BAKWATA yaishauri Serikali ifafanue mashaka katika Mkataba wa Uwekezaji wa bandari

Orketeemi

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
4,315
10,017
Baraza la Waislamu Tanzania limeitaka Serikali kufafanua maeneo yanayotiliwa shaka kuhusu uwekezaji bandari.

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Nuru Mruma ametoa wito kwa Serikali kupokea maoni ya wananchi kuhusu sakata la Bandari, huku akiitaka ifafanue maeneo yote yanayotiliwa shaka.

Hayo ameyasema leo Alhamis Juni 29, 2023 akihutubia Baraza la Eid El-Adh'haa lililofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco jijini hapa.

"Pia Serikali inapaswa kutoa elimu kwa wananchi ili waendelee kuuelewa mradi huu (uwekezaji bandari)," amesema.

Mruma amesema kubainika kwa mradi huo kuliibua mjadala na taharuki kwa wananchi ambao hawakuwahi kuwa na taarifa sahihi kuhusu mradi huo.

Mruma ameitaka Serikali kupokea maoni ya wananchi na kutoa ufafanuzi kwenye maeneo yote yanayotiliwa mashaka.

Hiyo ni kauli ya kwanza kutoka Bakwata tangu uanze mjadala baada ya Serikali kusaini mkataba wa awali wa ushirikiano wa uwekezaji na uboreshaji bandari na Serikali ya Dubai kupitia kampuni ya Dubai Port World.
 
Waziri mkuu kasha fafanua vizuri sana, kumbe hatukujua tulikua tunapotoshwa tu, hu wekazaji ni mzuri kwa bandari zetu.
 
Baraza la Waislamu Tanzania limeitaka Serikali kufafanua maeneo yanayotiliwa shaka kuhusu uwekezaji bandari.
Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Nuru Mruma ametoa wito kwa Serikali kupokea maoni ya wananchi kuhusu sakata la Bandari, huku akiitaka ifafanue maeneo yote yanayotiliwa shaka.

Hayo ameyasema leo Alhamis Juni 29, 2023 akihutubia Baraza la Eid El-Adh'haa lililofanyika katika Msikiti wa Mfalme Mohammed wa VI wa Morocco jijini hapa.

"Pia Serikali inapaswa kutoa elimu kwa wananchi ili waendelee kuuelewa mradi huu (uwekezaji bandari)," amesema.

Mruma amesema kubainika kwa mradi huo kuliibua mjadala na taharuki kwa wananchi ambao hawakuwahi kuwa na taarifa sahihi kuhusu mradi huo.

Mruma ameitaka Serikali kupokea maoni ya wananchi na kutoa ufafanuzi kwenye maeneo yote yanayotiliwa mashaka.

Hiyo ni kauli ya kwanza kutoka Bakwata tangu uanze mjadala baada ya Serikali kusaini mkataba wa awali wa ushirikiano wa uwekezaji na uboreshaji bandari na Serikali ya Dubai kupitia kampuni ya Dubai Port World.
Wafafanue mara ngapi? Serikali wametoa maelezo mengi sana. Alianza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, akaja mwanasheria aliyehusika , juzi kaongea Mwanasheria Mkuu

Tatizo sio Serikali kufafanua, Tatizo ni watu wamejaa ujinga na kutaka kusikia yale wanayotaka kusikia tu! Kwenye hili hata Serikali wakimleta malaika afafanue hataeleweka.

Serikali ndo inajua shida iko wapi na wanataka kuitatua iyo shida! Wameshaanza kuchukua hatua sasa hawatakiwi kurudi nyuma.

Watanzania ni watu wa kushikiwa masikio na wanapenda maneno sana bila kazi , na wanasiasa pamoja na wapenda sifa wanalijua hili hivyo wanajua sana kuwaendesha.

Wao hawajui dunia inaendaje, hawatoki nje kuona nchi zinafanikiwaje ila wamekalia maneno maneno na ujinga tu.

Kwenye hili Serikali iendelee na utekelezaji wa makubaliano na sasa waanze majadiliano ya HGA ili tusonge mbele.

Dunia haitusubiri
 
Kweli kabisa
 
Wee pimbi ufafanuzi unaotakiwa ni wa kifungu kwa kifungu cha mkataba huo na si kuwapiga watu sound za kisiasa.

Bandari ni mali ya umma na si ya hao wanasiasa uchwara!
 
Kifungu kipi hakijafafanuliwa?

Mali ya Umma huo umma umeiendesha kwa ufanisi? Mmefanikiwa nini kwenye kuiendesha nyie umma hadi kuifaidisha nchi?
 
Haya mambo ni kama timu moja wanacheza na wanapeana pasi tu...., Kutoka kwa kipa analipatia Pande Bunge, Bunge linapiga pasi ndefu kwa wazee wa Propagada hapa na Pale wanapiga vyenga na kurudisha mpira kwa Mdau mwingine ambaye anauliza maswali ambayo majibu yake yakirudishwa kwa Kipa Anatoa Pasi ndefu mpaka kwa Striker....

Wananchi kabla hamjagundua ni nini kinaendelea mshafungwa na mechi ishakwisha....
 
Back
Top Bottom