Kuna Viboko kumfanya mtoto aelewe na Kuna Viboko kumpa mtoto Nidhamu!

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
23,905
70,844
Nakumbuka wakati nasoma ,Kuna wanafunzi walikua Wana Uwezo wa kawaida , wengine kupuuza tu mambo Kwa kiburi n.k, Walimu walisimama kidete, Umepewa Kazi hujafanya Makusudi ,Bakoraa !! umepewa Kazi umekosa zaidi ya Nusu ,bakoraaa .. Mimi mwenyewe niliwah Chapwa bakora Kwa sababu ya Mwandiko mbovu !!.
Ndio, Wakati Mwingine Bakora humuogopesha Mwanafunzi ,na kumwondelea Uwezo na wengine Kugeuza Fimbo kama sababu ya Kuacha Shule.

Tukimchukulia yule Dogo wa Mtwara, yeye aliamua kuandika Barua mwenyewe Kwa Mkuu wa Shule, kwamba Bwana eeehh Mimi Kwa hiyari yangu sitaki shule tena, na anahojiwa anasema, Hata Wakimfunga Baba yangu, wao wamfunge lakini Shule siendiiiiiii siendiiii!!.

Je huyu kaacha shule sababu ya Fimbo?.

Kuna Wale Vijana walochoma Bweni kipindi fulan, nakumbuka Hayati JPM alisema, wachapweee Viboko, Wazazi wao waitwe wajenge Bweni, kama hawawez wafukuzwe shule !!.

Je wanafunzi kama Hawa , uharifu Huu ni sababu ya Uwepo wa Fimbo Shuleni?.

Ufaulu Kwa shule za Serikali kua mbaya, Je ni matokeo ya kuwepo Kwa Fimbo mashuleni ?.

Katika kanuni ya KIROHO na kimbingu, ,maandiko yasema

Mithali 13:24. Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.

He that spareth his rod hateth his son: but he that loveth him chasteneth him betimes.....

Hamna Uponyaji wa Akili na Tabia Kwa mtoto awaye yoyote yule hapa chini ya Jua ambaye Wazazi na jamii yake inayomzunguka itaamua kutougusa mwili wake Kwa Fimbo !!.

Leo hiii Bunge Linajadili Et na nyumbani pia kuwekwe Sheria za utoaji adhabu?.

Leo hii Bunge Linajadili Et, Tuondoe Fimbo mashuleni !?.

Kwamba Tuondoe Fimbo katika kizazi ambacho, Wazazi wamekua wahovyoo, wanazaa watoto wanaolelewa hovyo, Leo hii watoto wapo Shuleni Kwa Waalimu ambao nao ni Wazazi, huko Walimu wanahitajika kutumia Fimbo katika kurekebisha tabia fulan fulan za mtoto , Nako mnataka Fimbo zisitumike?.

Ni SHETANI pekee anayejificha nyuma ya Haki za Binadam ndiye aendaye kinyume na maelekezo ya Mwenyezi Mungu , Siku zote SHETANI yupo kinyume na Mungu, SHETANI anapambana Dunia iwe na kizazi Cha hovyooo kisicho na maadili ,kizazi kisichoogopa dhambi !!.

Badala ya Kujadili jinsi ya kulinda watoto dhidi ya Ushoga, mnajadili Fimbo?.

Filamu zinazochochea Ushoga, tamthiliya zinazochochea Ushoga, Jamii kua na lugha chafu mbele ya watoto, kiasi kwamba watoto Leo hii wanafirana Kwa Kasi ya ajabu, watoto wanakua wakiwa hawana Uanaume, badala ya Kujadili namna ya kumlinda huyu mtoto wa kiume, mnajadili kuondoka bakora ??.

ustaharabu gani huuu ?? Unaiga ustaharabu wa Magharibi?. Mataifa ambayo yamejichokea kabisa kinidhamu, Et Nawewe Muafrika, Sasa umuache mtoto wako aseme na atende apendavyo kwakua Kuna haki za Binadam?.

