Mabishano ya kidini ni kipimo cha uelewa mdogo na ufinyu wa akili

Mtuache

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
251
638
Habari wana Jamvi

Wakristo tunamjua Mungu kupitia Biblia. Kupitia hiyo tumefundishwa Mungu ni nani, hufanya kazi kwa namna, hupenda nini, nini hapendi na mambo kadhaa wa kadhaa vyote hivyo msingi mkuu ni Biblia. Naamini hata kwa Waislam ni hivyo hivyo, msingi wa dini yao ni Quran. Nisiende sana kwa Waislam maana sio lengo langu.

Kuna mikanganyiko mingi ipo ndani ya Biblia aidha imeandikwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya, au labda kwa akili zetu za kibinadamu ni ngumu kuelewa au tunaelewa tofauti.

Lengo la andiko hili ni kufahamisha umma ya kwamba kutolielewa jambo haimaanishi hilo jambo sio la ukweli au halipo na halijawahi kuwepo.

Tukiwa wadogo kuna mambo kibao hatukuwa tunajua, lakini yalikwepo. Tuliuliza wazazi wetu watoto hupatikana wapi!? Wengine tuliambiwa baharini wengine tuliambiwa hununuliwa. Tumekua wakubwa tukajua ili mtoto apatikane ME na KE lazima wafanye mapenzi itungwe mimba. Ila kwa teknolojia ya sasahivi kufanya mapenzi pia sio lazima

Sindio?

Lakini je? Hakuna watoto wanaopatikana baharini? Wazazi wao huwatupa due to sababu mbalimbali na wakapatikana huko na wasamalia wema.. Hakuna watoto wanaonunuliwa mahospitalini? Aidha kwa njia zisizo halali au halali?

Je, Wazazi wetu walivyotuambia watoto hupatikana baharini walitudanganya?

MIMI SIJUI, JIJIBU MWENYEWE
Pengine hatukuwa tumekomaa akili vya kutosha kuambiwa kila kitu kwa wakati huo. Tungeambiwa mtoto ili apatikane in the first place lazima watu wafanye mapenzi. Tungeibua maswali mengi mfn "kufanya mapenzi ndo nini?, Na mimi nikifanya mapenzi nitapata mtoto? Kwahyo baba na mama walifanya mapenzi ndo nikapatikana?" Na maswali mengine meeeengi naamin tungejiuliza.

Wakristo tunaamini Biblia iliandikwa na mtu zaidi ya mmoja, na kila mmoja aliongozwa na roho mtakatifu. Kila mwandishi aliandika katika zama zake na eneo lake alikokuwa anaishi. Baadae (sijui miaka mingapi mbele) Watu ambao sijui pia ni akina nani walikusanya hivi vitabu vyote ndio ikapatikana Biblia moja.

Je, haudhani kuwa kipindi walivyokuwa wanakusanya hakuna vitabu viliachwa? Aidha kwa makusudi au bahati mbaya? Unaamini vilikusanywa vitabu vyote? Na kama baadhi waliviacha, unahisi kwanini waliviacha?

Achana na huko kukusanya, Biblia pia imetafsiriwa katika lugha mbalimbali, unahisi hakuna makosa yalifanywa na hawa waliotafsiri?

Hudhani kuwa hii mikanganyiko unayopata ni matokeo ya ukusanyaji na Kutafsiri?

Kama jibu ndio, kwanini basi lawama zije kwa Mungu? Uone Mungu ni muongo na maandiko yake yana ukakasi?

MIMI SIJUI, JIJIBU MWENYEWE
Sifa ya mtoto ni udadisi, sifa ya mtu asiejua jambo ni udadisi pia. Mtu asiejua jambo ni kama mtoto, huwa na tabia ya kujiuliza maswali mengi. Sio kwa nia mbaya, hapana ila kwa nia nzuri tu ya kutaka kujua.

Sasa ubungo wa binadamu upo hivi, ukichambua kitu kwa mabaya yake utapata mabaya mengi saana. Ukikichambua kitu hicho hicho kwa mazuri yake utapata mazuri mengi sana.

