Bakwata ni mwakilishi halali wa waislam wote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bakwata ni mwakilishi halali wa waislam wote?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngongo, Sep 29, 2009.

 1. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara ni kwanini serekali imekuwa ikiitambua BAKWATA kama mwakilishi halali wa waislam wote Tanzania wakati wapo waislam wengi wasioitambua au wasiofungamanana na BAKWATA.Yapo madhehebu tofauti tofauti katika dini ya kiislam [Shia,Sunni na nk]kama sikosei BAKWATA imeegemea zaid Sunni sasa ni kwanini Shia nao wasiwe na kiongozi wao [Mufti].

  Serekali inatambua katika ukristo yapo madhehebu mbali bali kama vile wakatoliki,walutheri,wasabato,waanglikani,wapentekoste na nk.Mawasiliano baina ya viongozi[maaskofu] wa madhehebu haya na serekali hayana mgankanyiko kama ilivyo kwa waislam.

  Naomba kupata ufafanuzi wakina hii hali inasababishwa na serekali au labda madhehebu au taasisi zenyewe za kiislam ndiyo chanzo cha huu mparaganyiko.
   
 2. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Tatizo ni waislamu wenyewe na BAKWATA kwa ujumla.Serekali haina lawama hata kidogo,unajua taasisi nyingi za waislamu zimekaa kisanii sani.Ukiangalia namna zinavyoendeshwa utashangaa sana sana zinafanyakazi bila kuwa na vision wala mission.
  Hebu niambie Shura ya maimau kazi yake nini ?.ukiichunguza utakuta ni taasisi ya mfukoni haina ofisi kazi yake kubwa ni kuangalia wakristo wamefanya nini.kuna nyingine ya kudai/ kutetea mali za waislamu hawa ni wasanii kupindukia hawana lolote.

  Hivi ni serekali gani duniani itakayokubali kufanya mawasiliano na Shura ya maimamu au kamati ya kutetea mali za waislamu.Ni bora serekali iendelee kuitambua Bakwata kuliko hivi vikundi vya kihuni.
   
 3. K

  Kabonde JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 12, 2008
  Messages: 421
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ni haki kabisa kwa serekali ya JMT kuitambua Bakwata kama mwakilishi wa waislamu wote kwasababu mpaka sasa hakuna chama/taasisi ya kiislamu iliyojionyesha kuwa na nguvu kuliko Bakwata.

  Taasisi nyingi zimejikita katika maslahi binafsi kwa wanaoziongoza kuliko maslahi ya jamii yote ya waislamu.Bakwata wanaafadhali kidogo ingawa wameshindwa kwa kiasi cha kutisha kuwaunganisha waislamu wote Tanzania.
   
 4. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Napenda kuanza na historia kidogo ya BAKWATA. Hii iliundwa mara baada ya Nyerere kushinikiza kuvunjwa kwa iliyokuwa East Africa Muslim league. Hii ilikuwa na nguvu sana enzi hizo na Nyerere kwa kuhofia hilo alilazimisha kuvunjwa kwa hiyo na akaunda BAKWATA.

  hakika aliweka wana USALAMA akina Adam Nassib, Alhaj Kundya na wengine kwa nia na madhumuni ya kuwadhibiti waislamu

  Sasa utaona BAKWATA ipo pale kwa nia na madhumuni ya kudhibiti Uislam na waislamu. Na ni chombo mahsusi cha kiserikali kutimiza azma hiyo.

  Sasa ni lazima Serikali ifate hilo na inakataa mabalaza mengine yote kama Istiqama, Baraza kuu la taasisi za Kiislam.

  Hiyo ndio reason behind kwa Serikali kuikmbatia BAKWATA wakati waislam wenyewe hawaitambui.
   
 5. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Someni kitabu "The Cross Versus The Crescent" alichoandika prof Lawrence Mbogoni. Anaelezea mwanzo wa Bakwata na kufutwa kwa EAMWL. Haikuanzishwa na Nyerere ingawa ilianzishwa chini ya utawala wake.
   
 6. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Kwa nni unazungumza juu ya kuwadhibiti waislamu? wana matatizo gani?
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  .

  Ukitaka kujua chanzo cha kuvunjwa kwa EAMWL ni njama zilianzia Iringa na zilianzishwa na nani soma kitabu kinachoitwa Kanisa katoliki na Siasa za Tanzania kilichoandikwa na Padre Silvano.

  Kijitabu hiki kilieleza namna kanisa katoliki adui wake mkubwa ni UISLAMU.( pg 23 para 4).