Kizazi Bora kinaandaliwa, Kama lengo ni kuondoka Fimbo kama sehem ya adhabu, Je ni watoto wa aina gani mnawapeleka Shuleni ili Waalimu wetu wanaoishi Kwa shida sana , wasitumie Bakora ?.

Wajibu wa Wazazi katika kurekebisha Tabia za wanao kabla hamjawapeleka shule ni upi? Ili Walimu wetu wabaki na kazi ya kufundisha tu nasio kudeal na Nidhamu ya Mwanafunzi ?.

Kama Lengo ni kuondoa Fimbo ili wafaulu, ni kweli kabisa utafiti mmefanya mkagundua mkiondoa Fimbo watoto watafulu?.

Serikali na Bunge .....

Kwa Ajili ya Taaluma ...

1- Ufaulu ni matokeo ya Uwezo mzuri wa akili , Nchi Ina njaaa hii watoto hawali , amekula saa 10 jion, keshoa ende shule, Sukari imemshuka mwilin, ataelewa??.. HAKIKISHENI MTANZANIA ANAKULA MILO MITATU, HAKIKISHENI WATOTO WANAKULA ILI KUUJENGA UBONGO!!.

2.. Wekezeni Kwa dhati kwenye Elimu .
Mtoto ambaye tayari amekula, ubongo umetulia, anahitaji Mwalimu Bora wa Hesabu, anahitaji Mwalimu Bora wa kingereza ... Unataka Mwanafunzi afaulu hesabu alafu Mwalimu mwenyewe sio mjuzi wa Hesabu niile tu ni Mwalimu kwamba anaweza fundisha lolote Somo???

3-Toeni Motisha Kwa Walimu, Sisi Walimu tuna msemo wetu tunasema "uzuri mwisho wa mwezi mshahara unaingia" .....Hawa Walimu wanahitaji Motisha, mbona Afya tunakula hela mpaka unasema iiihhii Serikali Ina Hela ya kuchezeaa, kwann Walimu msiwakumbuke Kwa Motisha, msiwafanye wakajihisi kunipenda kazi .... Hivi mnajua, Mwalimu wa Tanzania ndio kiumbe mwenye stress za Maisha kuliko hata Mama Ntilie??. Mwalimu anastress za Maisha, anaingia kazin anakutana na Juma macho makubwa haadiki notice Kwa mwezi mzima, mnataka afanyeje ??? Mbona mahela mengi mnayapiga Kwa ufisadi Kila kukicha ?.

4-Wapeni Waalimu Uhuru wa Utumiaji Bakora Ndani ya Darasa kama sehem ya kufundishiaa , Mwalim anafundisha Kuna mtoto anapiga kelele chapa Fimbo , katoa H/Work hujafanya, chapa fimbooo !!.

na Mwalimu atapima Saikolojia ya mtoto Mmoja dhidi ya mwingine IKIWA huyu anaweza elewa Kwa Fimbo, au huyu anahitaji kuelewa Kwa ushauri .... TUSIMUONDOLEE MWALIMU UHURU WA KUTUMIA FIMBO !!.

5-Tuwaboreshee mazingira ya utendaji kazi Hawa Walimu wetu, Madarasa , maabara, michezo pia tuguse.

KWA AJILI YA NIDHAMU

1-Wazazi waache ujinga, Wazazi waache kusukumia nafasi zao Kwa watu wengine, Wazazi ndio Walimu wakwanza wa watoto, Wazazi wawajibike, na WAWACHAPE WATOTO WAO FIMBO, FIMBO HAIUI, CHAPENI WATOTO, MSIWALEE KIMAANDAZI MAANDAZI .

2-WALIMU WASIONDOLEWE NAFASI YAO YA UTUMIAJI WA FIMBO KUREKEBISHA TABIA ., ACHENI WATOTO WACHAPWE MAKALION ILA UWEKWE UTARATIBU MZURI TU NA WALIMU WAUFATE.

