BAKWATA walaani mauaji Palestine, wawataka Waislamu kuitumia Ijumaa kuiombea Palestine

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
BAKWATA WAITAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MGOGORO WA PALESTINA NA ISRAEL

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) limelaani vitendo vya Israel kuua raia wasio na hatia wa Taifa la Palestine katika mgogoro ulioanza Mei 10, 2021

Wamesema vitendo hivyo vinakwenda kinyume na Misingi ya Haki za kibinadamu na kuwataka Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua

Pia wamewataka waislamu wote nchini Tanzania kutumia swala ya Ijumaa, Mei 21, 2021 kuiombea Palestina na kufanya dua za kunuti katika swala zote tano

#JamiiForums
 
Hivi kwani huko Gaza ni vita ya kidini?

Bakwata watulie tuu mana kule sio mambo ya dini.

Mbona kuna boko haram, alshabab, IS na wengineo wanashambulia, kuua na kubaka watu kwa kisingizio cha Uislamu lakini hawasemi chochote.
 
Nilitaka niulize hili swali,ngoja nikaushe
 
Historia inaonesha kuwa Waisrael ambao dini yao kuu ni uyahudi walijipenyeza ndani ya Palestina na kuanza kujitanua kidigokidogo. Na kinachowasaidia ni nguvu zao na wakati mwingine msaada wa nchi ya Joe Biden (USA). Kama Wapalestina wangekuwa na jeshi imara basi huenda wangeheshimiwa na waisrael.
 
Mimi binafsi nawalaumu hawa Hama's kwanini wameanzisha ugomvi na hilo dubwana lililokuwa limelala zake ?
NI kweli maribifu ni makubwa sana na vifo ni vingi mno kwa palestina kwanini mwezi ule mtukufu aanze kulishambulia hilo dude kwa zaidi ya makombora 1000.
 
Jumlisha na mauaji ya kibiti na msumbiji juzi Tu hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…