  Choko choko ilianza mara baada ya EAMWL ilipotaka kufungua University ya kwanza Tanzania na uanja walipata pale karibu na Uwanja wa Taifa. fedha za ujenzi kila kitu kilikuwa ready. Nyerere na kanisa kuona hilo waliamua kuunda zengwe kwa kutumia vyombo vya serikali kuvunja umoja huo.

  nakushauri ukitaka uhondo huo soma kitabu hicho cha Padre Silvano kisha soma hicho kingine utagundua ukweli
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Mkuu HM Hafif.

  Nimeziona hoja zako lakini bado sijazikubali kwasababu zifuatazo.

  [1]Baraza kuu la taasisi za kiislam limefanya maendeleo gani kwa waislamu na jamii ya watanzania kwa ujumla.Ninapozungumzia maendeleo nina maana ujenzi wa mahospitals,shule,vyuo vikuu na mambo yote ya maendeleo kwa jumla.

  [2]Baraza kuu la taasisi za kiislamu linavyoonekana liko kwaajili ya kushindana na BAKWATA badala ya kutoa mwongozo kwa waislamu namna ya kujikwamua kiuchumi na kiimani.

  [3]EAC ilivunjika mwaka 1977 nchi ya Tanzania haikuacha kusimamia maendeleo yake kwa kisingizio eti Kenya walibaki na mali nyingi za iliyokuwa EAC.Ni hakika hiki kisingizio kwamba Nyerere aliunda BAKWATA hakiwezi kuepusha lawama kwa viongozi wa jumuiya mbali mabali za kiislam kutosimamia maendeleo ya waislam.Ni juzi juzi tulikuwa tunawasikia viongozi wa taasisi mbali mbali za kiislam wakipigania serekali ianzishe mahakama ya kadhi.Swali mahakama ya kadhi ikianzishwa na serekali madai siyatakuwa hayo hayo.
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  .

  Ni kosa kubwa sana la Kisheria kwa Serikali isiyo na DIni kuwaamulia watu na kulazimisha watu wafate dini fulani.

  Serikali imesajili taasisi nyingi sana za kiislam na zote zimesajiliwa bila moja kuwa juu ya nyingine.

  Serikali kama inaziona zinakwenda nje ya makubaliano ya usajili wao wana haki kisheria kuzifuta. lakini zote zina haki sawa kisheria.

  Sasa serikali kuikumbatia BAKWATA na kuziacha nyingine ni kinyume cha sheria. Waislam wana haki kuishitaki serikali.
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  .

  Naona umenena mengi sana. lakini kisheria sio vizuri kutaja watu majina kwani inaweza kuwa tafrani kwako.

  nakubaliana na maneno yako.


  Serikali inafanya makosa makubwa kuikumbatia BAKWATA. na inavunja katiba.
   
 11. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #11
  Sep 29, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  kwa sababu ya kirefu cha bwakwata.......wengine wanajiita shura ya maimamu sasa hapo serikali ifanye nini.......tatizo kwenye uislamu kuna misimamo mingi,kuna wale wenye msimamo vuguvugu,kati na msimamo mkali.......na hawa siku zote panapokuwa na uislamu hapakosi migogoro isiyoisha...........
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  .

  Tueleze pamoja na mali nyingi BAKWATA ilizorithi toka EAMWL. je imefanya maendeleo gani toka ianzishwe kuwafanyia waislamu?
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Serekali imesajili taasisi nyingi sana za Kiislam je ni kwanini taasisi zilizopata usajili zimeshindwa kuwaletea maendeleo waislamu ?
   
 14. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  .

  nafikiri hapa ndio mimi na wewe tujiulize kwanini Serikali ya Tanzania inaikumbatia BAKWATA pekee wakati wengine wapo?

  Kuna siri gani kati ya Bakwata na Serikali ya Tanzania? na Serikali na waislamu?

  .

  hata Ukristo kuna Ukatoliki, Lutheran, SDA, Anglican , etc. sasa Ni wajibu wa Serikali kuzitambua zote hizo japo wote ni wakristo.
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280

  Mkuu Barubaru.

