Bakhresa anakwepa kodi?

Bakhresa anakwepa kodi?

Weka ushahidi wa ukwepaji kodi isije ikawa ni lako jambo! Mtu kuwa na biashara nyingi si kiashirizi za kukwepa kodi..

Mleta mada hebu tupe orodha ya hilo kundi LA walipa kodi wakubwa. Kama huna hiyo orodha basi haya yatakua majungu

Mnachoshangaa hapa ni nini wadau hii nchi unadhani hao wangekuwa nalipa kodi stahiki nani kakwambia Tanzania ni masikini subirini vipimo time will tell nawaambia watu watashikwa na butwaa la mwaka kwa haya makitu yatakayochimbuliwa humo tuombeane uzima mtaulizana tu hata huyu:what:
 
Rais hawezi kufanya kazi ya kuchunguza mwenendo wa ulipaji kodi wa mfanyabiashara mmoja mmoja. Kama ulimwibia akakufukuza kazi acha majungu mwache Bakhresa apige mzigo msimpe mhe Rais kazi zisizo zake.
 
Bakhresa yuko kwenye "big taxpayers bracket". Hilo nina uhakika nalo.
 
Mnachoshangaa hapa ni nini wadau hii nchi unadhani hao wangekuwa nalipa kodi stahiki nani kakwambia Tanzania ni masikini subirini vipimo time will tell nawaambia watu watashikwa na butwaa la mwaka kwa haya makitu yatakayochimbuliwa humo tuombeane uzima mtaulizana tu hata huyu:what:
Tatizo sio kufichua madudu tatizo ni je watawajibishwa sio mtu ana makosa anaondolewa dar anapelekwa mwanza
Tatizo la wa Tanzania wengi tunapenda kujua mwanzo tu ila mwisho hatufatilii kama sakata la escrow ccm nawachukia sana
 
Biashara ya Vyakula,maji, soda ina kodi ndogo sana wanacharge kwa (Lita 1 kodi ni sh.6), mfano chupa ya soda ni ml 350 so mpk ifike Lita 1 ni kama chupa 3 hivi, so chupa 3 za soda anazouza bakhresa au mengi anakatwa sh 6 only.
Nb:siungi mkono ukwepaji wa kodi wa aina yoyote ile
 
Magufuli Naomba umchunguze huyu bwana mwenye Majengo lukuki nchini, maboti ya abiria, mashamba, viwanda Vya vyakula na vinywaji kedekede, Kama analipa kodi sawa na mapato yake.
Achunguzwe mfumo wake wa uajiri Kama unafuata taratibu na sheria, pia Kama analipa P.A.Y.E Kama inavyotakiwa.
Achunguzwe kwa nini hayuko Kwenye kundi LA walipa kodi wakubwa

huo unafiki sasa,hebu lete ushahidi hapa kama inayoonyesha BAKHRESA HALIPI KKODI ili tuamini kama ni kweli!
 
huyu dogo kakurupuka tu,tumeomba ushahidi atuletee hapa kimya.
 
huyo dogo kakurupuka tu, tumeomba alete ushahidi hapa kimya,kaamuwa kutukimbia
 
Tusiongee vitu visivyo na uhakika na ukweli ndani yake. Bakhresa ni mlipaji kodi mzuri na anajipatia Mali zake kwa uhalali kabisa ni muislam swafi huyu Mzee. Mimi ninafanya kazi kwenye moja ya biashara zake kitengo cha mapato hivyo basi naelewa nini ninasema. Lini wafanyakazi wa Bakhresa group of companies tumelalamika kuhusu mishahara au working condition for both skilled na unskilled labor.
 
Magufuli Naomba umchunguze huyu bwana mwenye Majengo lukuki nchini, maboti ya abiria, mashamba, viwanda Vya vyakula na vinywaji kedekede, Kama analipa kodi sawa na mapato yake.
Achunguzwe mfumo wake wa uajiri Kama unafuata taratibu na sheria, pia Kama analipa P.A.Y.E Kama inavyotakiwa.
Achunguzwe kwa nini hayuko Kwenye kundi LA walipa kodi wakubwa

Nifahamishe maana ya P.A.Y.E.
Halafu tutaijadili mada uzuri
 
Magufuli Naomba umchunguze huyu bwana mwenye Majengo lukuki nchini, maboti ya abiria, mashamba, viwanda Vya vyakula na vinywaji kedekede, Kama analipa kodi sawa na mapato yake.
Achunguzwe mfumo wake wa uajiri Kama unafuata taratibu na sheria, pia Kama analipa P.A.Y.E Kama inavyotakiwa.
Achunguzwe kwa nini hayuko Kwenye kundi LA walipa kodi wakubwa
Sina hakika sana lakini Bharesa anamiliki kampuni nyingi na pia sina hakika kama zipi chini ya kampuni moja kubwa.
Kama kila kampuni inajiendesha kipekee, huwezi kuona ulipaji wake wa kodi kwa kuwa kila kampuni inajitegemea.
Angeweza kuonekana kama mlipa kodi mkubwa sana kama wataangalia Majina ya kampuni anazomiliki na kujumlisha kodi yote anayolipa sehemu moja, anaweza kuwa anaongoza kwa ulipaji kodi kama mtu binafsi kupitia kampuni zake lakini kawaida kodi inalipwa kutoka kwenye biashara / kampuni.
 
Magufuli anavyosema wafanya biashara wakubwa hawalipi kodi na TRA haingaiki nao, anamaanisha anachokiongea wala hajaropoka

Ndio hawa akina Bakhresa, Manji, Dewji n.k
 
magufuli naomba umchunguze huyu bwana mwenye majengo lukuki nchini, maboti ya abiria, mashamba, viwanda vya vyakula na vinywaji kedekede, kama analipa kodi sawa na mapato yake.
Achunguzwe mfumo wake wa uajiri kama unafuata taratibu na sheria, pia kama analipa p.a.y.e kama inavyotakiwa.
Achunguzwe kwa nini hayuko kwenye kundi la walipa kodi wakubwa
bakhresa hakwepi kodi na ashawah kupewa tunzo na serikali kwa kuchangia pato kubwa la kodi kwa taifa hili zaidi ni yeye ndo analalamika makato yamekuwa mengi na hizo pesa za kodi aliwahi kuhoji zinakwenda wapi? sababu wanalipa pesa nyingi ila maendeleo hayaonekani!!!!
 
Nilifikiri mtoa mada angetoa details za mianya anayoifahamu kuhusu Bakhresa kumbe hisia tu. Baada ya kutoa uzi wa mafisi basi unaendelea kutoa tuhuma kwa kutumia hisia!!!!!
 
Back
Top Bottom