Bakhresa group punguzeni udini

Status
Not open for further replies.
Kwa hili nadhani itabidi walione mapema Na walipatie ufumbuzi maana ni wazi hili lipo hata counter zao za pale ferry booking office pia azam TV utakutana zaidi Na sura za kipemba tu
 
 
Kwa hawa ulotaja alikuwa hana namna experience waliyonayo upande ule mwingine hawezi pata mtu
 
Mkuu siwezi kukutukana hata moyoni, naomba unisamehe maana inawezekana moyoni umehisi nimekutukana
Kuhusu wingi wa like ni kwamba like haziamui uzito wa hoja, kama ambavyo watu hufanana akili ndivyo hivyo pia huweza kufana ujinga. Nakupenda na kukuheshimu sana ndugu yangu.
 
Yaani hao walishikwa mkono na viongozi wa serikali .
Kampuni yake Kila kitu chake umpangie, vyenu vya Umma (SU) mmevibinafsisha vyote, wafanyakazi tukabaki kama vifaranga vya kuku vilivyofiwa na mama yao na kudhulumiwa juu, majengo yamebaki magofu, watu wanajitolea kuficha aibu ya nchi mnaanza midomo, mbona Mengi kajaza wachaga hamsemi, akiwa upande wa pili midomo juu, mkuu pambana na hali yako
 
Usitetee usichokijua,mkristo anayeajiriwa kwenye viwanda vya bakhresa ni lazima awe mtaalam au na kipaji,wafanyakazi wa chini wote ni waaslam,tena ukiwa shombe hata huandiki maombi,nywele zako ndiyo CV ya kukupa kazi.Povu ruksa
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] wabongo mna manenoo. nimewashindwa aisee. vipi kwa mzee mengi hakuna ubaguzi?
 
Sio kweli wewe ndo mdini unataka kuifanya Azam iwe Vatican na hilo haliwezekani Nazi wanatoa kulingana na sifa zako za taaluma husika sio Dini
Hivi nao watangazaji wa Azam wote ni Waislam ?
 
Hata polisi mahakaman,shule kote umeuliza dini gani tuanzie huko serikalini kwanza halafu time ipp na azam
 
Mkaombe kazi CRDB na IPP huko mtapata, utaalamu huna unataka nani atolewe uajiriwe wewe?
 
Mleta thread una maana..'interview ni kujua kiarabu na juzuu kadhaa,halafu uwe na baraghashia na kanzu mpya,ama unatupia na suruali fupi...na makobanzi..

au sijaelewa?
 
Haya mambo ni kweli yapo, ila yana mizizi mikubwa sana na wala tusihukumu juu juu.
Waanzilishi wa kampuni hii ni muslim, na kama ujuavyo kuwa nchini kwetu kazi tunapeana kindugu au kwa kufahamiana ( ipo na wala usikatae) hivyo basi imetokea "wale kwa wale" ndo wanapeana kwa kuwa "wanafahamiana". Sio kweli kwamba kila muislam lazima apate ajira kama ataomba, ila wataopata ni "waislamu wenye ndugu zao mahala pale", mimi ni muislam na nilishawahi kukosa kazi kwa bakhresa na sikulalama, ni kwa sababu sina "anaenijua".

Tukienda mbele na tukirudi nyuma, kila kampuni huwa na sera zake ambazo wanahisi zitarahisisha "workflow" na kuongeza "efficiency" kwa namna waitakayo wao na hivyo kupelekea upande fulani unaoendana na sera zao kuangaliwa zaidi kuliko upande mwingine.

Mimi ni food technologists & nutritionist, niliwahi kukosa kazi world vision kisa tu sina cheti cha ubatizo na barua ya mchungaji, sikulalamika..! nikaelewa tu kuwa ni sera za taasisi na pengine mazingira ya kazi yangekua magumu kwangu kama nisingekuwa "yule wanayemhitaji".

By the way, sio kila kitengo huwa kina michezo hii, penye credit watu wapewe credit, Last time kuwa pale quality control department ilikuwa na wakenya wengi tu ambao sio 'waislam', hivyo tusiupe sana udini nafasi.

Natumai siku nyingine utafungua uzi mwingine kuelezea "ukabila na udini" kwenye kiwanda cha bwana "dk. Machache" kule "boo-night", naomba msumeno wako ukate kotekote.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…