Bahati Bukuku amuimbia Lowassa wimbo

Bahati Bukuku amuimbia Lowassa wimbo

Mimi namalizia mchoro wa picha ya Lowassa akiwa anaaapishwa (just an imagination) nakuhakikishia ntapiga milioni 15 kwny hii.

Mwaka wa kuvuna mapesa huu wakuu
"Kula CCM, Kura UKAWA!"
Unawaza nje ya box
Kila la kheri kwa ubunifu huo!
 
Huo wimbo unaitwaje Mkuu nami ni ckilize ili nitoe maoni yang
 
Dunia uwanja wa vita ... ulaji na urefu wa kamba yke ... tonge mdomon kwan umeladhimishwa kumpenda achana na project za watu ... kwan muimbaji kosa lake lipi ...
Kla mtu JF mwana siasa 😎😎😎😎
 
Nimeona bora nichangie tena baada ya kuna bandiko tata la anayejiita Rev Moses J ambalo limetuita na Mimi mmojawapo wajinga tulioona Kuwa mtumishi wa Mungu Bahati Bukuku amekosea kuimba nyimbp ya kumpigia kampeni my Lowassa na kumpa sifa za wateule wa Mungu mfalme Suleiman na baba yake mfalme Daudi.

Kwanza lugha ya ukakasi na kuwashambulia we ye maono tofauti na yeye inanipa taabu kuamini Rev Moses ni mchungaji wa kondoo wa Bwana. Au ni mmoja wa wale wachungaji walioenda nyumbani kwa Lowassa kufanya maigizo ya kumuomba agombee Raisi?

Pili kimtokacho mtu mdomoni ndicho kilicho moyoni mwake,nanukuu moja ya kauli zake"...kinachotusumbua kwanza ni wale walio na pipi midomoni za wagombea wanaohaha why Lowassa?"

Reading between the lines inaonyesha kwa neno kinachotusumbua,ina maana yeye na wenzake ambao bila ya mashaka ni team Lowassa! Kwa hi ana pipi mdomoni kutoka kwa Lowassa kwa akili ndogo asiyemkubali basi anatoka kwa wapinzani wake.WRONG!!!!

Mimi sikubaliani na Lowassa wala kitendo cha Bahati,ni maoni yangu na wala sishabikii kiongozi yeyote wa CCM,Kwa hiyo ni mjinga kwa maneno ya Rev Moses? Tumeshudia wachungaji wa calibre ya Rev Moses wakiandamana kwenda kwa mh Lowassa kupewa pipi anayoimung'unya had I kutuita tunaopinga wajinga na kututisha tusichangie kwa uhuru,soma"hili siyo bunge ni kunakolindwa hat a kauli zisizofaa,kauli za kumdharirisha mtu, hakikisha una utetezi wake kisheria kabla hujazitoa" hii kauli inaweza kutolewa na MTU aliyelewa madaraka,asiyependa kukosolewa, ya vitisho visivyo maana,kutuita wajinga kwa kubisha kwako safi tu.

Nukuu zako Rum13:1-3,timotheo 2:1-2,mathayo 28:18,zote hizo zinazungumzia mamlaka,kwa maana nyingine tawala zilizo madarakani! Hivi Lowassa kwa tafsiri ya vifungi hivi anaongoza taifa gani hapa? Mh Jakaya Mrisho ni na ni basi? Kwa nini kutumia neno la Mungu kupotosha watu? Mnasomea wapi hii uchungaji wenu?

Au ndiyo tayari LOWASSA ni chaguo la Mungu kama tulivyoambiwa jk ni chaguo la Mungu pia?

Upotoshaji wa maneno ya Mungu unafanywa tu na wanaojiita wachungaji kwa kujua kuna watu wanaowaamini kuwa kweli ni watumishi wa Mungu wakati wengi ni zuga turn,nadhani watanzania basi hawajasahau wachungaji wa DECI jinsi walivyocheza na ani za watu na wakawaibia mabilioni ya hela,he ilikuwa ni kazi ya Mungu au ya Shetani,na walioenda kumshawishi Lowassa agombee wanafanya kazi ya Mung I au us shetani? Ukipata majibu haya utajua hata hii kazi ya Bukuku na Rev Moses ni ya Mungu au shetani.