3-VIONGOZI WA DINII, MMELALA SANAA,. VIONGOZI WA DINI WAMELALA, NA KUSHUKA KWA NIDHAM ZA WATOTO KWA UJUMLA ,KWA NAMNA MOJA NI MATOKEO YA DINI ZETU KUJIKITA KWENYE MAFUTA YA UPAKO , CHUMVI, UTAJIRI, FEDHA, MAGARI, WANASAHAU KUNA KIZAZI KINACHOHITANI MALEZI, VIONGOZI WA DINI WANAKULA MUDA WA WAZAZI MPAKA WAZAZI WANASHINDWA TIMIZA WAJIBU WAO HOME, HAO HAO VIONGOZI WA DINI , HUWEZ KUTA WANAFUNDISHA JUU YA MALEZI YA WATOTO, KUWAFUNZA WATOTO N.K!!.

4-MTOTO WA MWENZIO NI WA KWAKO, JAMII USIMPUUZE KUMREKEBISHA MTOTO WA MWENZIO.

5-TUMTANGULIZE MUNGU MBELE , KWA SASA PAMBANO KUU NI BAINA YA SHETANI BABA WA MAOVU ,DHIDI YA UUNGU UTAKATIFU... TUMTANGULIZE MUNGU MBEKE., TUOMBEE WATOTO WETU!!.
 
Nakumbuka wakati nasoma ,Kuna wanafunzi walikua Wana Uwezo wa kawaida , wengine kupuuza tu mambo Kwa kiburi n.k, Walimu walisimama kidete, Umepewa Kazi hujafanya Makusudi ,Bakoraa !! umepewa Kazi umekosa zaidi ya Nusu ,bakoraaa .. Mimi mwenyewe niliwah Chapwa bakora Kwa sababu ya Mwandiko mbovu !!.

Ndio, Wakati Mwingine Bakora humuogopesha Mwanafunzi ,na kumwondelea Uwezo na wengine Kugeuza Fimbo kama
Umeongea mambo ya muhimu sana, ubarikiwe sana.
 
Nakumbuka wakati nasoma ,Kuna wanafunzi walikua Wana Uwezo wa kawaida , wengine kupuuza tu mambo Kwa kiburi n.k, Walimu walisimama kidete, Umepewa Kazi hujafanya Makusudi ,Bakoraa !! umepewa Kazi umekosa zaidi ya Nusu ,bakoraaa .. Mimi mwenyewe niliwah Chapwa bakora Kwa sababu ya Mwandiko mbovu !!.
Hayo ndo Masharti ya MIKOPO.

Mtoa PESA ndo huchagua WIMBO,

Tanzania ni Nchi special, Mungu ameichagua kuwa Taifa la mwisho Kwa AGANO lake.

Yuaja mtawala atakayetawala Kwa kufuata Sheria za Mungu.

Matendo makuu ya Mungu yatadhihirika juu ya nchi hii.

Ni Tanzania pekee itakayougomea Utawala wa SHETANI duniani, na wote wamwaminio Mungu watakuja Bandari salama au NYIKANI kujificha na kupata pumziko,

Si mbali, ni KARIBU.

Aaamen.
 
Nakumbuka wakati nasoma ,Kuna wanafunzi walikua Wana Uwezo wa kawaida , wengine kupuuza tu mambo Kwa kiburi n.k, Walimu walisimama kidete, Umepewa Kazi hujafanya Makusudi ,Bakoraa !! umepewa Kazi umekosa zaidi ya Nusu ,bakoraaa .. Mimi mwenyewe niliwah Chapwa bakora Kwa sababu ya Mwandiko mbovu !!.
Uchambuzi mzuri. Lakini mada ni ndefu mno. Nimeshindwa kumaliza kuisoma yote kwa sasa. Labda siku nyingine nikiwa na muda.
 
Nakumbuka wakati nasoma ,Kuna wanafunzi walikua Wana Uwezo wa kawaida , wengine kupuuza tu mambo Kwa kiburi n.k, Walimu walisimama kidete, Umepewa Kazi hujafanya Makusudi ,Bakoraa !! umepewa Kazi umekosa zaidi ya Nusu ,bakoraaa .. Mimi mwenyewe niliwah Chapwa bakora Kwa sababu ya Mwandiko mbovu !!.

Ndio, Wakati Mwingine Bakora humuogopesha Mwanafunzi ,na kumwondelea Uwezo na wengine Kugeuza Fimbo kama sababu ya Kuacha Shule.
Umeongea point za msingi, ubarikiwe. Mtoto ni lazima apate bakora pale anapo enenda kinyume na sheria na taratibu, kitu kinachoitwa haki za binadamu kimekuja kuvuruga familia nyingi, kwani hao watoto wa shule wanatoka kwenye familia na wanaona wazazi wao wanavyo vurugana nyumbani kwa kugombania mamlaka kwenye family level.

Me ndo ningekuwa na mamlaka ya juu hii tabia ningeirekebisha kwa muda wa miaka miwili tu, watu wangerudi kwenye utaratibu wa kiafrika
 
Kuna mambo mengi tu ya ajabu kwenye biblia na hakuna anayeyafuata. Hata kanisani hayasomwi, kila mtu anajifanya hayaoni.

Hata wakati wa biashara ya utumwa watu walitumia biblia hiyohiyo kuhalalisha na kuwaasa watumwa 'wawatii' mabwana zao.

Serikali haiwezi kuacha kuwalinda watoto dhidi ya ukatili eti kisa biblia inasemaje sijui. Ni mambo ya ajabu.
 
Walio walimu naomba waje washuhudie...juzi kati kuna dogo kashakua teja...anajidunga alafu ni form 6..
Ila dalili zilikuepo lakin mwisho fimbo 4...hutakiw kumchapa dogo mpaka kawa teja...
 
Vizazi vyenye maadili na tamaduni vilivyozalishwa na viboko ndio majizi na mafisadi wakubwa walioitia nchi hii na bara hili katika umaskini uliotopea usioisha.
Utandawazi tusipouwekea mikakati, utatuburuza sana. Tutazalisha vizazi vya hovyo sana, visivyo na maadili wala tamaduni.
 
Wote walio katika bunge lenu hawakulelewa katika utandawazi bali katika ujima na wengi wao ni wafahidhina watupu wasiopenda mabadaliko wala utandawazi.

Usiandike tu kama kuku aliyekatwa kichwa.
Na Huu utandawazi , sio tu umekula watoto wetu, ndio umekuka mpaka Bunge letu !!
 
Fimbo na marungu mliyopigwa mkiwa wadogo yamewafikisha wapi wengi wenu zaidi ya kuwaacha makupuku hoehae waoga kama fisi wasio na mbele wala nyuma
Nakumbuka wakati nasoma ,Kuna wanafunzi walikua Wana Uwezo wa kawaida , wengine kupuuza tu mambo Kwa kiburi n.k, Walimu walisimama kidete, Umepewa Kazi hujafanya Makusudi ,Bakoraa !! umepewa Kazi umekosa zaidi ya Nusu ,bakoraaa .. Mimi mwenyewe niliwah Chapwa bakora Kwa sababu ya Mwandiko mbovu !!.
Ndio, Wakati Mwingine Bakora humuogopesha Mwanafunzi ,na kumwondelea Uwezo na wengine Kugeuza Fimbo kama sababu ya Kuacha Shule.
 
Kizazi Cha NYOKA hawataki watoto waadhibiwe Kwa fimbo Ili wakue na UPUMBAVU vichwani mwao na baadae wawe waasi na mashoga.

ADHABU ni lazima Kwa mtoto bt ADHABU iendane na umri na isimdhuru mtoto. Mtoto aadhibiwe na ajue kosa linalosababisha aadhibiwe.
 
Kwanza watoto wa wanaotoa hayo matamko hawasomi katika shule hizo.
Wanaoendelea kuharibikiwa ni watoto wa hao hao raia wa kawaida. wakwangu aadhibiwe tu akikosa na sitawapeleka kwa mkuu wa wilaya wala kituo cha polisi.

.
 
Nitafuatilia mwenendo wake shule, kama kiburi basi viboko alivyovikosa shule atavikuta home. Kuna mitoto bila kuchapa haelewi maelekezo
 
Kwa hiyo Dunia nzima mpaka UN walioona kwamba viboko ni ukatili dhidi ya mtoto ni wajinga na hawajui kulea isipokuwa wewe ? Mbona sasa kote walikopiga marufuku viboko wanapata nobel prizes kila siku ? Isitoshe hakuna watoto wanaolelewa kwa ukatili na chuki kutoka kwa wazazi/walezi wao Dunia hii kama Tanzania lkn Tanzania bado ni ya mwisho katika kila kitu cha kimaendeleo Dunia hii, Panya road walitokea wapi kama viboko vinasaidia chochote?

Kwa kuwa tu wewe ulilelewa kwa ukatili na Wazazi/Walezi haimanishi kwamba ni lazima na wewe uwachukie watoto wako damu yako, mpende mtoto wako klk chochote Dunia hii klk hata unajivyojipenda wewe, na kama ukimpenda mtu huwezi kumfanyia ukatili na unyama, mimi mtoto wangu hata nikisikia tu analia naumia sana, kwa maana nampenda klk najivyojipenda mimi.

Hivi unafahamu hata Mnyama kisheria hauruhusiwi kumpiga? Kuna haki za Wanyama sasa sembuse mtoto ambaye ni damu yako mwenyewe?
 
Hao wanao pinga hadhabu ya viboko ni mazuzu na hawana hoja za msingi kwa sababu ukiwauliza njia mbadala ya kumdhibiti mtoto pale atakapo kosea hawana majibu.

Hivi kama nyinyi watu wazima wenye akili mnao jiita wasomi mmeshindwa kupngozwa kwa mdomo tu mpaka serikali imewawekea polisi ,mahakama na jera sembuse watoto.
 
Kwa hiyo Dunia nzima mpaka UN walioona kwamba viboko ni ukatili dhidi ya mtoto ni wajinga na hawajui kulea isipokuwa wewe ? Mbona sasa kote walikopiga marufuku viboko wanapata nobel prizes kila siku ? Isitoshe hakuna watoto wanaolelewa kwa ukatili na chuki kutoka kwa wazazi/walezi wao Dunia hii kama Tanzania lkn Tanzania bado ni ya mwisho katika kila kitu cha kimaendeleo Dunia hii, Panya road walitokea wapi kama viboko vinasaidia chochote?

Kwa kuwa tu wewe ulilelewa kwa ukatili na Wazazi/Walezi haimanishi kwamba ni lazima na wewe uwachukie watoto wako damu yako, mpende mtoto wako klk chochote Dunia hii klk hata unajivyojipenda wewe, na kama ukimpenda mtu huwezi kumfanyia ukatili na unyama, mimi mtoto wangu hata nikisikia tu analia naumia sana, kwa maana nampenda klk najivyojipenda mimi.

Hivi unafahamu hata Mnyama kisheria hauruhusiwi kumpiga? Kuna haki za Wanyama sasa sembuse mtoto ambaye ni damu yako mwenyewe?
Hao hao walio sema kuwa kupiga mtoto ni ukatiri ndo hao hao walio sema kufanya ushoga na kutoa mimba ni halali.

Kufananisha mfumo wa maisha wa mnyama na binadamu ni upumbavu maana ni mifumo miwili tofauti kabisa.
Kwani mnyama akiuwa au akijeruhi huwa nafungwa jera kama binadamu anavyo fungwa?
Binadamu ameubwa katika mfumo ambao ili haache makosa ni lazima ayajutie na ili ayajutie ni lazima haadhibiwe pale anapo fanya makosa.

Kwahiyo ww mtoto wako akikosea huwa unamuita na kufanyia sherehe na kumpongeza?
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom