BIN BOR
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 1,013
- 407
Inategemea ni dini gani unayoiongelea, usiziweke dini kwenye kapu moja.Dini Nyingine hata Lusekelo ni "Mtume"
Kwani polisi walikuwa wanapambana na dini gani Arusha?
Inategemea ni dini gani unayoiongelea, usiziweke dini kwenye kapu moja.Dini Nyingine hata Lusekelo ni "Mtume"
Dini zinafundisha kukubali ukweli na wewe ungekubali ukweli. Si ulinyamaza kimya hadi sasa?
kwenye bold hapo juu "inatowa",ni kiswahili au?? Mimi mpagani, but lazima niwe mkweli ndugu...
Mimi natowa tamko la kuwalaani wote walioanzisha na kushadidia maandamano yaliyozuiliwa na polisi kufanyika.
Walaaniwe wote waliolazimisha ya fanyike na damu za hawa waliofariki ziwasute maisha yao yote.
Ndugu zangu wana jamvi kwanza nasema HAPPY NEW YEAR japo nimechelewa kuwatakiwa mwaka mpya mwema, ninauhakika kabisa lilotokea Arusha limemkera hata Kikwete japo hasemi, mmoja wa watu waliokerwa ni Sitta ameamua kulipiza kwa kumkaanga Ngereja mchana kweupe,Kuhusu tamko la BKWATA wachangiaji baadhi yao haiwapasi kusema kidini badala ya kiukombozi wa nchi zaidi.Unataka kuniambia kuwa viongozi wa dini hawaruhusiwi kukemea uovu uliofanywa na vyombo vya Serikali, km Jeshi la Polisi, eti kwa hofu ya kuogopa kuchanganya dini vs siasa?
nani kakuongopea? "muislam ndugu yake muislam" kwa vyovyote tutaipinga bakwata lakini hatutoisaliti ni tofauti za kawaida si kwamba bakwata haitakiwi na waislam. alafu yalipofanyika mauwaji kule pemba hao wagala wa kwanza kupinga tamko waliongea nini?
au ndo mkuki kwa nguruwe?
Jamani udini huko wapi hapa!!! Aliyekataliwa kutambuliwa na maaskofu ni mkristo wala sio muislamu. Je angekuwa ni muislamu ingekuwaje???? Ni wapi maaskofu wa Arusha wametamka kwamba hawamtaki Kikwete kwa kuwa ni muislamu? Huu ni ujinga uliokithiri na kujaribu kutafuta mchawi wakati ukweli unajulikana!!! Hawa wanasahau kwamba ni kanisa hilo hilo liliowahi kutamka kwamba Kikwete ni chaguo la Mungu? Mbona waislamu hawakuipinga hiyo kauli? This sounds like cheap politics to me!!!
Tiba
KAUMZA....kuna tafsiri tatu juu ya wewe na ujumbe wako huu.
1. Wewe ni fisadi au unafaidi matunda ya ufisadi unaotekelezwa na CCM
2. Wewe unaweza kuwa na tatizo la kusoma, kuelewa, kufikiri na kuoanisha mambo
3. Wewe ni mdini na udini wako umeuweka wazi bila kificho.
Therefore, without hesitation, I call this a MALEVOLENCE
Wana siri ya pamoja, lengo likiwa ni kuhakikisha wanashika nchi ili kanisa liendelee kushika hatamu na UTAMU wa nchi hii. JK kawanyang'anya utamu kupitia MoU kati ya kanisa na serikali. JK alitaka awanyime utamu baada ya mwaka jana kutaka mali zinazoingizwa na makanisa nchini zilipiwe kodi. Leo wanasema hawamtambui Meya Arusha kisa mauaji. Mbona hawakumtambua Rais baada ya mauaji ya januari 21 ambapo watu 27 waliuawa na wanawake kubakwa. AU NI SIASA ZA UZANDIKI?
Huu ni upupu!!! Wewe unaishi dunia gani aisee? Huoni aibu kuleta bandiko kama hili hapa? Wewe ni mdini na udini hatutakaa tuupe nafasi Tanzania kwani udini ni sumu kupita kiasi. Kupanda mbegu za udini ni kuyatafuta yale yaliyotokea Rwanda kati ya Wahutu na Watutsi ila sisi hapa itakuwa ni kati wa wakristo na waislamu. Ng'oa hii mbegu mbaya ya udini kutoka kwenye jamii ya Watanzania kwani ni hatari na mbaya kuliko ukoma!!! Wewe unasema hayo na umesahau kwamba meya wa Arusha aliyekataliwa na viongozi wa dini ya kikiristo ni mkristo mwenzao vipi angekuwa ni muislamu hapo tena si ingekuwa ni balaa? Umepewa akili itumie kuchambua mambo na wala usije hapa kuweka mabandiko kwa ajili ya kuwafurahisha waliokutuma!!!!
Nani ali-engineer mauaji ya Rwanda? Kumkataa meya wa Arusha ni kama adhabu kwa wote walio/wanaom-support JK. Ukweli unabaki palepale, KANISA lina hisa na CDM. Udini wangu uko wapi? Tusikariri kwamba kila anaekosoa dini fulani ni mdini. Hata Padri Karugendo huwa anakosoa mwenendo wa kanisa. Naye ni mdini? Umepewa akili ufikiri, FIKIRI SASA