Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

wewe tatizoi lako kubwa ni lowassa na sio chadema...
lakin labda unataka kujua wenye imani na chadema,sawa,ila kama wapo ?unafanye na kama hakuna unafanyaje?
na chadema wasinge fanya hayo unayo yaita makosa makubwa sana wewe ungepata wapi maneno ya kuandika leo hii..
tujifunze kuishi kwa muda halisi...
 
CHADEMA Walitaka Publicity,na Wameipata!na Hata Kusema Kuwa Watumishi wa Mungu Kuwaomba Watulie Bado ni Kick Nzuri!
Na Mpaka Oktoba Mosi CHADEMA Haita Kauka Vinywani Mwenu!
Hivi Usafi Kesho Unaendelea,ahahaha!
CHADEMA Wametanguliza,wao Wamepiga Kona Fasta!

Hivi ndio mnavyo danganywa Na "mkwepa kodi" JPM alisema hajaribiwi Na hamkujaribu.
October Tena RC Makonda anata mumjaribu sio usafi Ila kupanda miti.
 
CHADEMA kama chama cha siasa ni TAASISI siyo MTU. Watu watapita, TAASISI itabaki. Mleta mada acha RAMLI
 
Kama viongozi wa dini na wale wooote wenye nia njema na wanaoitakia mema ya dhati Tanzania waliona watu wa kuikomboa hii Nchi na machafuko ni CHADEMA, wakaongeanao na wakaelewana na Nchi ni tulivu kwanini tusiongeze kuwa na imani na watu wanaojali maisha ya Mtanzania?
 
Inashangaza kwamba bado Watanzania wenye uelewa kama wewe unapigia debe Siasa za Kishabiki badala ya Maendeleo. Hivi kama CHADEMA wangeandamana unadhani madhara yangetokea kwa Waandamanaji tu? je wananchi wanaowazunguka?

Kumbuka amani inapochafuka haingalii kwamba wewe uko chama gani bali inamwathiri kila mmoja wetu. Kumbuka hata hao CHADEMA pia ni WATANZANIA kama wewe na ukifuatilia kwa umakini unaweza ukakuta familia moja ina Wanachama wa CCM na wale wa CHADEMA kwahiyo usidhani kwamba ukosefu wa amani uko kwa wapinzani tu.

Bila shaka nia yako ilikuwa ni kuona leo watu wamepigwa risasi au kupigwa virungu na kujeruhiwa vibaya ama kufa. Huo ni uchochezi mbaya sana.

CHADEMA kama Chama kingine chochote cha SIASA wana haki ya kufanya maandamano ilimradi tu hawavunji Sheria na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa unaposhabikia mabavu ya uonevu yanayofanywa na Serikali iliyoko madarakani usidhani kwamba ni sifa au inakusaidia chochote zaidi ya kuwa mwenye mawazo mgando.

Tukumbuke kuwa Nchi hii ilikubali kuanzishwa SIASA ya vyama vingi yenyewe mwaka 1992. Nakumbuka kipindi kile nikiwa mdogo ilipigwa kura ya maoni kama je Watanzania wanataka Siasa ya vyama vingi na 80% walitaka tubaki kwenye Siasa ya Chama Kimoja. Sasa Serikali yenyewe ama kwa shinikizo la IMF (Kupewa misaada) waliamua kuingia kwenye Siasa ya vyama vingi. Sasa kama tumekubali wenyewe kuingia kwenye Siasa hiyo, je ni kwanini tunawakandamiza wale raia walioamua kuwa vyama vya upinzani?

Nakumbuka Rais aliyepita Mhe. JK pamoja na mapungufu yake kama binadamu yeyote lakini aliweza kuongoza kwa kufuata Utawala wa Sheria/Katiba na aliweza kupambana na hawa wapinzani kwa kutumia hoja na si vitisho na kuwakandamiza. Kwa kutumia njia hii hii aliweza kuweka mkakati wa kutembea Nchi nzima (Kinana pamoja na Mhe. Nape) ili kukiimarisha Chama. Hii ndio njia inayopaswa kuigwa na Rais aliyeko madarakan.

Kutumia ubabe na mambo mengine ambayo sio ya msingi yanaturudisha nyuma kwa enzi za Chama kimoja ambazo kamwe hazitaweza kufanikiwa maana hizi ni dhama nyingine na karne tofauti kabisa. Pia namshauri Mheshimiwa Rais asitumia nguvu nyingi sana kuwabana wapinzani kwani wanampotezea sana muda wa kufanya shughuli za maendeleo na kutekeleza ilani ya CCM.

Mkuu umenena vyema sana tu.Mambo yote ya msingi umeyaweka hadharani.Vitu viwili ambavyo hujavigusia ni matusi Na kejeli dhidi ya JPM kutoka upinzani.Wewe ukiwa mwana JF unasoma wapinzani wanafanya ubabe wa kumtusi Raisi Na serekali anayo iongoza. Je Kama Wewe ndio Raisi uta taka kukutana Na hao upinzani?Kitu cha Pili JK aliwapa uhuru wanao utaka Matokeo yalikuwa ni kumtusi Na kumuita dhaifu..
Namuunga mkono JPM asije kuitwa dhaifu tena
Kama alivyo sema"HAJARIBIWI "
 
Naamini kuna kitu kimekujaa kifuani. Na hicho kitakuua. Kama kuna maisha yanakutesa, omba msaada wa kisaikolojia. Tafuta mfumo wa maisha utakaokupa unafuu wa hisia zako. Lakini kama unaishi kwa kazi hiyo nakupongeza, ila jitahidi kusoma salama za nyakati, utakuja kujilaumu sana.
 
NYANI
Politics is dynamic not static
Mambo yanaenda kutokana na hali halisi na mjuvi huzunguruka navyo
Sidhani hata uta nielewa
 
Una masikio lakini hayasikii na una macho lakini hayaoni. Kwanini usiiamini CDM wakati ndiyo inayokupangia ufanye nini. Kwasasa ndiyo inayopanga tarehe gani (lini) iwe siku ya kufanya usafi au kupanda miti.
 
Mimi familia na marafiki zangu, bado tunai support chadema na ukawa kwa ujumla
 
Mlisema chama kinachopenda vurugu, imekuwaje tena mnataka kifanye vurugu, vijana wa lumumba, buku 7 imekata nn?
 
Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
Hawakuwa na dola lakini walipata kura milioni 6 na wenye dola waliambulia kura milioni 8.Hata wenyewe ni maji marefu tu.
 
Kwani hata kabla ya maandamano kuna MTU alikuwa na imani na CDM? CDM ilishafariki siku Dr Slaa alipofanyiwa uhuni! Haitafufuka tena period!!
 
Hizi kauli nazisikia mwaka wa 6 huu.Eti chadema itakufa,wamekufa wao kisiasa and Chadema is getting stronger everyday.So tumewazoea vidampa wa lumumba.
 
Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
Wewe acha maneno mengi, njoo ofisini nikuongezee buku 3 kwenye hiyo ya Lumumba uwe na msimbazi
 
Back
Top Bottom