Bajeti ya Dawa ifutwe ni kiini macho na Upigaji wa Wazi

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,854
35,860
Nimefika katika hospitali mbali mbali ndani ya msimu huu wa mafua ya kawaida na sikukuu za mwisho wa mwaka.

Katika hospitali zote nilizokwenda kama mgonjwa au kupeleka wagonjwa nimethibitisha tashwishi yangu kuhusiana na bajeti ya dawa.

Hakuna wagonjwa wanaopata huduma ya dawa. Dawa zote wagonjwa wananunua wenyewe baada ya kuonana na daktari.

Hii ikiwa ni pamoja na malipo kwa ajili ya kumwona daktari na kulipia pia vipimo vyovyote vitakavyo hitajika.

Kwa mpango huu pesa tunazoambiwa zinanunua dawa kwenye hospitali za umma zinaishia wapi?

Si bora bajeti hii ikaelekezwa hata kwenye ajira mpya kuliko kuishia kusikojulikana?
 
Kwani Serikali inaposema inanunua ndege hizo ndege ni kwa ajili ya Wananchi kupanda tu bila kulipia?

Kila mwaka budget ya dawa hupitishwa. Kila dawa huuzwa kwa wagonjwa na usipoangalia hospitali hata muhimbili bill ya dawa utabambikizwa.

Pesa ya dawa hutolewa kwa mujibu wa budget bado kila dawa inalipiwa tena na wagonjwa.

Huoni kuwa dawa hizi zinanunuliwa mara 2 ndugu?

Bado mfano wako wa ndege huuoni unapo sambaratikia?
 
Samia alishasema tunapenda vya bure, inawezekana kweli hiyo bajeti ya dawa iko siku itafutwa.
 
Kila mwaka budget ya dawa hupitishwa. Kila dawa huuzwa kwa wagonjwa na usipoangalia hospitali hata muhimbili bill ya dawa utabambikizwa.

Pesa ya dawa hutolewa kwa mujibu wa budget bado kila dawa inalipiwa tena na wagonjwa.

Huoni kuwa dawa hizi zinanunuliwa mara 2 ndugu?

Bado mfano wako wa ndege huuoni unapo sambaratikia?
Muhimbili wanauza dawa maana na wao wananunua MSD..na MSD mapato yanaenda serikalini.

Wapi dawa zinauzwa mara mbili hapo?
 
Kama wagonjwa wanalipa dawa hospitalini 100% na faida juu, bajeti ya dawa ni ya nini ndugu?

Fungua macho. Fyongo kama hiyo Iko wizara ya elimu pia:

Serikali haipo kwa maslahi yetu bali kufanikisha upigaji wao

Tungali na safari ndefu.
Muda mwingine ni kutafiti kwanza kabla ya kuweka mada, sera ya Tanzania ni kuchangia matibabu hivyo basi serikali inachangia na mwananchi anachangia, bei za matibabu kwenye hospitali za serikali sio gharama halisi bali zinaruzuku ndani yake. Kwahiyo usione unanunua dawa mia moja ukasema hiyo ndo thamani yake ni kama tulivyokuwa tu nalipa ada shs 20,000 sekondari enzi hizo haikuwa gharama halisi ya elimu
 
Enzi hizo siyo? Leo malipo ni 100% + interest.
 
Back
Top Bottom