Bahati Bukuku amuimbia Lowassa wimbo

Bahati Bukuku amuimbia Lowassa wimbo

Jamani mi mgeni naomba mnisaidie mi mgeni,mnamzungumzia lowasa yupi au ni yule ambae baada ya kusomewa mashtaka yake jinsi alivyo shiriki kwenye dili la richmond yeye aka amua kujiuzulu Alafu bosi wake akatia saini barua yake au ni lowasa yupi?

Hapana, sio Huyo ni yule mwingine
 
Jamani mi mgeni ndugu zangu mnamzungumzia lowasa yupi au yule ambae baada Ya kusomewa mashtaka yake bungeni jinsi alivyo shiriki dili la richmond ye akakimbilia kuandika barua ya kujiuzulu ,alafu bosi wake akaitia saini barua yake ndo lowasa huyu mnae mzungumzia.
 
Nimeona bora nichangie tena baada ya kuna bandiko tata la anayejiita Rev Moses J ambalo limetuita na Mimi mmojawapo wajinga tulioona Kuwa mtumishi wa Mungu Bahati Bukuku amekosea kuimba nyimbp ya kumpigia kampeni my Lowassa na kumpa sifa za wateule wa Mungu mfalme Suleiman na baba yake mfalme Daudi.

Kwanza lugha ya ukakasi na kuwashambulia we ye maono tofauti na yeye inanipa taabu kuamini Rev Moses ni mchungaji wa kondoo wa Bwana. Au ni mmoja wa wale wachungaji walioenda nyumbani kwa Lowassa kufanya maigizo ya kumuomba agombee Raisi?

Pili kimtokacho mtu mdomoni ndicho kilicho moyoni mwake,nanukuu moja ya kauli zake"...kinachotusumbua kwanza ni wale walio na pipi midomoni za wagombea wanaohaha why Lowassa?"

Reading between the lines inaonyesha kwa neno kinachotusumbua,ina maana yeye na wenzake ambao bila ya mashaka ni team Lowassa! Kwa hi ana pipi mdomoni kutoka kwa Lowassa kwa akili ndogo asiyemkubali basi anatoka kwa wapinzani wake.WRONG!!!!

Mimi sikubaliani na Lowassa wala kitendo cha Bahati,ni maoni yangu na wala sishabikii kiongozi yeyote wa CCM,Kwa hiyo ni mjinga kwa maneno ya Rev Moses? Tumeshudia wachungaji wa calibre ya Rev Moses wakiandamana kwenda kwa mh Lowassa kupewa pipi anayoimung'unya had I kutuita tunaopinga wajinga na kututisha tusichangie kwa uhuru,soma"hili siyo bunge ni kunakolindwa hat a kauli zisizofaa,kauli za kumdharirisha mtu, hakikisha una utetezi wake kisheria kabla hujazitoa" hii kauli inaweza kutolewa na MTU aliyelewa madaraka,asiyependa kukosolewa, ya vitisho visivyo maana,kutuita wajinga kwa kubisha kwako safi tu.

Nukuu zako Rum13:1-3,timotheo 2:1-2,mathayo 28:18,zote hizo zinazungumzia mamlaka,kwa maana nyingine tawala zilizo madarakani! Hivi Lowassa kwa tafsiri ya vifungi hivi anaongoza taifa gani hapa? Mh Jakaya Mrisho ni na ni basi? Kwa nini kutumia neno la Mungu kupotosha watu? Mnasomea wapi hii uchungaji wenu?

Au ndiyo tayari LOWASSA ni chaguo la Mungu kama tulivyoambiwa jk ni chaguo la Mungu pia?

Upotoshaji wa maneno ya Mungu unafanywa tu na wanaojiita wachungaji kwa kujua kuna watu wanaowaamini kuwa kweli ni watumishi wa Mungu wakati wengi ni zuga turn,nadhani watanzania basi hawajasahau wachungaji wa DECI jinsi walivyocheza na ani za watu na wakawaibia mabilioni ya hela,he ilikuwa ni kazi ya Mungu au ya Shetani,na walioenda kumshawishi Lowassa agombee wanafanya kazi ya Mung I au us shetani? Ukipata majibu haya utajua hata hii kazi ya Bukuku na Rev Moses ni ya Mungu au shetani.

HITIMISHO:
Bukuku ni maarufu kama watu engine maarufi akiwemo mh Lowassa,tofauti ni jinsi kila mmoja alivyopata umaarufu wake,wengine sasa,wizi na ufisadi,engine utajiri,michezo,kuimba nyimbo za kidunia na za kumsifu Mungu.

Bukuku amepata umaarufu wake kwa kumtumikia Mungu kwa njia ya kueneza injili kwa kuimba na kumsifu Bwana,ni muimbaji kama Jaydee lakini Jaydee anaimba nyimbo za kidunia,akiimba kumtukuza na kumsifu yeyote hakuna atakayeshtuka.

Lowassa ni mwanasiasa ambaye anataka kugombea Raisi na si kiongozi kama unavyojaribu kupotosha maandiko

Dhambi unayotaka kufanya ni kutuaminisha Kuwa Bukuku ni mtakatifu kiasi Mungu anamtumia kutuchagulia taiga hili kiongozi,tena Mungu watu Hutu ametuteulia Lowassa awe mpakwa mafuta wake kama ilivyokuwa kwa mfalme Daudi na baadae Suleiman,nenda katubu na baada ya hapo ushindwe kabisa Mungu watu ni mwema hana haja na watuhumiwa wa wizi na ufisadi.

Kufanya kazi ya Bwana so ile michezo yenu ya maigizo kwenda kumshawishi MTU we nu kwa kutaka kumuingiza na Mungu

Hata kwa nukuu zako za kupotosha,hata na title ya Rev bado utafanya kazi sana kutushawishi kwa mpakwa mafuta we nu Lowassa na Mtumishi mwenzako Bukuku,tuliwaamini wachungaji mkatuingiza kwenye DECI, Sasa mnakuja na DECI nyingine kabambee,hii mkituingiza tumeumia miaka mitano,tumeshtuka HATUDANGANYIKI,
Kama ametenda dhambi kubwa sanaaa, uwe wa kwanza kumpiga panga
 
Hivi Tusipoona Kupitia Kwa Wajumbe Wa Mungu Wetu Tutaona Hekima Zaidi Kupitia Kwa Nani?.. Zibarikini Kazi Za Watumishi Wa Bwana Japo Wanadamu Kama Sisi Ndipo Tutapokea Mibaraka Iliyotukimbia Ktk Nchi Yetu, Pia Jilindeni Nafsi Zenu Na Choyo Kwa Maana Ni Laana Mjumbe Wa Mungu, Ama Mkuu Ktk Taifa Lako Kumnena Vibaya Mbele Ya Wacha Mungu.
 
Balaa la MALARIA kupanda kichwani si zito kama balaa la NJAA kupanda kichwani.

Namuunga mkono Lowasa kwa kuwa ninayo dhamira ya kumuondoa SHETANI na kumuweka BINAMU YAKE, lkn dada yetu ameenda mbali
 
Ametumia uhuru wake kikatiba, mbona hamuwaongelei wasanii waliokutana na kikwete jana mlimani city?
 
Mualiko na kumuimba lowasa akimfananisha na daudi na suileiman ni kufuru shetani yu ndani yake nikimaanisha kahongwa c cku nyingi akiongezwa dau na lowasa atamfananisha na mungu subirini.
 
Walio mtusi mama WA watu JANA leo wanamuunga mkono "UNAFIKI SI MZURI"
 
Back
Top Bottom