Kuna binadamu wenzetu wanaabudu Ng'ombe, wengine sanamu, naamini wewe mkristo au Muislam unawaona kundi la waabudu Ng'ombe na sanamu limepotea. Ni moto kwa kwenda mbele mpaka sijui nini. Lakini wao wanajiona wapo sawa, unajua kwanini? Kwasababu ubongo wao umeelekezwa na kufundishwa hivyo kwa Ng'ombe sio mnyama kama mnyama ni Mungu na anapswa kuabudiwa.

Hupaswi kuwacheka au kuona wamepotea, kama unahisi hawapo unapaswa kuwaelekeza.

Kwani ulipouliza lile swali kwa wazazi wako, walikucheka? Baada ya kuambiwa watoto hununuliwa na ukakubali, walikucheka?

Unadhani kwanini hawakukucheka?

MIMI SIJUI, JIJIBU MWENYEWE

HITIMISHO:

Mabishano ya kidini ni kipimo cha uelewa mdogo, ufinyu wa akili, au matumizi mabovu ya akili zetu zilizo perfect. Muislam vs Mkristo, Mkristo vs Mkristo, Muislam vs Muislam na Versus zengine zoote. Wagonjwa wa akili ndo hubishania mambo ya dini, tena sio dini tu mambo kibao. Wagonjwa wa akili ndo huona dini yake ni bora kuliko nyengine.

Umezaliwa katika Ukristo, ubongo wako ukaelekezwa Ukristo ndo dini bora na wenyewe ukaamini hivyo. Usione Waislam wamepotea, hata wewe ungelelewa kwenye mazingira ya Kiislam ungeamini vile vile wanavyoamini wao.

Hivyo hivyo kwa Muislam, mtu ambae sio wa dini yako sio mpotevu na wala sio kuni ya motoni. Wewe ungekuwa katika nafasi yake ungekuwa kama yeye.

DINI ZOTE NI BORA
 
Habari wana Jamvi

Wakristo tunamjua Mungu kupitia Biblia. Kupitia hiyo tumefundishwa Mungu ni nani, hufanya kazi kwa namna, hupenda nini, nini hapendi na mambo kadhaa wa kadhaa vyote hivyo msingi mkuu ni Biblia. Naamini hata kwa Waislam ni hivyo hivyo,

DINI ZOTE NI BORA
Exactly
 
Kichwa cha habari ni DINI ila umeongelea dini mbili tu, ambazo technically ni kama dini moja tu maana ni kama dini zinazoabudu mungu yuleyule ila zilitengana sehemu flani katika historia.

Sasa kuna kama miungu wengine zaidi ya 1000. Yupi ndio mungu wa kweli? Kila dini inasema mungu au miungu yake ndo kweli.... miungu wapi ni kweli basi au mungu yupi ni wakweli? Huu mzozano wa watu kutoamini ungetatuliwa kama mungu au miungu waje wathibitishe uwepo wao.

Na kuna sababu kwann nchi kama china, japan, korea zina waumini wachache sana wa dini za kiabraham (ukristo, usilamu na uyahudi).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana Jamvi

Wakristo tunamjua Mungu kupitia Biblia. Kupitia hiyo tumefundishwa Mungu ni nani, hufanya kazi kwa namna, hupenda nini, nini hapendi ...
Dini zote ni bora kwa hao walioamua kuziamini kwamba kila mtu akiulizwa kwanini anaamini dini fulani,hawezi kosa sababu nzuri upande wake.

Kuna dini inaruhusu kuoa wake wengi hii inaweza kuwa sababu nzuri kwa anaependa wanawake wengi.

Kuna dini inaruhusu watu kuvuta bangi,pia inaweza kuw sababu nzuri kwa yule anaependa kuvuta bangi.

Tutaongea meeeeengi kuhusu dini ila dini Nzuri ni ile inayomuabudu Mungu wa kweli.
 
Watu Wana-amini simu kuliko vitabu vyao vya dini na hizi Taarifa zinazoamua tuwe wapi na tujadili vipi suala hili hatuwezi pona huu ugonjwa.

Chochote kinachokulia muda wako unakiabudu.
 
