Hii inanikumbusha siku moja tunasafiri usiku na mtumbwi ziwani, tupo vijana wanne na mzee mmoja, tunaendalea kupiga makasia na stori za hapa na pale, basi tukawa tunayakaribia mawe mawili yanayotazamana, yule mzee akauliza hapa nani kitinda mimba kwa mamake, hakupatikana, akauliza tena nani kifungua mimba kwa babu yake!! Akapatikana jamaa mmoja, akamwambia aombe kwa mizimu kupita katikati yaa Yale mawe mawili, au kama hatutaki tuyazunguke, ambapo ni mwendo kama wa dakika kumi hivi kuyazunguka, na kukatisha ni hata dakika haiishi, basi kila mtu mle kwenye mtumbwi akacheka almanusuru adondoke, tukamwona huyu mzee anazeeka vibaya huyu, au Jana alikesha kwenye kilabu, tutayazungukaje mawe leo wakati sisi tunazaliwa hadi tunakua sasa ni vijana wa makamo tunasikia tu hapo kuna watu waliwahi potelea hapo lakini hakuna aliyethibitishahilo, tukajua hizo ni stori tu za wazee wetu, sisi mbona kila siku tunakatisha hapo, ingawa mda mwingine unaweza pita mchana ukakutana na upepo mwanan, sisi tunachulia yale mawe ndo yanasababisha ile hali, basi yule mzee kuona amepuuzwa akakaa kimya, ile tupo katikati ya mawe mawili mara tukaona tunapiga makasia lakini hatusogei, kila tukiongeza nguvu wapi tuko hapohapo tu, tukaanza kumsihi yule jamaa aombe radhi kwa mizimu, kumbe jamaa kifungua mimba kwa babu akiongea sauti haitoki, basi mvua ikaanza kunyesha, kumbuka hapo hatusogei na mvua inapiga balaa, baada kama ya Massa matatu kila mtu kachoka kupiga makasia na amekata tamaa, ameamua litalokuwa na liwe, hapo tuaomba tu kifo chema, kila mtu anasali kivyake, kumbuka sisi mvua imetupiga tumeloa chapachapa ajabu yule mzee hata tone LA maji mwilini hana, na unga tuliobeba wote umeloa, yule mzee akatuangaliaaa akacheka sana akaomba apewe kafia, akaigeuza juu chini akaichoma kwenye maji huku akitamka maneno fulani, nilibahitika kuambulia majina ya watu tu wachache ambao walikufa miaka hiyo na wengine nasikia walikuwaga watata, ghafla ukaja kama upepo hivi, kutahamaki zimebaki hatua chache kufika tulipokuwa tunaenda, tupo wakavu kabisa na unga wetu mkavu ajabu yule mzee aliyekuwa mkavu wakati sisi tunyanyeshewa ndio kaloa sasa, kumbuka umbali tokea kwenye jiwe hadi hapo tulipokuwa tunaenda ni Masaa mawili lakini ndani ya nusu saa tulikuwa tumeshafika, yule mzee akatuonya tusihadithie zile masahibu kwa watu hadi msimu wa mvua ujao utapoisha, kwani kwa kukiuka vile mvua zingekata msimu mzima, hivyo njaa kubwa ingetokea kwa uzembe wa watu watano.
Nikipata mda ntakuja kumalizia nini kilikuwa kinafanyika, kwanini yule aliyetakiwa kuomba kupita alipata ububu wa ghafla/muda mfupi, kwanini sisi tuliloa na yule mzee hakuloa, ila mwishoni kaja kuloa yeye wakati sisi tupo wakavu, kwanini tulitumia nusu SAA sehemu ya kusafiri Masaa mawili, na kwanini watu wakikumbwa na madhila pale walikuwa hawasimulii kwa wengine,.......
Yani sasa nikipita kwenye yale mawe nakatisha umbali wa mita mia sitaki hata kuyasogelea, nahisi kimvuamvua tena kinataka kipige.
Tazama hadi sasa nimekuwa nayasimulia haya kwa faida ya wanaoamini sayansi ya mzungu huku wakipuuza hii yakwetu