Mkuu hivi unaamini kuna uchawi? Je,umewahi kufanya utafiti wa kina juu ya matukio na simulizi zote zinazohusu uchawi? Nami nakuthibitishia hakuna kitu kinaitwa uchawi,majini wala pepo isipokuwa mashetani(shetani na kundi lile la malaika walioasi).Kinachoitwa uchawi ni hofu tulizorithishana na masimulizi ya matukio yasiyokuwepo.
Kwa mfano,wiki hii nilikuwa maeneo ya Mbagala kwenye Mgahawa mmoja namngojea mgeni wangu.Kukawa na jamaa wanapiga stori eti kuna kitabu kimoja cha Kiislamu kinauzwa milioni 2!Na kitabu hicho kimejaa miujiza sana.Ukiwa nacho unaweza kusafiri juu ya Bahari na kufanya mambo sana ya kustaajabisha.Maneno yale nilishindwa kuyavumilia kuyasikiliza nikaona niingilie kati kwa kuuliza kwa upole maswali kadhaa:Je,hicho kitabu wamewahi kukiona na kinapatikana duka gani au Msikiti gani? Je, kama kitabu hicho kinaweza kuwapa watu uwezo wa pekee namna ile kwa nini wafanyabiashara ya usafirishaji abiria majini wasikinunue ili waweze kutumia "tekinolojia" yake kusafirishia watu? Maswali yangu mengi yalisambaratisha mjadala ule kwa maana yote yalikuwa mambo ya kutunga tu na uongo mkubwa.
Kwa hiyo hakuna uchawi wala majini!