Bakhresa anakwepa kodi?

Bakhresa anakwepa kodi?

Magufuli Naomba umchunguze huyu bwana mwenye Majengo lukuki nchini, maboti ya abiria, mashamba, viwanda Vya vyakula na vinywaji kedekede, Kama analipa kodi sawa na mapato yake.
Achunguzwe mfumo wake wa uajiri Kama unafuata taratibu na sheria, pia Kama analipa P.A.Y.E Kama inavyotakiwa.
Achunguzwe kwa nini hayuko Kwenye kundi LA walipa kodi wakubwa

Kwanini umtaje Bahkresa mkuu?
Kama kuna unalolijua kuhusu Bahkresa, ni vema ukakiweka wazi ili tupate pa-kuanzia kumjadili.
 
Swali la msingi sana.
...kwanini bakhresa hayupo kwenye orodha ya walipa kodi wakubwa ?

bakhresa ni group of companies, jumuisha kodi za kampuni zote kujua ukweli, vinginevyo yeye binafsi anaweza kuwa analipa p.a.y.e. kama mwajiriwa wa kampuni yake.
 
Bakhresa kwenye vitabu vyake vya hesabu anase anapata hasara! Hii nchi hii
 
Magufuli Naomba umchunguze huyu bwana mwenye Majengo lukuki nchini, maboti ya abiria, mashamba, viwanda Vya vyakula na vinywaji kedekede, Kama analipa kodi sawa na mapato yake.
Achunguzwe mfumo wake wa uajiri Kama unafuata taratibu na sheria, pia Kama analipa P.A.Y.E Kama inavyotakiwa.
Achunguzwe kwa nini hayuko Kwenye kundi LA walipa kodi wakubwa

kwa taarifa yako amna mfanyabiashara anayefanya biashara zake kwa uwazi kama bakhresa , hapata tanzania , biashara zake ziko wazi kabisa na ni rahisi mno kufuatilia , wafanyakazi wanalipwaje, kodi kiasi gani inalipwa ,njoo huku kwa MENGI vibarua wa kutosha , huku wakiingiza superprofi , . mengi ana campuni inaitwa tanzanite africa na kwa kwa makusudi kabisa AMEJIRENK kama mchinbaji mdogo ili asilipi kodi , kwanzia 2007
hadi hii leo anazalisha tone za tanzanite lakini anajificha nyuma ya wachimbaji wadogowadogo
 
Swali la msingi sana.
...kwanini bakhresa hayupo kwenye orodha ya walipa kodi wakubwa ?


mtaji wa biashara yake naskia et alipewa na rais mstaaf mzee ruksa mwinyi enzi zilee, so mwinyi nae ana hisa zake pale,,sijui kama watamgusa,
ila kinyume na hapo labda jamaa hayupo kwenye orodha hiyo labda analipa kodi stahiki ndo maana humuoni kwenye orodha ya wakwepa kodi
 
Bakhresa kwenye vitabu vyake vya hesabu anase anapata hasara! Hii nchi hii
Weka ushaidi wa hayo maneno yako badala ya kupambana na makampuni ya madini hayalipi kodi wewe unapambana na Bakhresa bila data zozote zaidi ya chuki zako tu.

Mitanzania bana.
 
Magufuli Naomba umchunguze huyu bwana mwenye Majengo lukuki nchini, maboti ya abiria, mashamba, viwanda Vya vyakula na vinywaji kedekede, Kama analipa kodi sawa na mapato yake.
Achunguzwe mfumo wake wa uajiri Kama unafuata taratibu na sheria, pia Kama analipa P.A.Y.E Kama inavyotakiwa.
Achunguzwe kwa nini hayuko Kwenye kundi LA walipa kodi wakubwa

Hapo kwenye PAYE makampuni mengi yanapiga pesa unaweza ukafanyakazi kwenye kampuni za wahidi unakatwa PAYE kumbe haiendi mpaka hata kwenye mifuko ya kijamii kuna makampuni hayapeleki....
 
Magufuli Naomba umchunguze huyu bwana mwenye Majengo lukuki nchini, maboti ya abiria, mashamba, viwanda Vya vyakula na vinywaji kedekede, Kama analipa kodi sawa na mapato yake.
Achunguzwe mfumo wake wa uajiri Kama unafuata taratibu na sheria, pia Kama analipa P.A.Y.E Kama inavyotakiwa.
Achunguzwe kwa nini hayuko Kwenye kundi LA walipa kodi wakubwa

ACHA UNAFIKI,BAKHRESA NI MLIPAJI KODI MKUU
i
 
Superman alileta thread mwaka jana, kuhusu walipaji kodi wakubwa


1 Tanzania Telecommunications Company Ltd - Ttcl
2 Tanzania Electric Supply Company Ltd - (Tanesco Ltd)
3 Tanzania Port Authority - (Tanzania Harbours Authority)
4 Tanzania Revenue Authority
5 National Housing Corporation
6 Tanzania Zambia Railway Authority - (Tazara)
7 Tanzania Post Corporation
8 National Service
9 Bank Of Tanzania
10 Parastatal Pensions Fund - (Ppf)
11 National Social Security Fund - (Nssf)
12 Tanzania Postal Bank
13 Vocational Education Training Authority - Veta
14 Dar Es Salaam Water & Sewerage Authority - (Dawasa)
15 National Insurance Corporation Tanzania Ltd - Nic (T) Ltd
16 Tanzania Investment Bank Limited - (Tanzania Investment Bank)
17 Air Tanzania Company Ltd
18 Twiga Bancorp Ltd - (National Bureau De Change Limited)
19 Police Force
20 Wizara Ya Elimu Na Utamaduni
21 Permanent Secretary Ministry Of Finance
22 Ministry Of Defence And National Services
23 Dar Es Salaam Water & Sewerage Corporation - (Dawasco)
24 Tanzania Standard Newspapers Limited
25 National Printing Company Limited
26 University Of Dar-Es-Salaam
27 Dar Es Salaam City Council
28 Muhimbili National Hospital
29 Tazama Pipelines Limited
30 President's Office - Cabinet Secretariet
31 Tanzania National Parks Ltd - Tanapa
32 Ngorongoro Conservation Area Authority
33 Tanzania National Roads Agency - (Tanroads)
34 President's Office
35 Prison Service
36 The National Health Insurance Fund
37 Tanzania Petroleum Development Corporation - Tpdc
38 Ministry Of Natural Resources And Tourism
39 Local Authorities Pensions Fund - Lapf
40 Public Service Pension Fund - Pspf

Source: Verified source but undisclosed

Mleta mada hebu tupe orodha ya hilo kundi LA walipa kodi wakubwa. Kama huna hiyo orodha basi haya yatakua majungu

Weka ushahidi wa ukwepaji kodi isije ikawa ni lako jambo! Mtu kuwa na biashara nyingi si kiashirizi za kukwepa kodi..
 
Last edited by a moderator:
Jackbauer naye alishawahi post hili.

Kwa ufupi😱nly one mining company,one telecom company,no gas/fuel company!!

1.TBL(Tsh bilioni 165.4)

2.NMB(Tsh bilioni 108.6)

3.TCC (Tsh bilioni 92.1)

4.NBC (Tsh bilioni 89.9)

5.CRDB Bank Ltd(Tsh bilioni 79.2)

6.Tanzani Ports Authority(Tsh bilioni 76.8)

7.Tanzania Portland Authority(Tsh 73.4 bilioni)

8.Airtel(T) Ltd(Tsh bilioni 63.6)

9.Tanga cement company Ltd(Tsh 43.6)

10.Standard chartered Bank Ltd(Tsh bilioni 40)

11.Citibank(T) Ltd(Tsh bilioni 35.7)

12.Resolute(T) Ltd(Tsh bilioni 32.1)

13.TICTS(Tsh bilioni 25.9)

14.Tanzania Distillers Ltd(Tsh bilioni 13.4)

15.Group five international(PTY) Ltd(Tsh bilioni 9.5)

source:hotuba ya waziri mkuu bungeni tarehe 28/8/2011.
 