HITIMISHO:
Bukuku ni maarufu kama watu engine maarufi akiwemo mh Lowassa,tofauti ni jinsi kila mmoja alivyopata umaarufu wake,wengine sasa,wizi na ufisadi,engine utajiri,michezo,kuimba nyimbo za kidunia na za kumsifu Mungu.

Bukuku amepata umaarufu wake kwa kumtumikia Mungu kwa njia ya kueneza injili kwa kuimba na kumsifu Bwana,ni muimbaji kama Jaydee lakini Jaydee anaimba nyimbo za kidunia,akiimba kumtukuza na kumsifu yeyote hakuna atakayeshtuka.

Lowassa ni mwanasiasa ambaye anataka kugombea Raisi na si kiongozi kama unavyojaribu kupotosha maandiko

Dhambi unayotaka kufanya ni kutuaminisha Kuwa Bukuku ni mtakatifu kiasi Mungu anamtumia kutuchagulia taiga hili kiongozi,tena Mungu watu Hutu ametuteulia Lowassa awe mpakwa mafuta wake kama ilivyokuwa kwa mfalme Daudi na baadae Suleiman,nenda katubu na baada ya hapo ushindwe kabisa Mungu watu ni mwema hana haja na watuhumiwa wa wizi na ufisadi.

Kufanya kazi ya Bwana so ile michezo yenu ya maigizo kwenda kumshawishi MTU we nu kwa kutaka kumuingiza na Mungu

Hata kwa nukuu zako za kupotosha,hata na title ya Rev bado utafanya kazi sana kutushawishi kwa mpakwa mafuta we nu Lowassa na Mtumishi mwenzako Bukuku,tuliwaamini wachungaji mkatuingiza kwenye DECI, Sasa mnakuja na DECI nyingine kabambee,hii mkituingiza tumeumia miaka mitano,tumeshtuka HATUDANGANYIKI,
 
we ulietoa vifungu vya biblia hapo juu muogope Mungu.
Katika mistar uliyotoa hapo Mungu anazungumza juu ya mamlaka, Lowasa ana mamlaka gani kwq watz, bukuku anasema Lowasa anatawala kwa amani, je anatawala wapi? nadhani Bukuku hajawa makini ktk hili, Lowasa ni mbunge ktk jimbo fulani hivyo yeye ni mwakilishi wa wananchi watz ktk jimbo hilo na sio mtawala!! Bukuku angekuwa sahihi sana kama angeimba uwakilishi wa Lowasa ktk jimbo lake na sio habari za utawala na mafuta. Aombee nchi nasio kutajataja watu, majina ya watu yanatusaidia nini?
 
Hivi wabongo tunaakili gani ! yani mtu anuutaka urais kwa udi na uvumba kwa kutumia mamilioni ya fedha na sisi tunakaa na kumshabikia.
kwa kweli hii itatucost sana kama huyu jamaa atapita.
kumbukeni Nyerere alivyotuletea uhuru wa nchi hii alifadhiliwa na wala hakumwaga fedha. Mwinyi nae aliibuliwa na Nyerere nae hakumwaga fedha. Mkapa aliibuliwa dakika za mwisho nae hakumwaga fedha kabla na JK halikadhalika, sasa inakuaje hatuyaelewi haya au tunataka tu ushabiki ili jamaa akiingia alipe visasi. Tuweni makini ndugu zangu tuache ushabiki usio na kichwa wala miguu, hotuba za Nyerere zanaelekezaa vizuri rais tumtakaye.
 