Kichwa cha habari ni DINI ila umeongelea dini mbili tu, ambazo technically ni kama dini moja tu maana ni kama dini zinazoabudu mungu yuleyule ila zilitengana sehemu flani katika historia...
Uislam siyo dini ya ki-abraham na Wala haufanani na ukiristo ambao umesema kiufundi ni dini moja,uislam ni Imani juu ya mungu mmoja, muumba wa kila kitu, hakuzaa Wala hakuzaliwa, hafanani na chochote na kwamba baada ya maisha ya dunia ambayo ni mtihani/test Kuna akhera kwenye malipo wakati ukiristo ni Imani juu miungu mitatu wanaogonga kolabo kutengeneza mungu mmoja,aliyemtia mimba mwanamke bikira ili yeye mungu azaliwe aje duniani kutukomboa(Emanuel) na mungu huyohuyo ndiye baba na mwana
 
Uislam siyo dini ya ki-abraham na Wala haufanani na ukiristo ambao umesema kiufundi ni dini moja,uislam ni Imani juu ya mungu mmoja,muumba wa kila kitu,hakuzaa Wala hakuzaliwa,hafanani na chochote na kwamba baada ya maisha ya dunia ambayo ni mtihani/test Kuna akhera kwenye malipo wakati ukiristo ni Imani juu miungu mitatu wanaogonga kolabo kutengeneza mungu mmoja,aliyemtia mimba mwanamke bikira ili yeye mungu azaliwe aje duniani kutukomboa(Emanuel) na mungu huyohuyo ndiye baba na mwana
Usilam ni dini ya kiabraham. Kwamaana kwamba wasilamu wanaamimi mungu wa Abraham.
Na ukristo hauamini katika miungu watatu tofauti, hivo sivyo biblia inavosema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu miungu ya kihindi,Anza na ng'ombe unayemla supu kila siku
India kuna dini kibao (hivo pia kuna miungu kibao). Ila hakuna dini inayosema kua ng'ombe ni mungu wao, la hasha. Bali kuna baadhi ya dini zinaamini kua binadamu wanapokufa wanapewa miili mingine, hata ya wanyama. Ivo ndiomaana hawali nyama wakiamini kua huenda akawa ni binadamu kwenye mwili wa mnyama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
India kuna dini kibao (hivo pia kuna miungu kibao). Ila hakuna dini inayosema kua ng'ombe ni mungu wao, la hasha. Bali kuna baadhi ya dini zinaamini kua binadamu wanapokufa wanapewa miili mingine, hata ya wanyama. Ivo ndiomaana hawali nyama wakiamini kua huenda akawa ni binadamu kwenye mwili wa mnyama

Sent using Jamii Forums mobile app
Wahindu Hadi nyani ni mungu,Wana miungu mungu,katika hizo namna ambazo ukifa wanaamini unabadilika,samaki na kuku hawamo!?..hawali samaki!?
 
Watu Wana-amini simu kuliko vitabu vyao vya dini na hizi Taarifa zinazoamua tuwe wapi na tujadili vipi suala hili hatuwezi pona huu ugonjwa.

Chochote kinachokulia muda wako unakiabudu.
Hapana. Sio kweli.... kuabudu. Je wajua kitu kimoja binadamu anachofanya kwa muda mrefu ni kipi..? Kulala.. that's it unaspend muda mrefu kwa mkupuo kwa kulala. Kwa mantiki yako basi ni kwamba binadamu tunaabudu usingizi/vitanda?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kichwa cha habari ni DINI ila umeongelea dini mbili tu, ambazo technically ni kama dini moja tu maana ni kama dini zinazoabudu mungu yuleyule ila zilitengana sehemu flani katika historia
Pata nafasi ya kujielimisha kabla ya kukomenti mitandaoni. Waislam wana mungu wao anayeitwa Allah halafu wakristo na wayahudi Mungu wao anaitwa Yahweh (pia Jehovah, Yeshua, Yesu Kristo nk)

Uislam ulianzishwa kwa mohamed kushushiwa maandishi akiwa mecca na medina wakati uyahudi na ukristo ni rekodi ya mambo yaliyowatokea watu halisi na ikaandikwa kama historia na maagizo ya Mungu wao wakiwa katika nchi ya Israel.
 
Back
Top Bottom