ni DHULMA TU.
 
Bakwata yataka ustahimilivu viongozi wa dini

Mwandishi Wetu

BARAZA Kuu la Waislam (Bakwata), limewataka waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu na madhehebu mengine nchini kuendelea kustahimiliana katika mustakabali mzima wa maendeleo ya taifa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, jana jijini Dar es Salaam, Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban Simba alisema, ustahimilivu ni suala la msingi sana na hasa kwa kuwa tangu nchi imepeta uhuru kumekuwapo tabia njema ya kuvumiliana bila kujali dini ya mtu.

"Watanzania tunatakiwa tuendeleze tabia ya uvumilivu na kuwatazama viongozi hao si kwa dini bali kwa uadilifu na utendaji wa kuwatumikia wananchi,"alisema.
Aliendelea, " tunawaomba Watanzania waendelee kuwa wastahamilivu kwa sababu nchi hii tunaiendesha kwa kuvumiliana."

"Tusiwatazame viongozi kwa dini zao na tunaomba linapotokea jambo linalohitaji kukosoa kiongozi basi busara itumike na wala siyo jazba, kejeli au dharau," alisema.

Katika taarifa hiyo, Mufti Simba alisema kuvumiliana na kustahimiliana kwa madhehebu mbalimbali Tanzania ndiyo nguzo ya amani na utulivu ambao umedumu tangu taifa lipate uhuru wake mwaka 1961.

"Tunaombeni ndugu zetu Watanzania tuendelee ta tabia njema ya kuvumiliana ili tuendeleze mustakabali mwema wan chi yetu,"alisema Mufti.

NOTES: Mufti ameonyesha kuwa mtu mwenye busara sana kuliko Masheikh wotee waliokuwa wakitoa matamko siku za hivi karibuni. Hivi
matamko hayo yaliyotolewa na waislamu siku za nyuma hayakuwa na baraka za BAKWATA? Na kama yalikuwa na baraka za BAKWATA, ujumbe huu wa Mufti unawalenga nani zaidi. Kwa vyovyote hauwalengi maaskofu kwa vile wao walikosoa serikali na wala hawakutamka lolote kuhusu dini ya kiislamu, ila matamko ya mashehe ndiyo yalikuja na kushambulia dini za kikristo hasa katoliki.

HATIMAYE JK AOMBA MSAMAHA KWA MAASKOFU BAADA YA UBISHI WA MUDA MREFU,..NA BADO MPAKA ATAWANGUKIA MWENYEWE ACHA SASA HIVI ALIVYOWATUMIA BAKWATA KUOMBA MSAMAHA...KWA HIYO MASHEIKH WAMESHINDWA VITA,WAMESURRENDER...bakwata kweli wasanii leo wanawatukana maaskofu kesho wanawomba msamaha indirectly..kikwete..you suck
 
Back
Top Bottom