Kwa Maelezo ya Omary Nzowa ni kwamba EAMWS ilianzishwa na Aga Khan. Jee kuna ukweli wowote katika hili. Lakini nyongeza kwa swali la
Proved na
platozoom inakuwaje Waislamu wa Kenya na Uganda hawakuendelea na EAMWS baada ya shirikisho hilo kupigwa marufuku Tanganyika?
Allen,
Kwani taaasisi ikiwa imeanzishwa na
Aga Khan ndiyo ipigwe marufuku?
Tuna taasisi nyingi nchini za Kikristo zilizoanzishwa na Wazungu kama
hizo hapo chini:
White Fathers (Tabora, Karema, Kigoma, Mbeya, Mwanza na Bukoba);
Holy Ghost Fathers (Morogoro na Kilimanjaro); Benedictine Fathers
(Peramiho na Ndanda); Capuchin Fathers (Dar es Salaam); Consolata
Fathers (Iringa na Meru); Passionist Fathers (Dodoma); Pallotine Fathers
(Mbulu); Maryknoll Fathers (Musoma); na Rosmillian Fathers (Iringa).
Mbona haya makanisa ya Wazungu hayakubughudhiwa na haya ni kutoka
mataifa mengi ya Ulaya?
Shida iwe
Aga Khan peke yake?.
Sasa miaka 50 Waislam wameuliza swali hili na wahusika hawajatoa jibu
mnakuja nyie akina
Allen kwetu sisi Waislam na maswali ya vichekesho.
ati mnataka kujua EAMWS ya Kenya na Uganda.
Mambo kama haya ndiyo maana kwa miaka 50 Waislam tumeipuuza
BAKWATA na hao
BAKWATA wanajua kama tumewapuuza.
Ndiyo sababu siku zote utawasikia viongozi wa
BAKWATA wanajinasibisha
na Waislam.
Hujapata kusikia Waislam wanajinasibisha na
BAKWATA.