Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread


home affairs kunani? hawajui kutengeneza bajeti au ndio wamepigwa panga? home affairs bajeti yao haifiki hata nusu ya ministry of defence? duh

kuna tofauti gani kati ya defence and ministry of defence na national service?


haya mambo ya sheria mbona yemegawanywa gawanywa hivi, ndio kusema kule wizara ya sheria na mambo ya katiba kumejaa wameshindwa kushindilia.
 
hii bajeti ni muhimu sana kwani utegemezi wa nje umepungua na serikali imeongeza bajeti ya elimu. Kikwete anafanya kazi ila wapinzani wake hawaoni hili.

Hongera Kikwete na serikali yako kwa kazi nzuri hasa kwenye bajeti ya mwaka huu.
 
hii bajeti ni muhimu sana kwani utegemezi wa nje umepungua na serikali imeongeza bajeti ya elimu. Kikwete anafanya kazi ila wapinzani wake hawaoni hili.

Hongera Kikwete na serikali yako kwa kazi nzuri hasa kwenye bajeti ya mwaka huu.

Kitu ambacho serikali ya Tanzania ilichokuwa inakikosa ni CONSISTENCY; kwa bajeti ya mwaka huu nawapongeza kwa sababu vipaumbele vimeendelea vile vile... this means tukifanya hivyo for the next 3 years... tutakuwa mahali.

Angalia kwa mfano... sasa hivi baada ya miundo mbinu ya elimu kuboreshwa... sasa watu wengi wanahamia kwenye UBORA... and this is a nice challenge.
 
Donors drag feet on budget support

2008-06-11 09:28:32
By Guardian Reporter


Development partners are yet to make final decisions on disbursement to the 2008/09 budget until they receive substantive progressive reports on the government`s commitment to tackling corruption.

They also want to see improvements in governance and implementation of the Controller and Auditor General`s recommendations related to the EPA account and Bank of Tanzania 2005/06 audit.

The chairman of the donors` group, Danish Ambassador Bjarne Sorensen, told The Guardian yesterday that constructive dialogue between the government and the development partners was still going on.

``We will continue to meet regularly with the Finance and Economic Planning Minister to monitor and facilitate further progress,`` he said.

He, however, said the donors group, which provides budget support to Tanzania, had already submitted its budget support commitments for the 2008/09 financial year.

``On the other hand, before making their final decision, the development partners are looking towards receiving further information on work currently in progress to deal with bribery allegations,`` said Sorensen.

He said the government was making good progress towards ensuring the right conditions for general budget support in 2008/09 existed.

Donors seem hesitant to support the government, following reports of massive corruption and embezzlement of billions of shillings in government institutions, including the Bank of Tanzania (BOT).

Initially, there were fears that some development partners might scale down their budget support because of the high profile bribery scandals.

Finance and Economic Planning Minister, Mustafa Mkullo was recently quoted as saying that donors might hesitate to support the government.

In of spite the donors` apparent reversal of their rigid stance after renewing their pledge to continue financing the country`s budget, the government has already announced its intention to make the budget locally-financed in the long run.

According to the finance minister, the government intends to reduce donor dependence.

In the budget proposals expected to be tabled in Parliament this week, donors` contributions will be cut down from 41 per cent in 2007/08 budget to 34 percent.

Prime Minister Mizengo Pinda has already been quoted as stating that the government is committed at self-financing its annual budget by at least 70 per cent.

The government expects to increase spending by 19 percent during the 2008/09 financial year to 7.22 trillion shillings (USD 6.05bn), the bulk of which will go to education, infrastructure and health.

But analysts say the government needs to widen its sources of tax revenue to non-traditional areas like mining and logging.

The prospect of the government raising all its domestic revenues without resorting to borrowing in the domestic market is also a welcome move, observers said.

``We should expect interest rate levels to stabilize if the government lives up to its promises of not coming to borrow from the market,`` Christopher Makombe, head of trading at Standard Chartered Tanzania, told Reuters.

Tanzania largely relies on agriculture, tourism and mining, and it is increasingly attracting investment in financial services and telecommunications.

Business wants better infrastructure and improved power supply, which is erratic.

Tanzania, Kenya and Uganda will table their budgets on Thursday.

SOURCE: Guardian
 
Kwani Tanzania kuna Bajeti?Mi nilisikia zamani kidogo kuwa Karibu sehemu yote ya Huo mpangilio wa Matumizi ya pesa inatoka kwa wafadhili ni kweli?Na mwaka huu si nasikia kuna baadhi ya wadau wa ng'ambo wmetishia nyau kuwa hawatachangia kiasi kikubwa kwenye mambo hayo kwa sababu Tanzania imekua nchi ya "Kufisadika".