Ujinga na kujikomba na kutaka kumtumia Mungu vibaya!
Hawa waimbaji binafsi wa nyimbo za injili wote ni wajasiliamali tu wanaotumia dini kujipatia kipato. Waimbaji wa kweli wa nyimbo za injili ni zile kwaya zinazoimba kanisani wakati wa ibada kama sehemu ya mahubiri na kupamba ibada, kama kwaya kuu, kwaya ya uinjilisti, kwaya ya vijana, kwaya ya kina mama, kwaya ya watoto nk ambazo hata kama zitatengeneza kazi na kuziuza, mauzo yake huwa ni kwaajili ya kanisa sio binafsi kama walivyo hao akina Bukuku, Rose Muhando, Jenifa mgendi, Flora Mbasha na wengineo walio mmoja mmoja au kakandi nje ya kanisa.
 
Ndo mana manabii wa uhongo wanaishia kuwapa mimba na kuvunja ndoa zao.....Lowasa hana tofauti na yule aliyemuimba kwenye wimbo
wa mfalme wa Aman sasa anatuimbia nini hapa....Pengne kakosea kuandika badala ya ku Un-like yeye ka-like!!!Natabiri Bahati B-kajiua kimziki.

Nadhani Mungu hadhihakiwi kwa maono na tamaa binafsi na ilivyo biblia waweza itumia utakavyo na ikakusaport kwa kuchagua vifungu uvitakavyo... Neno huua na Neno huuisha... kwa hili kama ni kweli bahati hayuko sahihi.. subiri tuone mwishowe.
 
Du kweli pesa imevaa suruali injili ya kweli itabak kwenye jukwaa
 
hiz imani za kimapokeo zina shida kweli kweli, pili njaa ina mtesa sana huyo binti, tatu anataka kuwa first lady siku lowasa akiingia madarakani,,, bukuku anataka kumusafisha mwizi, jangili....
 
Huyu Mdada Bukuku namjua vizuri sana, kipindi anakaa kinondoni Mkwajuni , niliwahi kwenda nyumbani kwake alikuwa hapendi ndugu wala marafiki wa mme wake. aliwafukuza shemeji zake wote wote, akiwasingizia eti wanamtaka ,jamani !!! ,Baadaye wakahamia kijito nyama, karibu na shule ya Masijidi Ghuba. pale alikimbia familia yake kutokana na Choyo aliyokuwa nayo. " JE utamtambuaje Mtu aliyeokoka"? Mme wake aliwachukua Wadogo zake akaanza kuishi nao. Hana lolote huyu

Vp kuhusu mkorogo? nakumbuka kuna uz humu waliweka picha zake kipindi anatoka mbeya na alivyo sasa hiv sijui ndio hayo mafuta?
 
Sawa pamoja na kumjua vizri mno kwa vile labda alikuwa wifi/shemeji yako, sio haki kuweka mambo yake hadharani, yote ni Maisha.Kama wewe mi mkristo anadhani unajua kuwa Yesu hakuna duniani kuwaita wenye afya wakamwone daktari , bali wenye dhambi ili wapate kutubu.

Hivyo mimi kama shabiki mkubwa wa nyimbo zake kamwe siwezi kukwaruzika kwa tabia yake/mambo yake.Hayo ni yake binafsi.Kumbuka hapa duniani shetani anapambana na watu wa Mungu kwa kila njia.

Chakula kitamu kinachopikwa kwenye jiko chafu.!
 
Utumwa ,utumwa,utumwa.
Subirini moto tu,hasa viongozi wa dini ndio moto utawashukia kwa nguvu kwa sababu ya kuweka maslahi yao mbele kwa kisingizio cha jina la mungu.
 
Jamani mi mgeni naomba mnisaidie mi mgeni,mnamzungumzia lowasa yupi au ni yule ambae baada ya kusomewa mashtaka yake jinsi alivyo shiriki kwenye dili la richmond yeye aka amua kujiuzulu Alafu bosi wake akatia saini barua yake au ni lowasa yupi?
 
Back
Top Bottom