Kalamzuvendi
JF-Expert Member
- Sep 21, 2009
- 639
- 741
Asante Baba, salute kwako.Akajitupa chini na kulala tulikuwa tumejenga kama futi tatu ndipo kwa chini ya ngazi nikawaona wale waovu wanakuja nikamuamsha yule mtu mkubwa akajinyoosha na kusema aaah divai na usingizi vimenifanya nijisikie kijana tena aah kama taa inayopanda kabla haijazimika usiogope nitapigana vema.
Makumazahn nimeota ndoto mimi nawe tupo katika nyota na miguu yetu imeelekea dunia ila sikuweza kuuona uso wangu aah saa yetu imefika eeh mwindaji mzee na ije tumeishi si haba ila ningependa kuona vita vingine kama vile vya jana wanizike kwa desturi za kikwetu makumazahn wauelekeze uso wangu kuelekea nchi ya uzulu.
Kumbu kumbu zimetulia umewakumbuka Nylephta na mwenzie Sorais, acha tu. Nilikuwa nacho hiki kitabu akakichukua rafiki yangu hakukirudisha tena kwangu.
Na huu mpela mpela wa maisha nikatoka kidogo nje ya Nyumbani, sina hakika Kama bado anacho au nae keshagawa.
Kila nikija Tanzania huwa nazunguka kwenye maduka ya vitabu kukitafuta lakini sikuwahi kufanikiwa kukipata.
Nilikisoma mwishoni kabisa mwa miaka ya 80 au mwanzoni mwa 90,mkuu Kama upo Tanzania na una uwezekano wa kukipata hicho kitabu tafadhali mkuu, ntamtuma bro wangu aje, ntaweza kukinunua kwa bei nzuri kutoka kwako halafu wantumie nakopiga box huku.