Hivi kuna ka chuo wanakofundisha kozi ya ufisadi maana kuna mwanangu anaisumbua kutaka kujiunga huko! Kidding
 
Bajeti ya TZ inachekesha sana eti KILIMO imepewa 6% ya bajeti yote.
Kila kukicha wanaimba ''KILIMO NI UTI WA MGONGO'' na % kubwa ya waTZ ni wakulima je ni haki kuwatengea hawa wakulima 6% na ukizingatia ndo wapiga kula wao.
Huku bajeti hii ikiwaneemesha wao watunga sera na kuwaacha wakulima ambao ndo walalahoi wakipiga miayo tu.
Kwa khari hii tunastahili kwendelea kuwa maskini wakutupwa tu.
 
Look here!

Nyie donors..This is the time mkae chini mtafakari "Busara toka kwa Walala hoi"

We have said it time and again...Wala hizo donation zenu hatujui zinako kwenda. Ni majuzi tu tumesikia kumbe kuna "shimo la kuzimeza" hapo BANK KUU.

So ...? Get to know kwamba hatuishi wala kuwa sustained na hiyo misaada yenu. Na hapo ndipo... Labda mtuulize tumedunda vipi all that time.

Sisi Donor wetu ni Mungu Tu!

Kwani kama sio hivyo leo hii tungewasilianaje? Mapesa wanaita vipesa..its all very sad.

SiSi hatumjui mwingine zadi ya Mugu yule tunayemuimba kila siku kwenye wimbo wa taifa letu, maana tangu tupate uhuru hatujawahi kumona mfadhili wala kupata fukuto lake. Lakini tunaishi...Na huo ..Utanzania huo.

Leo mnapokuja kutuambia habari za Donors watia ngumu, EPA, BANK KUU that is you matter..sisi wa "jua kali" ..inatuhusu nini?

See? watuhumiwa.. wanaotajwa na kusemekana wanazirudisha Ni size yetu kweli..Sisi makabwela ..tunafit wapi? Msitughasi tuko bussy na shughuli zetu.

"So please take your time... dont waste our time.." Tunawahi msikitini na makanisani kufanya last reconciliation na the only donor ambaye has been with as for all that time, ..."Mungu" Ibariki Tanzania...Hako kawimbo ndio salam na sala yetu..and you know what? It works. Before we sleep tunajikusanya tunaimba...asubuhi kabla ya kukimbia vijiweni tunajikusanya tunaimba na kujipa moyo...then tunawahi!

Tumelia na kulia.

Tukasema nama ya kuwalipua hawa mafisadi wanaokula na kuteketeza ..all the donation..ni kusimamisha ufadhili..."They will die and we will Live..." hiyo ni kanuni ya donor wangu... Mungu ...ibariki..! Na muasisi aliwahi kufanya hii jeuri ninayoisema hapa na tuliona dalili... Lakini leo? Mh!!!

Sisi tutakufa kwa vipi? Let them withdraw...!

Lini tumeshawahi kuwa affected na ..what you call Donation? Waulize hao wa vijisenti..at al. I know watagara gara kama samaki aliyetupwa nchi kavu. Lakini sisi? Oh Tumesha evolve..breathing system nyingine... Tunaweza kuishi majini na nchi kavu...Shida zilitufundisha hayo.....wao? I swear..it wont take a minute..they will all die. Sisi tukikumbuka kale kawimbo ketu..oh we get energized...tunadunda. Wafadhili kitu gani bwana na katiba inasema kujitegemea ..sisi ndio tunajitegemea bwana.

Nyie wafadhili nyie...

Nanyi mkae choncho siku moja tutawapandia huko mliko...kwani nyie na mafisadi lenu moja..!

Inakuwaje wachezee Misaada na nyie muedelee kuwapa?

Kumuongezea kinywaji mlevi ni kumtibu? au sio!!?

Sikama mnawafanya mazezeta?

Kwani hawajawa?

Unaiba mchana kweupe all the money hapo EPA alafu wanatangaziana kurudisha wao kwa wao? what is that? si kilevi juu ya ulevi? Waona wamejifunika na hawaonekani. Really?

Vipi mtoto wako achezee pocket money ..na wewe uendelee kumzidishia kama sio unamfanya ..zezeta. si kama unambomolea UTU wake?

Wafadhili? Stop the game you are playing with our viongozi mafisadi.

Stop taking their humanity away! Tumechoka kuongozwa na Watu wasio Na utu....Nusu watu..nusu wanyama/wafisadi.

Stop it now ..and dstop the Donation!!

They wiil die and we will Live.

Good Lord..bless our Nation.
 
Bajeti ya TZ inachekesha sana eti KILIMO imepewa 6% ya bajeti yote.
Kila kukicha wanaimba ''KILIMO NI UTI WA MGONGO'' na % kubwa ya waTZ ni wakulima je ni haki kuwatengea hawa wakulima 6% na ukizingatia ndo wapiga kula wao.
Huku bajeti hii ikiwaneemesha wao watunga sera na kuwaacha wakulima ambao ndo walalahoi wakipiga miayo tu.
Kwa khari hii tunastahili kwendelea kuwa maskini wakutupwa tu.

wapewe pesa nyingi za nini,kilimo chao ni cha jembe la mkono,kuku wanakula kwa kujitafutia chakula wao wenyewe,ngombe,mbuzi,kondoo wanakula majani mwituni,mbwa makombo ya mabwana zao.sasa ukiwaongezea hizo pesa ili wanunue nini ?,bei ya mafuta imepanda kwa hiyo hatuna haja ya matrecka kwa ajili ya kubana matumizi.mbolea ni kinyesi cha mifugo.naungana na mkulo kwa kuipa pesa kidogo.
 
Eti wanajiita parteners wa maendeleo .Nyooooooooooooooooooo.Mnaendeleza wizi .Mnatoa kidogo na kufadhili kutunza pesa nje na deal chafu .You create jobs for your own people in my own country then mnakimbilia CNN kuonyesha plights magomeni na kusema kuna drugs na hakuna kazi na maisha mabovu .It is time watanzania tuamke na kuwasemewa mbovu hawa .Ni wezi na wajanja kama Sullivan .
 
Huu ni muziki wa kawaida tu ingawa nimeamua kuuwahisha kablaya Mkulo, enjoy
 

Attachments

  • BEJETI 2009.doc
    226 KB · Views: 249
This caught my attention:

e) Katika bajeti ya Nishati na Madini, ni vyema nieleze kwamba zile fedha zitokanazo na kufutiwa madeni ya IMF (MDRI), ambazo zilitumika kulipia mitambo na jenereta za kuzalisha umeme wa dharura na kulipia chakula likichoagizwa kutoka nje wakati ule wa uhaba wa chakula sasa zimekwisha. Hivyo miradi katika sekta hiyo sasa itategemea fedha za wahisani pamoja na za kwetu wenyewe. (Kifungu cha 44)

my reaction?.. Uh!! .. just like that "sasa zimekwisha"? Gademu!!

Nimesoma hotuba hiyo one thing is missing and it has been missing katika bajeti zetu nyingi... wachumi mtanisaidia..

"how much does corruption affects our budgeting hasa suala la suspending ya serikali na ukusanyaji wa mapato? Je corruption kubwa haina adverse effect katika kubajeti?"

Katika hotuba nzima neno "rushwa, ufisadi, wizi, au upotevu" hayaonekani.... tunaishi katika sayari gani?
 
halafu huu mtindo wa lazima kubadilisha kodi kila mwaka hasa kwenye vitu vya anasa (kileo, sigara n.k) utakoma lini? Yaani bado wanafanya mambo ya "classical economy" bila kuangalia mabadiliko makubwa ambayo yametokea katika uendeshaji wa serikali duniani. Ni kweli kanuni za uchumi nyingi zinaendelea kubakia jinsi zilivyo lakini linapokuja suala la matumizi na usimamizi wa fedha za umma, serikali nyingi zimeanza kufuata a very different approach ambayo inategemea sana private sector, more on regulation n.k lakini kwenye sisi bado tunazungusha mambo mengi ndani ya serikali kuu kuja serikali ya mitaa, halmashauri n.k ..
 
Huu ni muziki wa kawaida tu ingawa nimeamua kuuwahisha kablaya Mkulo, enjoy

Naona JF tuko kwenye right track, tunachukua nafasi ya kuwa wabunge bubu ambao hutukuchaguliwa lakini hakuna kuona aibu ni kumkoma nyani tu. I LOVE JF - Bajeti ndio hii! Ngoja tuichungulie kwa makini.
 
Bajeti 2008/09: Mambo Magumu!

2008-06-11 18:01:14
Na Sharon Sauwa, Jijini


Wakati Waziri wa Fedha na Mambo ya Uchumi, Mhe. Mustafa Mkulo akitarajiwa kuwasilisha bajeti ya mwaka 2008/09 katika mkutano wa 12 wa Bunge kesho, bei ya vitu imepanda maradufu kulinganisha na kipato na hivyo kuwafanya wananchi wengi kuwa na maisha magumu zaidi.