Last edited by a moderator:
Walipa Kodi 15 Wakubwa Tanzania (Tanzania Top 15 Tax payers) & the missing household names
Posted by zittokabwe
Kutoka Hotuba ya Waziri Mkuu 26.08.2011 ? Makampuni yanayoogoza kwa kulipa kodi
Note: (Highlights)
Only one Mining company (the smallest ie Resolute Mining), only one telecom company(Airtel Tanzania).
Household names like MeTL, Bakhresa/Azam, IPP, VodaCom, Coca cola, Pepsi(SABCO), Serengeti Breweries, Barrick Gold, AngloGold Ashanti not seen. No oil marketing companies pia.
One can conclude that, TBL is the most profitable company in Tanzania, NMB is the most profitable Bank.
A public debate is needed.
Here under is the an extract from the Prime Minister speech;
Mheshimiwa Spika,
1. Nitumie nafasi hii kuwapongeza baadhi ya Walipakodi Wakubwa kwa Serikali na ambao wamefanya vizuri kati ya kipindi cha mwaka 2005 na 2011. Kwa kipindi hicho, Makampuni yaliyoongoza kwa kulipa kodi ni pamoja na:
i. Tanzania Breweries Ltd. (Shilingi Bilioni 165.4 );
ii. National Microfinance Bank (Shilingi Bilioni 108.6 );
iii. Tanzania Cigarette Company (Shilingi Bilioni 92.1 );
iv. National Bank of Commerce (Shilingi Bilioni 89.9 );
v. CRDB Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 79.2 );
vi. Tanzania Ports Authority (Shilingi Bilioni 76.8 );
vii. Tanzania Portland Cement (Shilingi Bilioni 73.4 );
viii. Airtel (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 63.6 );
ix. Tanga Cement Company Ltd. (Shilingi Bilioni 43.6 );
x. Standard Chartered Bank Ltd. (Shilingi Bilioni 40.0 );
xi. Citibank (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 35.7 );
xii. Resolute (T) Ltd. (Shilingi Bilioni 32.1 );
xiii. Tanzania International Container Terminal Services (Shilingi Bilioni 25.9 );
xiv. Tanzania Distillers Ltd. (Shilingi Bilioni 13.4 ); na
xv. Group Five International (PTY) Ltd. (Shilingi Bilioni 9.5 ).
2. Napenda kutoa rai kwa Makampuni yote Nchini kuiga mfano huu mzuri. Wito wangu kwa Makampuni, Wafanyabiashara Wakubwa kwa Wadogo na Wananchi wote ni kuongeza juhudi katika kufanya biashara zao ili zizalishe kwa wingi na kupata faida kubwa zaidi. Faida kubwa itachangia katika kuongeza Mapato ya Serikali kwa njia ya Kodi na hivyo kusaidia kukuza uchumi, kuongeza Pato la Taifa na la Mwananchi mmoja mmoja na kuondoa Umaskini. Niwadhihirishieni kwamba, Serikali inatambua umuhimu wao kwa maendeleo ya Nchi yetu na itahakikisha inaongeza juhudi zake za kuweka Mazingira Wezeshi kwa Makampuni hayo kufanya shughuli zao vizuri ili kuwezesha kulipa Kodi kwa mujibu wa Sheria.
Loading...
 
Jibu ni rahisi,tuache kutumia bidhaa za wakwepa kodi. Mimi naanza kwa baadhi ya bidhaa ya huyu Bakhresa
 
Weka ushahidi wa ukwepaji kodi isije ikawa ni lako jambo! Mtu kuwa na biashara nyingi si kiashirizi za kukwepa kodi..

TRA hutoa orodha ya walipa kodi wakubwa na kuwatunuku vyeti. Katika orodha ya makampuni 10 hakuna hata moja linalomilikiwa na Bakharesa!
Ajabu yeye yupo kwenye orodha ya matajiri wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika!
Mbona Reginald Mengi anaezidiwa utajiri na huyu bwana yeye yupo kwenye orodha ya walipa kodi wakubwa???
(orodha ya walipa kodi mwaka juzi)
Kuna haja ya kumchunguza Bakhresa!
 
TRA hutoa orodha ya walipa kodi wakubwa na kuwatunuku vyeti. Katika orodha ya makampuni 10 hakuna hata moja linalomilikiwa na Bakharesa!
Ajabu yeye yupo kwenye orodha ya matajiri wakubwa Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika!
Mbona Reginald Mengi anaezidiwa utajiri na huyu bwana yeye yupo kwenye orodha ya walipa kodi wakubwa???
Kuna haja ya kumchunguza Bakhresa!
Bora useme achunguzwe kuliko kusema alipi kodi..
 
Kama hawalipi kodi nani analipa kodi ? wewe unalipa ngapi ?
Kulipa kodi sawa lakini kama ukomoe watu kwa kodi za TRA za kubambikiza kuna athari katika uzalishaji na bei ya bidhaa zitapanda na watu hawatakua na uwezo wa kununua hatimae viwanda vitakufa na kazi nazo zitakwenda arijojo.

kila mtu ana andika pumba zake humu kwa chuki za kijinga . serikali haina njia ya mapato zaidi ya kodi za wafanya biashara.Na cha kustajaabisha ni kuwa hizi choko choko zinaelekezwa kwa makampuni ya ndani ambayo yanalipa hio kodi ambayo serikali inajidai nayo. HAKUNA HATA MMOJA AMBAYE ANO ONGELEA SUALA MADINI NA KODI ZAKE.HAWA HAWALIPI kodi na wanasafirisha madini bila ya kufanyiwa audit. miaka 20 sasa na nchi haijafaidika chochote na secta ya madini.

kufukuza watu makini kama kina Rished Babde wa TRA kwa sababu za hisia wakati TRA imekusanya 97% ya malengo yake mpaka sasa hivi ni kukurupuka.
hayo makontena 300 yallopotea ni katika ripoti ya uchunguzi ya Barde na tayari alishachukua hatua za kuwafata wahusika. alishawaandikia barua ya kulipa kodi kwa macontena yao.
wengine waliyatoa kwa mashinikizo na maagizo lakini yeye kama kuchukua tahadhari aliweka rekodi na kuwaaindikia.

discpline ni muhimi katika sehemu za kazi pamoja na uadilifu lakini maamuzi ya pupa bila ya taarifa za uhakika juu ya chanzo cha haya ..sasa tuchukulie mfano yale makontena yalitoka kwa ajili ya kusaidia kampeni za ccm ? watu wataumbuana katika hili jambo.

tunahitaji sera ya uchumi , sera ya kuongeza uzalishaji na sera ya ajira. kuwabana wafanya biashara kwa makodi makubwa ndio chanzo cha kukwepa kodi ..kodi ni kubwa mno kiasi hata TRA wenyewe hawaelewi namna ya kuzitoza . Leo ukiagiza nondo basi mpaka imfikie mlaji itakua imetozwa kodi ya asilimia zaidi 60% ..TRA wanapata faida zaidi ya huyo muagiziaji na hata mwenye kiwanda huko uturuki.. biashara haziwezi kwenda namna hio....
 
kibaya zaidi huyu jamaa anauza mpaka maandazi na chapati zilizokua ziuzwe na mama ntilie.
 
Back
Top Bottom