  Nakubaliana na wewe kwa asilimia zote BAKWATA imeshindwa kuwaletea maendeleo waislam,sina kipingamizi kwa viongozi wa BAKWATA wamefuja mali nyingi za waislamu.Je waislam na taasisi nyingine wamefanya nini kuzuia mali za waislamu zisiendelee kuchezewa.je taasisi nyingie zimefanya mambo gani ya kimaendeleo tofauti na BAKWATA ?.
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Barubaru,
  Bahati nzuri ninavyo vyote. Ni Padre Sivalon na si Silvano. Na page uliyoitaja, page 23 ina paragraf 2 tu, paragraf ya kwanza anazungumzia uhusiano maalum baina ya viongozi wa Kanisa Katoliki na viongozi wa Chama na serikali. Para ya 2 anazungumzia lengo la utume wa kijamii wa Kanisa Katoliki kuanzia 1953-1966 ambao ulikuwa ni "kulinda nafasi ya Kanisa katika jamii kwa ujumla kwa kupinga kuenea kwa falsafa ya Marx hapa Tanzania...... na kuhami nafasi ya kanisa katika kupinga kuenea kwa dini ya Kiislamu." Lakini kilichopelekea Nyerere kupiga marufuku EAMWL ni kujihusisha kwa kundi hilo katika siasa za Tanganyika na njama za kumwondoa Nyerere kwenye uongozi wa TANU. Tena waliomtonya Nyerere walikuwa ni viongozi wa Kiislamu ambao kwao uzalendo ulikuja kwanza.
   
 17. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Sijui serikali imemlazimisha nani kufuata dini gani?
  Unasema serikali imeikumbatia Bakwata, sasa unataka inapotaka kuongea na waislamu iongee na chombo gani maana vyombo (taasisi) zingine za kiislamu nazo haziko pamoja. Zimegawanyika na kila moja inajinadi kuwa inasimamia waislamu. Katika mazingira hayo, ndiyo maana serikali inaamua kuwasiliana daima na Bakwata. Isitoshe Bakwata ndiyo mtoto wa kile chombo kilichovunjwa huko nyuma.
   
 18. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Tofautisha kati ya madhehebu na vyombo vilivyoundwa kuwakilisha madhehebu hayo. Madhehebu ya Kikristo yako mengi kama yalivyo pengine hata ya Kiislamu. Lakini katika wingi wa madhehebu ya Kikristo kuna vyombo ambavyo vimeundwa. Kuna TEC (TAnzania Episcopal Conference = wakatoliki) na CCT (the Council of Churches of Tanzania).

  Kwa hiyo kwa waislamu chombo kinachofanana na hivyo ni Bakwata, ambayo ni chombo cha waislamu wote. Sasa sijui kwa nini hamkitaki?
  Kumbe usilinganishe madhehebu ya kikristo na taasisi za kiislamu. Taasisi za kiislamu siyo madhehebu ya kiislamu kwa sababu haziko mbadala ya Sunni, Shia, nk. Taasisi hizi ni vyama fulani (associations) au vikundi kama ilivyo VIWAWA, WAWATA, nk kwa wakatoliki.
   
 19. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hiki kijitabu nitakitafuta kesho. Je naweza kukipata bookshop gani?

  Hakika Nyerere alikuwa mjanja sana aliweza kuzua jambo na kuweza kulihalalisha. VP EAMWL itake kumuondoa yeye madarakani? Ukweli EAMWL ilikuwa powerful sana na ilianzishwa kabla kuanzishwa kwa EAC.

  naungana na barubaru kusema kuwa walim shock JKN pale walipokuja na kuanzisha Chuo kikuu cha kwanza ndani ya TZ.

  hakikakatika kuuwa hilo alijenga fitina na kuwafitinisha mashehe na waumini wao na kisha kuwasingizia uhaini.

  Vp ipindue Tanzania na isifanye hivyo kwa Kenya, Uganda na hata zanzibar.

  naipenda sana mada hii Barubaru na jasusi kwa ufafanuzi wenu.
   
 20. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135

  Ina maana kuna waislamu wanaotaka kudhibiti uislamu na waislamu wenzao? Kwa maana hao wana usalama ulio wataja hapo juu ni waislamu. Serikalini napo kuna waislamu wengi tu ambao wako kwenye vyeo vikubwa vya maamuzi including raisi mwenyewe. Sasa hao waislamu ambao wana cheo serikalini wata ruhusuje serikali idhibiti uislamu? Kama usemacho ni kweli basi ni unasema kuwa adui mkuwa wa waislamu Tanzania ni waislamu wenyewe. Maana unavyo ongea ni kana kwamba serikali imejaa Wakristo.

  Swali kubwa ni je. Kama usimacho ni kweli kwa nini hao waislamu ambao wapo serikalini wapo tayari kudhibiti dini yao wenyewe na waislamu wenzao?
   
Loading...