Bakora hazimjengi mtoto kinidhamu

Bakora hazimjengi mtoto kinidhamu

Kweli kila MTU anaupeo wa kufikili samahani kidogo embu jaribu tena kufikili
 
Bakora kwa mtoto zinahusika ila sio lazima umchape kila anapo fanya kosa.
 
Habari zenu wanajamvi,

Binafsi nimekuwa nikiwaona wazazi wengi wakiwachapa bakora watoto wao kama njia ya kuwatia nidhamu na nimekuwa nikisikitishwa sana na hii tabia kwani binafsi siamini kama bakora zinamjenga mtoto kinidhamu.

Badala ya kutumia bakora kumtia mtoto nidhamu jiulize kwanza je huyu mtoto anao uwezo wa kuwaza na kuwazua ikiwa anao basi mweleze kwa maneno ya kumjenga, usimpige bakora wala na kitu chochote.

Na kama hana uwezo wa kuwaza na kuwazua basi mwekee vizuizi vitakavyomfanya asiweze kuharibikiwa.

Je wewe una mtazamo gani juu ya bakora?
Mtazamo wako tu
 
Msituletee mila za kizungu mtoto wa kiume anacheza disco na mama yake with zero distance
 
Bakora zinawajenga watoto maana hata kama mtoto alikuwa hataki kufanya Jambo Fulani la kumjenga ila akikumbuka fimbo lazima afanye.
Mfano. Una mtoto nyumbani ni mchafu sana hataki kuoga , umejaribu kumuelimisha bado hataki, ila pale unapoanza kutumia bakora mtoto lazima atayatafuta Maji yako wapi mwisho wa siku anazoea.

KWA mazingira haya fimbo zinakuwa zimemsaidia sana na zimemjenga
Na ukijaribu kufuatilia watoto ambao wanakulia kwa bibi mara nyingi huwa wanakuwa wazembe Kwasababu bakora zinakuwa haziwatembelei
Sii unajua mambo ya mabibi tena.
 
eti bakora nini watoto bila bakora hawaelewi somo lolote tusubiri wale wa mayai ya kupumbaza watakaozaliwa bila m'ke lakini hawa wa kawaida bakora ndio mfumo
 
Wife alikuwa a koto a kisago kwa watoto na matusi juu, matokeo yake watoto wote sasa hivi wanamchukia kabisa . bakora zinajenga chuki badala ya friendship.
 
Kati ya kitu wazazi walikosea ni kuto wachapa watoto wao
Watoto wa sikuhizi wana majibu mabaya sababu ya malezi mabaya
 
Kati ya kitu wazazi walikosea ni kuto wachapa watoto wao
Watoto wa sikuhizi wana majibu mabaya sababu ya malezi mabaya
Tatizo wazazi wengi hawaangalii tatizo linaanzia wapi wao wanakimbilia kulitatua tu kwa kucharaza bakora watoto wao. Katika ulimwengu waetu wa sasa hivi wazazi wanahitaji kuwa karibu sana na watoto wao ili waweze kuwaongoza vizuri lakinimwengi wao hawana mda kabisa na watoto wao halafu watoto wao wakikosea wao wanakimbilia kuwacharaza bakora.
 
Wife alikuwa a koto a kisago kwa watoto na matusi juu, matokeo yake watoto wote sasa hivi wanamchukia kabisa . bakora zinajenga chuki badala ya friendship.
Bakora zinawaharibu watoto kisaikolojia wengine wanakua wakiwa na chuki dhidi ya wale waliokuwa wanawatesa na wengine wanakuwa wakorofi kupita kiasi.
 
hizi habari za kuchapa watoto zipo afrika tu sjui tutaendelea lini na m_bara wetu wa kijinga
 
Habari zenu wanajamvi,

Binafsi nimekuwa nikiwaona wazazi wengi wakiwachapa bakora watoto wao kama njia ya kuwatia nidhamu na nimekuwa nikisikitishwa sana na hii tabia kwani binafsi siamini kama bakora zinamjenga mtoto kinidhamu.

Badala ya kutumia bakora kumtia mtoto nidhamu jiulize kwanza je huyu mtoto anao uwezo wa kuwaza na kuwazua ikiwa anao basi mweleze kwa maneno ya kumjenga, usimpige bakora wala na kitu chochote.

Na kama hana uwezo wa kuwaza na kuwazua basi mwekee vizuizi vitakavyomfanya asiweze kuharibikiwa.

Je wewe una mtazamo gani juu ya bakora?
Kiasi, kila kitu kifanywe kwa kiasi. Ukisema usimwazibu kabisa mtoto Ni sawa na kucheka na nyani shambani
 
nafurahi kuona majadiliano kama haya leo na mimi ngoja nijiunge.

that's true brother. mimi nina miaka 15 it means ni bado mtoto kisheria na maisha yangu yote nilipowahi kupigwa ni shuleni pekee cause wazazi hawajahi nipiga na hawanipigi. na kwa uhalisia niliouna ni kwamba watoto wenzangu wote waliokua wanapigwa now ni drug users,thiefs and any kind of bad behaviors you can predict. bakora haijengi tabia bali tabia hujenga tabia.

In my perspective as a young man or a teenager this is the truth.
bakora isn't the right decision for making right behavior.

My motto is mtoto ana haki ya kusikilizwa. I'm running out of pages.
 
Fafanua kidogo brother.
Watoto hufanya mambo kwa kuiga tu, uwa hawasikilizi wanachoambiwa. So ikiwa utatimia mdomo kila muda bila vitendo hyo Ni sawa na imani bila matendo

KUNA WAKATI NI LAZIMA APEWE ADHABU ILA SI MARA ZOTE
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom