Mtoa mada angalia busara zako ztakukosesha malezi bora..!!!
M nnavojua jua nidham Na tabia ya mtoto hujengwa mtoto anapokuwa Na umri Usiozd miaka mitano hadi sita( mlio soma psychology hamta nipinga)..
Kimsing huu ndio umr ambao mtoto anakuwa Na hurka ya kujarb kfanya kla kinacho wezekana maana ndio umri anaojifunza mazngira kw kias kikubwa..
Hivyo katka umri huu sidhan Kama mtoto anakiwa Na utambz Na upeo mkbwa wa kurekebishwa pind anapokosea kwa ktumia maneno Tu Kama unavodai mtoa mada..!!!
Unatakiwa kumkanya Na kumuonya kwa njia itakayo mtia uoga Ili asrudie.....HIYO UNAYOSEMA UTAITUMIA BAADA YA KUSHINDA KUMNYOOSHA KATKA UMRI NILIO UTAJA HAPO JUU..!!
Mimi namchapa mtoto wangu mara chache sana, lakini mara nyingi natumia maneno. Na anafahamu ni wakati gani nimekasirika na ninamaanisha hasa ninachosema. Neno langu moja ni zaidi ya fimbo za mama yake (ambaye anapenda sana kupiga). Hapa simaanishi kwamba watoto waachwe tu wafanye yale wanayojisikia kufanya.
Ninavyopendelea mimi ni kujenga hatua za makanyo kiasi kwamba mtoto anaelewa uzito wa kila hatua pale anapokuwa anafanya makosa. Hata jicho linatosha kumkumbusha mtoto kwamba hapa nimeshaharibu, na adhabu inaweza ikanijia any time. baada ya hapo ni maneno, haya nayo yana ngazi zake, na "tone" inaweza kumpa picha.
Kama alikuwa anaharibu au kuchezea kitu, unaweza kwenda kukitoa kitu hicho au kumtoa yeye, na "utoaji" huo ukiunganisha na maneno inaweza pia kumpa picha mtoto ni kiwango gani haujapendezwa na hilo.
Fimbo au corporal punishment inatakiwa iwe ya mwisho. Nakubaliana na kuwepo kwa option hii ili mtoto anapotaka kufanya kosa afikirie uwezekano wa kutandikwa, jambo ambalo linaweza kusaidia kupunguza "tendency" yake ya kufanya kosa husika.
Tatizo ni kwamba wazazi wengine wanaona kuwa hii ndiyo "the only option" wanayoijua na kuitumia, kwa kosa lolote afanyalo mtoto. Matokeo yake mtoto akishaizoea hali hiyo basi anakuwa nunda maana hakuna adhabu ya kutisha zaidi anayoihofia. Ikifikia hatua hii ndio unakuta wazazi/walezi wanakuwa desperate na kuamua kutumia visu, moto, kunyima chakula, etc baada ya kuona hata fimbo hazifanyi kazi...na ikifikia hatua hiyo, mimi na wewe tunawaita WAKATILI tunapoona matukio hayo yakitangazwa kwenye vyombo vya habari. Tukumbuke kuwa most of the time, inakuwa process hadi kufika hapo.