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa gazeti hili katika baadhi ya maeneo Jijini, umebaini kuwa bei ya bidhaa na huduma mbalimbali muhimu zimepanda mno na hivyo Serikali, kupitia kwenye bajeti yake itakayotangazwa kesho, kuwa na changamoto ya kulainisha makali hayo ya maisha kwa wananchi wake ambao yenyewe inataka wawe na maisha bora.

Mwandishi amebaini kuwa mbali na pesa nyingi wanazolipa wakazi wa Jijini kutokana na kupanda kwa gharama za usafiri, pia vyakula, huduma za matibabu, umeme na hata vifaa vya ujenzi vimepanda mno kwa namna inayofanya maisha yawe magumu zaidi.

Wakati nauli ya daladala ikiwa shaghalabaghala na kutozwa kati ya Sh. 250 hadi Sh. 1,000 kulingana na eneo na umbali wa safari yenyewe, katika baadhi ya maeneo mengi Jijini, unga wa mahindi huuzwa kati ya Sh. 700 hadi 800 kwa ujazo wa kilo moja.

Mwandishi wa Alasiri amebaini kuwa mchele huuzwa kati ya Sh. 900 hadi Sh. 1,300, maharage Sh. 1,200 hadi Sh. 1,500 huku kipimo kimoja cha mkaa kikiwa kati ya Sh. 700, 1,000 na hadi Sh. 1,200 kwa maeneo kama ya Kimara Bonyokwa.

Aidha, mwandishi amebaini kuwa bidhaa nyingine zilizo katika bei ya juu ni vitunguu na nyanya ambavyo vyote, huuzwa kwa wastani wa Sh. 100 kwa kimoja, au Sh. 400 kwa fungu lenye nyanya tatu hadi nne au vitunguu vya idadi hiyo huku fungu la bamia likiuzwa kati ya Sh. 100 na 300.

Hata hivyo, bei ya nyama ya kawaida imekuwa kimbilio la wengi kwa sasa, kutokana na ukweli kuwa yenyewe imeendelea kuuzwa kwa wastani wa Sh. 2,800 hadi 3,500, kulingana na eneo.

Sukari nayo huuzwa kwa Sh. 1,000 hadi Sh. 1,200 kwa kilo, mafuta ya kula huuzwa Sh. 150 kwa kipimo kidogo kabisa kwenye maeneo kama ya Tandale na Buguruni huku fungu la bamia ni sh 100.

Mwandishi amebaini vilevile kuwa bei ya samaki imekuwa haishikiki, ingawa hushuka kidogo pale wanapovuliwa kwa wingi wakati bahari inapotulia na giza kutawala usiku.

Bei ya dagaa wanaopendwa zaidi toka Kigoma huuzwa kwa kati ya Sh. 7000 hadi sh 9,000, nanasi Sh.1,000 na 1,500, embe dodo sh. 500 hadi 700 na machungwa Sh.100 hadi 150.

Aidha, bei ya maji yanayouzwa kwenye madumu katika maeneo yenye shida ya maji huuzwa kwa kati ya Sh. 300 hadi Sh. 500 kwa dumu moja la lita 20.

Nayo bei ya mafuta ambayo hutajwa kuwa ni sababu kubwa zaidi ya kupanda kwa maisha imeendelea kupanda siku hadi siku ambapo sasa, katika baadhi ya vituo vya mafuta, dizeli huuzwa kwa Sh. 1,950 kwa lita, Petroli Sh. 1850 na mafuta ya taa Sh. 1,300.

Hata hivyo, kwa mujibu wa taarifa zilizopo, ni kwamba kupanda kwa bei ya mafuta kunachangiwa pia na bei yake katika soko la dunia.

Kwa mujibu wa mwelekeo wa bajeti ya 2008/2009 uliotolewa na Waziri Mkullo, Serikali haitarajii kuongeza ushuru wa mafuta ya dizeli na petroli.

Walipoulizwa kuhusiana na maoni yao ya kupanda kwa gharama za maisha kusikoendana na kipato, baadhi ya wabunge wamekaririwa na vyombo vya habari wakisema kuwa watashupalia sula hilo baada ya kutangazwa kwa bajeti hiyo kesho.

SOURCE: Alasiri
 
hii bajeti ni muhimu sana kwani utegemezi wa nje umepungua na serikali imeongeza bajeti ya elimu. Kikwete anafanya kazi ila wapinzani wake hawaoni hili.

Hongera Kikwete na serikali yako kwa kazi nzuri hasa kwenye bajeti ya mwaka huu.

Mwenzetu ushaiona bajeti kabla hata ya kusomwa!!!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom