BAKWATA walaani mauaji Palestine, wawataka Waislamu kuitumia Ijumaa kuiombea Palestine

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,830
2,000
BAKWATA WAITAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA MGOGORO WA PALESTINA NA ISRAEL

Baraza Kuu la Waislamu Tanzania(BAKWATA) limelaani vitendo vya Israel kuua raia wasio na hatia wa Taifa la Palestine katika mgogoro ulioanza Mei 10, 2021

Wamesema vitendo hivyo vinakwenda kinyume na Misingi ya Haki za kibinadamu na kuwataka Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua

Pia wamewataka waislamu wote nchini Tanzania kutumia swala ya Ijumaa, Mei 21, 2021 kuiombea Palestina na kufanya dua za kunuti katika swala zote tano

#JamiiForums
IMG-20210520-WA0015.jpg
 

Zeus1

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
5,011
2,000
Hivi Bakwata mbona mauaji mengine yakitokea hatuwasikii wakilaani? huko Nigeria Boko Haram wanaua watu hatujawasikia Bakwata wakilaani,mauaji ya kimbali ya Rwanda, Bakwata hatujawahi kuwasikia je hao sio binadamu ila Wapalestina ndio wanastahili peke yao.
Nilitaka niulize hili swali,ngoja nikaushe
 

mchezo mbaya

JF-Expert Member
Feb 11, 2017
221
250
Historia inaonesha kuwa Waisrael ambao dini yao kuu ni uyahudi walijipenyeza ndani ya Palestina na kuanza kujitanua kidigokidogo. Na kinachowasaidia ni nguvu zao na wakati mwingine msaada wa nchi ya Joe Biden (USA). Kama Wapalestina wangekuwa na jeshi imara basi huenda wangeheshimiwa na waisrael.
 

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
12,214
2,000
Mimi binafsi nawalaumu hawa Hama's kwanini wameanzisha ugomvi na hilo dubwana lililokuwa limelala zake ?
NI kweli maribifu ni makubwa sana na vifo ni vingi mno kwa palestina kwanini mwezi ule mtukufu aanze kulishambulia hilo dude kwa zaidi ya makombora 1000.
 

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
826
1,000
Hivi Bakwata mbona mauaji mengine yakitokea hatuwasikii wakilaani? Huko Nigeria Boko Haram wanaua watu hatujawasikia Bakwata wakilaani,mauaji ya kimbali ya Rwanda, Bakwata hatujawahi kuwasikia je hao sio binadamu ila Wapalestina ndio wanastahili peke yao.
Jumlisha na mauaji ya kibiti na msumbiji juzi Tu hapa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom