Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bajeti ya Serikali 2008/09 - Exclusive Thread

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Steve Dii, May 3, 2008.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni statement inayotia matumaini... hata hivyo mambo bado kabisa, tunahitaji kukusanya 'vijisenti' vyote toka kwa wahalifu na kuboresha vitega uchumi vyetu na miundombinu zetu, wakati huo huo tukiwekea mkazo kuondokana na hii 'donor dependency syndrome' kwa asilimia 100.

  Source: IppMedia.com


  SteveD.
   
 2. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  huyo nae badala ya kutueleza lile swala letu limefikia wapi!! anaanza style zilezile za kina mramba na Yonna,,atueleze kuhusu uvujaji wa fedha pale BOT ukiachia mbali EPA
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Nyerererist, yote uliyosema ni sawa, ila hili nalo linatia matumaini...indirectly labda kwa kutoa ahadi kama hiyo kutawafanya wafatilie kwa undani ufujaji mali ulioenea sehemu mbalimbali... hivyo the end result would still be positive.


  SteveD
   
 4. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  may be steve, otherwise lets pray for miracles...
   
 5. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  "The forthcoming 2008/09 budget should at least guarantee that we can pay salaries to public servants and leave development budget to be catered for by aid from donor community".

  Hii inasikitisha sana, na ukiwambia kuwa CCM na Serikali wameshindwa kuleta maendelea wanaweza kukataa. Kama mawaziri wanaweza kuwa na vijisenti vingi nje ya nchi, bila shaka kama vingetumika hapa nyumbani basi tungekuwa mbali sana na tusingekuwa hapa tulipo!
   
 6. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ....Bongolander, lakini unaona hapo juu jinsi alivyo jihami na hayo hayo aliyosema?......au nimemwelewa vibaya...
   
 7. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  natamani nimuulize Mkulo kwa nini hela tanzania bado expensive (interest rate 18%-22%) halafu kama waziri wa vijisent wala haongelei kabisa analeta siasa,,anyway may be italeta some changes,, lets wait and see
   
 8. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2008
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ni habari nzuri but its strange...Ghafla hayo yanawezekana?

  Swali ni .... nini hasa kimepelekea hayo kuwezekana?
   
 9. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Hiki bado ni kichekesho, hakuna kujitegemea kokote alikotaja hapo zaidi ya reallocation! Yaani anachosema ni kuwa badala ya donors kufadhili 40% matumizi ya kawaida ya serikali na asilimia fulani ya matumizi ya maendeleo, sasa serikali inagawana majukumu na wafadhili ambapo sasa serikali itagharamia yenyewe bajeti yote ya matumizi ya kawaida na kuwaachia wafadhali bajeti ya maendeleo! Yaleyale tu, changa la macho. Zile tulizokuwa tunatumia kwenye maendeleo zote tumerudisha kwenye matumizi ya kawaida na kuwaachia wafadhili bajeti ya maendeleo. Usanii wa kipuuzi tu, alianza kutudanganya kuwa shilingi inaongezeka thamani akidhani sisi ni watoto wadogo kuwa hatujui hizo hesabu za kuilinganisha shilingi inayoporomoka na dola ya Marekani inayoporomoka pia! Sasa anatuletea usanii wa kuhamisha hela kutoka mfuko mmoja kwenda mwingine na kutudanganya zimeongezeka! Huyu ni wa kuzomea!
   
 10. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...Azimio, sababu alizotoa za kufanikisha hilo, yaani makusanyo ya kodi n.k. ilitakiwa wabunge wamuulize, je tofauti ya makusanyo hayo ya bajeti zilizopita na hii bajeti tarajio ni kiasi gani..... ili kujua kama ulivyo uliza kwanini haikuwezekana hapo kabla....

  ....mimi kikubwa ninachofikiri hapa ni kuwa, tofauti za makadirio katika tofauti za bajeti hazitakuwa kubwa, ila hii hoja ni mabadiliko ya msimamo wa kisera unaosababishwa na kero na madukuduku ya wananchi yaliyo enea kila kona na kuonekana waziwazi kivitendo wakitaka majibu.

  SteveD.
   
 11. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kithuku, very good insight!!
   
 12. Power to the People

  Power to the People JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2008
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 1,193
  Likes Received: 238
  Trophy Points: 160
  i hope haya makusanyo ya kodi yatabaki huko huko kwenye madini na utalii na sio mzigo kuongezwa kwa walala hoi kama ilivyo kawaida ya viongozi wa wa hii nchi
   
 13. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ni kitu cha ajabu kuwakabidhi bajeti ya maendeleo wafadhili,,Steve tunaweza tukapata summary ya hiyo exp-budget?? samahanni lakini
   
 14. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #14
  May 3, 2008
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Ukweli ni kwamba serikali haina uhakika kwa sasa na fedha toka kwa wafadhili kutokana na kushindwa kushughulikia ufisadi mkubwa uliopita na unaondelea.
  Hili swala la wafadhili ku-freeze misaada limeongelewa sana na Mkulo amekanusha mara nyingi tu lakini sasa ukianza kusikia sentensi toka serikali hiyohiyo kuwa "serikali kujitegemea katika bajeti ya matumizi ya ndani" ni dalili tu kuwa ukweli uko mbioni na kama imefikia serikali kutangaza hivyo jua matumaini yao ya kuwashawishi wafadhili wao yanazidi kupungua
   
 15. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2008
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  SteveD, kweli kuna ka-ujanja kwenye hiyo sentense yake, lakini mimi kwa maoni yangu ilitakiwa kuwa vice versa, miradi ya maendeleo tui-finance wenyewe, kwa sababu hiyo ndio msingi wa maendeleo.

  Hata hivyo mpaka sasa bado naona uchumi wetu na nchi yetu ni highly mismanaged, viongozi wangekuwa na nia ya kweli withi two three years tungeweza kufikia level ya kujitegemea. Ufisadi na ubinafsi unatula sana, hiyo ndio cancer iliyopo kwenye serikali na chama kinachotutawala.
   
 16. N

  Nyerererist JF-Expert Member

  #16
  May 3, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 443
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hata mie nakuunga mkono kwa mtazamo wako,,ni vyema tukajitegemea upande wa bajeti ya maendeleo na sio kutegemea wafadhiri...hiyo ni aibu,,nchi nyingi zimeshatoka hapa tulipo
   
 17. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2008
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Shukrani Kithuku, hili changa KUBWA kuliko hata yale ya Mkapa na Mramba; jamaa wana AKILI sana!

  Mchezo unaochezwa hapa ni kwamba kwa kuwa wameshaona skendo za kifisadi zimeshitukiwa na mabwana zao (wafadhiri), na kwa kuwa hakuna uhakika wa pesa wanazohitaji zikiwemo za posho za vikao hewa plus "maendeleo", sasa wanaanza kutudanganya kwamba "maendeleo" wanawaachia mabwana zao ili kesho tukilalamika waseme Mabwana hawajachangia huku wao wakiendelea kulipana posho hewa. TUFUNGUKE MACHO NA HIZI STATEMENT ZITATUUMIZA!!
   
 18. Bin Maryam

  Bin Maryam JF-Expert Member

  #18
  May 3, 2008
  Joined: Oct 22, 2007
  Messages: 685
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Maneno ya Mkullo kwa kuanzia sio mabaya. Lakini je hii ni mara ya kwanza kwa viongozi kutoa ahadi kama hiyo?

  Na kilichotakiwa ni kwa wahusika kuchukua matamko ya waziri na mwakani wamuulize amefikia wapi? Tatizo linalokuja ni kwa wahusika kuuliza na kujibu maswali hayohayo kwa kutumia lugha nyingine.
   
 19. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hilo swali perspicacious! Babu kubwa mtu wangu.

  Yani hata hayaja wezekana bado: "That goal could be achieved through maximising tax collection, especially effective taxation of natural resources such as forest products and tourism."

  Kama SteveD alivyo mkamata na ki usanii cha "should at least guarantee" hapa anasema 'could be achieved.'

  Trying to hoodwink everybody. Adanganye wabunge wa Sisiem huko. Mkullo tafadhali!

   
 20. Insurgent

  Insurgent JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2008
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 469
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tukitaka kujua tunakwenda wapi inabidi tuangalie tunatoka wapi, la sivyo tutaishia kucheza mduara...

  Budget ya 2005-2006

  Recurrent expenditure 2791 billions
  Development expenditure 1385 billions
  Total 4176 billions (approximately 4.2 trillions)

  The budget was funded as follows:

  Domestic revenue(taxes) 2067 billions
  Grants and Loans 1725 billions
  Govt Reserves 256 billions
  Sale of PE shares 10 billions
  Non bank borrowing 115 billions

  Budget ya 2007-2008

  Recurrent expenditure 3866 billions
  Development 2201 billions
  Total 6067 billions (approximately 6.1 trillions)

  The budget was funded as follows:

  Domestic revenues(taxes) 3502 billions
  Grants and Loans 2549 billions
  Privatization Proceeds 15 billions


  Ukiangalia haraka haraka utaona kama mpango wake ni kuongeza taxes on tourism and mining ni kwamba anajaribu kucover difference ya 3866 - 3502 billions = 364 billions (Refer to 2007-2008 budget Recurrent expenditure). Kwa maneno mengine hakuna kipya zaidi ya kuongeza taxes!

  Development which needs 2.2 trillions to maintain current growth anaachia kudra za Donors. So kitakachopatikana ndio tutakitumia kuendelea, wasipotupa tutasurvive pale pale bila miradi yeyote ya maendeleo (stagnant).
   
Loading...