BAKWATA na Mauaji Arusha


Nikuulize wewe maaskofu wanawakilisha chama gani? Kama hawamtambui meya wa Arusha? It is a cheap politics but combine with massive poverty, stupidity, and gross injustice towards muslims it will lead to something no one anticipated. Kumbuka vita vingi duniani huanza kimzaha zaha hivi hivi wakukemewa ni maaskofu kwa kulianzisha na sio masheikh wao wanaweka sawa na tu na kuwastua maaskofu hii SIO NCHI YA KANISA!!!
 
... ukweli ni huu hapa... NDIO KIKWETE HAFAi... wote tulopiga kura kutaka mabadiliko tulifanya hivyo kwa zaidi ya asilimia 60!! Hafai, hatumtaki. Ndio
 
Kwa taarifa yenu ni kuwa wakuu wa polisi wanalaumu Usalama wa taifa uliowapenyezea taarifa potofu za kiintelijensia zilizosababisha kusitisha maandamano bila kutathmini madhara ya kuzuia dakika za mwisho. Wanasema usalama wa taifa kweli sasa unaelekea kuwahalibia kazi maana wao(usalama wa taifa) wanafanya kazi za CCM zaidi kuliko za taifa
 
Ndg zangu wana JF salaam kwenu.

ccm nadhani sasa tumetambua mdini ni nani, aua nani anainitiate udini Tanzania. Ni ukweli ulio wazi kwa yoyote ambaye anachambua bila kushabikia dini yoyote, wala chama chochote wala mtu yoyote, atagundua kuwa wanaoanzisha udini ni viongozi wa ccm kwa maslahi yao binafsi.

huku mtaani hakuna udini mnaoutamka nyie walafi wa madaraka sisi tunaishi kwa amani na dini zote, na kwa taarifa yenu we need Changes.

MAASKOFU,MASHEHE, MAIMAMU NA WACHUNGAJI, endeleeni kuikosoa na kuikemea serikali na vyama vingine vyote bila kuogopa lolote maana tunajua mwisho wao umefika. WE NEED CHANGES

mimi ni muislam safi kabisa lakini simfagilii Kikwete japo ni dini moja na pia siwapendi Lowasa na mafisadi wengine weather waislam au wakristo, na kuna rafiki zangu wengine ni wakristo nao wako kama mimi au tofauti na mimi.

ccm wanapenda mara zote kusifiwa, wakikemewa au kukosolewa wanaanza kuzungumzia udini, mbona wakisifiwa wanafurahi na kuwapongeza viongozi wa dini?

wamegundua mwisho wao umekaribia na sasa wanatafuta njia za kujikomboa, moja ya njia ni kuwagawa watu kwenye udini huku wao wakijifanya neutral...,
 

First of all ukae ukilijua na wenzio walifahamu kuwa WAISLAMU NI WENGI KUSHINDA WAKRISTO TANZANIA na wamekuwa kimya muda mrefu sasa the sleeping giant is awakening my friend. Pili wakristo na waislamu ndio dini mbili kuu Tanzania wahindu na wengineo wanapercentage yao but wakichambuliwa hawafikiii wengi kama waislamu na wakristo sasa it is important for these two groups to reconcile.
 

Kwa post hii, sitaki kuamini kwamba sehemu kubwa ya Waislam wana uwezo mdogo sana kufikiria mambo kisayansi, Pia sitaki kuamini kwamba sehemu kubwa ya waislam wanaamini kwamba muislam akifanya kosa akihojiwa na Mkristo inamaanisha kupiga vita uislam hata kama kwa kufanya hivyo kuna maslahi ya kitaifa. Pia sitaki kuamini kwamba Sehemu kubwa ya waislam wanaamini Jk Yupo madarakani kihalari na yeyote anaye charange utaratibu uliotumika kumuweka madarakani anapiga vita Uislam. Nasisitiza sitaki kuamini hivyo japo kuna watu wana lazimisha watu tuamini hivyo rasmi.
 

Mkuu naomba unifafanulie hichi kipengele katika nondo uliyotoa:-

Fifteen years ago, tens of thousands of Catholics were hacked to death inside churches. Sometimes priests and nuns led the slaughter. Sometimes they did nothing while it progressed. The incidents were not isolated. Nyamata, Ntarama, Nyarubuye, Cyahinda, Nyange, and Saint Famille were just a few of the churches that were sites of massacres.

Hapa huoni hata hawa maaskofu wetu nao wanataka kutupeleka huko huko?

Na hii nimeitoa Wikipedia je unasemaje?

Though religious factors were not prominent (the event was ethnically motivated), the Human Rights Watch reported that a number of religious authorities in Rwanda, particularly Roman Catholic, failed to condemn the genocide at the time.[22] Some in its religious hierarchy have been brought to trial for their participation by the International Criminal Tribunal for Rwanda and convicted.[21] Bishop Misago was accused of corruption and complicity in the genocide, but he was cleared of all charges in 2000.[23] The majority of Rwandans, and Tutsis in particular, are Catholic, so shared religion did not prevent genocide.


Hebu tupe upeo wako wa ufahamu.
 
Uislamu ni dini ya kinafiki sana!...................kwani oic imefikia wapi?
 

Vile vile sitaki kuamini kwamba Mdondoji ni Mwislaam, maana kwa kufanya hivyo nitamaanisha Waislam wana uwezo kama wake katika kutafakari mambo,
 
Mimi natowa tamko la kuwalaani wote walioanzisha na kushadidia maandamano yaliyozuiliwa na polisi kufanyika.

Walaaniwe wote waliolazimisha ya fanyike na damu za hawa waliofariki ziwasute maisha yao yote.

we vp?kwani walioandamana walilazimishwa??
 
Sikujua kuwa hujui kuwa polisi hawana mamlaka ya kuzuia mikutano wala maandamanoya viumbe wowote achilia mbali ya vyama vya siasa kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi hii ambazo zimetungwa kwa matakwa ya CCM. Nchi haiendeshwi kwa amri tena amri haramu, tuambieni polisi walpata wapi mamlaka ya kuzuia maandamano au mnashbikia wauaji kwa vile walouawa si wa chama chako? Kumbuka risasi hazikuchagua dini
 
wajinga ndio wali wao huo! demokrasia inavunjwa wao wanalilia kikwete kutotakwa...
 
Tuache ushabiki usiokuwa na mbele wala nyuma! Kuna watu hapa jamii forums wao kazi yao ni kufuata mkumbo na kuchangia pasipo hata kufikiri. Hata kama ulijariwa akiri kidogo mno, zitumie hizohizo kuchambua mambo maana hayaitaji akiri nyingi, yako wazi mno! Mtu anayesema swala la udini awe kiongozi wa dini au muumini wa dini nadiriki kumshauri asome na kuvielewa vitabu vya dini yake kadiri ya imani yake alafu aangalie historia ya dunia! Katika historia ya dunia ni dhahiri kabisa kuwa wanasiasa pale wanaposhindwa kutawala huangalia ni sehemu ipi wanaweza kuegemea ili kuficha udhaifu wao. Mojawapo ya vitu wanavyoweza kuvitumia ni pamoja na kuwagawa watu kidini, kikabila, kikanda (regions) n.k. Kwa kuwa Tanzania si rahisi kuigawa kikabila na kikanda kwa jinsi ambavyo tumeingiliana ni dhahiri kabisa kuwa sasa wanasiasa wanatumia dhana ya dini kutugawa watanzania. Ieleweke kabisa kuwa kwa muumini yoyote yule anayeishi tanzania apime mwenendo na mafanikio ya viongozi yetu kisiasa hawezi kusema eti wakristu au waislam hawamtaki Kikwete! Anayesema haya ni mpuuzi na huenda akiri zake zina matatizo. Hakuna Mwislamu au Mkristu au mpagani anayefurahia mwenendo mzima wa uendeshaji nchi kwa sasa! Kama ni mfumuko wa bei sote unatugusa, kama ni kukaa gizani sote tunakaa gizani, kama ni suara la richmond/dowans sote tunahusika katika ulipaji, kama ni huduma mbaya za jamii sote tunahusika, kama ni mabomu na risasi hazichagui wewe ni mkristu au mwislam au mpagani! Ni dhahiri kabisa kuwa pale viongozi wa dini wanapokemea uovu kwa watawala istaafsiriwe kuwa ni udini! Kiongozi wa din anayeona binadamu anauwawa kwa kudai haki yake yake, na kwa kupigwa risasi hadharani akabeza na kushangilia, hafai kuwa kiongozi wa dini. Mojawapo ya majukumu ya viongozi wa dini ni kuhakikisha kuwa siku zote haki inatendeka ili amani iweze kupatikana, kama haki haipo amani haiwezi kuwepo.

Suara la kukemea uovu lisitafsiriwe kuwa ni udini na serikali ikalikumbatia! Mimi ninaishi na waislamu ni marafiki zangu, tunateseka wote pale mtaani kwangu, hatuna maji, umeme unakatika kila mara, hakuna barabara, hakuna hospitali, kula ni taabu! Iweje leo inapotokea viongozi wa dini wanapokemea uovu itafasriwe kuwa ni udini! Haijalishi anayekemea uovu serikalini ni kiongozi wa dhehebu gani, kila mtu kwa uwezo wake wa kuchambua mambo anayopicha halisi ya maisha ya mtanzania kuanzia nafsi yake mwenyewe na jamii inayomzunguka! Leo UDOM wamegoma kwa sababu ya ufinyu wa mawazo yetu tutasema wakristu hawamtaki Kikwete! TUCTA Wataandama tutasema wakristu hatumataki Kikwete! CHADEMA wameandama mnasema Wakristu hawamtaki Kikwete! Hivi huyu Kikwete alichaguliwa na nani kama si wewe, mimi na yule! (Mkristu, Mwislamu na Mpagani). Wekeni mambo ya dini pembeni ongelea hali halisi ya maisha unayoishi kuanzia ndani ya familia yako, jamii inayokuzunguka na taifa kiujumla then utapata jibu kuwa kweli kuna udini ama utawala umeshindwa kutawala na sasa unataka kuwagawa watanzania wamoja kwa kutumia dini. Kimsingi hili halikubaliki maana wote tunaumia!
 

SALAAM ALAEIKUM.Ndugu zangu waislamu wakati mwingine tusishabikie maswala kama ligi ya mpira. Inabidi tuwe analytical. Hivi tumesahau pale Askofu Polikapi Pengo alipomwambia Mkapa kuwa CCM ni kichaka cha majambaz???!!! Wakati Mkapa naye ni Mkristo!!Sasa hapo kulikuwa na udini gani hapo. Hivi kupanda kwa bei ya umeme na hali mbaya tunayoipata sasa hivi inawaathiri wakristo peke yao?? Hela ambazo serikali inataka kuipa DOWANS, hujui itawafaidia akina LOWASA,ROSTAM NA CHENGE?? Sasa hao mapapa watatu na wengine wanyonyaji wanadini hao?
Kama tusiposhikamana pmoja hawa mafisadi wataendelea kutugawa kusudi watunyonye na tubaki na chuki za kidini.
Mafisadi hawana dini,
 
Kwani ni lazima walaani kwa kupitia vyombo vya habari?

sasa wakilaani misikitini ujumbe c utafika kwa waendao msikitini peke yao??yani bado hujui umuhimu wa vyombo vya habari??
 
:angel:Hivi nani wakulaumiwa kwa lililotokea Arusha
1.ni serikali iliyonyima watu wasiandamane bali wafanye mkutano ambao kwa maoni yangu ndo ungezungumza yale yalitaka kuzungumzwa,kwa utulivu na amani na bila kuvuruga hata shughuli za watu wengine????
2.Ni CHADEMA walioamua kwenda kinyume na tamko la serikali na polisi wakatumia fact kwamba wamekiuka taratibu na kwa hiyo wakatumia nguvu?
3.Ni polisi waliotumia nguvu kwa watu waliokiuka agizo la kutokuandamana?
4. Ni kosa kwa BAKWATA kukaa kimya au kuona kama wanavyoona wengine kuwa CHADEMA ilikosea kukiuka agizo la serikali?
5.Kuna haja gani ya kutafuta mchawi na kuacha kujadili hoja za msingi ambazo CHADEMA wanazidai ambazo zinatugusa watanzania wote kama DOWANS, suala la uchaguzi wa Meya na Katiba??????
6.Nani awajibishwe na ni namna gani ya kumwajibisha?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…