Bakwata yataka ustahimilivu viongozi wa dini

11th January 2011 09:49 PM #1
Gurudumu
  • profile.png
    View Profile
  • forum.png
    View Forum Posts
  • message.png
    Private Message
  • article.png
    View Articles
user-online.png

JF Premium Member
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_pos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png
reputation_highpos.png



icon1.png
Wanaojiita BAKWATA Arusha ni mavuvuzela?


Habari za uhakika kutoka uongozi halali wa BAKWATA Arusha na Mufti Mkuu Dar, zinasema waliolaumu Chadema na kutambua Meya wa Arusha ni BAKWATA vuvuzela. Siyo viongozi halali wa BAKWATA, ni wahuni watoto wa familia moja ya mzee Mkindi ambao wamekula dili na ccm na polisi​
 
Bakwata yataka ustahimilivu viongozi wa dini




Mwandishi Wetu

BARAZA Kuu la Waislam (Bakwata), limewataka waumini wa dini za Kikristo na Kiislamu na madhehebu mengine nchini kuendelea kustahimiliana katika mustakabali mzima wa maendeleo ya taifa.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, jana jijini Dar es Salaam, Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban Simba alisema, ustahimilivu ni suala la msingi sana na hasa kwa kuwa tangu nchi imepeta uhuru kumekuwapo tabia njema ya kuvumiliana bila kujali dini ya mtu.

“Watanzania tunatakiwa tuendeleze tabia ya uvumilivu na kuwatazama viongozi hao si kwa dini bali kwa uadilifu na utendaji wa kuwatumikia wananchi,”alisema.
Aliendelea, “ tunawaomba Watanzania waendelee kuwa wastahamilivu kwa sababu nchi hii tunaiendesha kwa kuvumiliana.”


“Tusiwatazame viongozi kwa dini zao na tunaomba linapotokea jambo linalohitaji kukosoa kiongozi basi busara itumike na wala siyo jazba, kejeli au dharau,” alisema.

Katika taarifa hiyo, Mufti Simba alisema kuvumiliana na kustahimiliana kwa madhehebu mbalimbali Tanzania ndiyo nguzo ya amani na utulivu ambao umedumu tangu taifa lipate uhuru wake mwaka 1961.

“Tunaombeni ndugu zetu Watanzania tuendelee ta tabia njema ya kuvumiliana ili tuendeleze mustakabali mwema wan chi yetu,”alisema Mufti.


NOTES: Mufti ameonyesha kuwa mtu mwenye busara sana kuliko Masheikh wotee waliokuwa wakitoa matamko siku za hivi karibuni. Hivi matamko hayo yaliyotolewa na waislamu siku za nyuma hayakuwa na baraka za BAKWATA? Na kama yalikuwa na baraka za BAKWATA, ujumbe huu wa Mufti unawalenga nani zaidi. Kwa vyovyote hauwalengi maaskofu kwa vile wao walikosoa serikali na wala hawakutamka lolote kuhusu dini ya kiislamu, ila matamko ya mashehe ndiyo yalikuja na kushambulia dini za kikristo hasa katoliki.

Kwanza awaambie wajahidina wenzie ambao wanatumika na na huyo Kikwete kufunika makashfa waache matamko yao ya chuki dhidi ya dini ya kikristo. kila tamko lao lazima lioneshe chuki dhidi ya ukristo. Lini ulisikia wakristo wakiwabeza waislamu. Au lini ulisikia Maaskofu wakitoa tamko la kuwabeza mashehe. Ila wao ndo kila siku matamko ya chuki.
 
Jamani mimi naomba kueleweshwa tu( sio kubeza) bila shaka kiongozi mkuu wa waislamu hapa Tanzania ni Mufti sheikh Shaban Simba, sasa naomba mwenye kujuwa mkuu wa waislamu dunia mzima ni nani? na ni wapi makazi yake? waismailia namjuwa mkuu wao ni Aga Khan na anaishi ufaransa, sasa hawa waislamu ambao wanaotoa matamko ya kilevi kila siku ni nani mkuu wao wa dunia mzima? maana nimejitahidi kufuatilia waislamu wa madhehebu yenye admistration nzuri mambo yao yako supa kabisa na hawana makelele yasiokwisha kila siku.
 
Back
Top Bottom