Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

Bado wapo wenye imani na CHADEMA?

... si kweli. alikuwa bepari hadi 1967 akageuka akawa mjamaa; alimuunga mkono maasi ya Ojukwu wa Nigeria baadaye akawa kigeugeu, aliua jumuiya ya EA na kuanzisha SADC na COMESA, n.k.
Huo ni ukigeugeu?
 
Kuiamini CHADEMA ni sawa na kuamini iko siku Lowassa atakuwa Rais jambo ambalo haliwezekani. Mbowe haaminiki hata kidogo.
 
Hawa CHADEMA ndo basi tena.

Naona wapo kwenye mwendokasi wa kuelekea kaburini.

Hii si mara yao ya kwanza kuwapandisha watu mzuka halafu wanaishia kubadili gia angani na kuwaacha watu wakining'inia.

Nani tena atawaamini hawa jamaa? Manake baada ya kuwaaminisha watu kwa miaka mingi kuwa Lowassa ni fisadi, matokeo yake ndo akaja kuwa mgombea wao. Mamlaka ya kimaadili ya kukemea ufisadi wakayapoteza.

Baada ya kuwapandisha watu mzuka wa UKUTA, leo wameufyata mbele ya Ngosha.

Sasa eti wametangaza hayo maandamano yatafanyika Oktoba mosi.

Watampata nani hiyo Oktoba mosi? Wake, waume, na watoto wao?

Wameishiwa kabisa. Hawana jipya tena. Hawana dira wala mwelekeo wowote ule.

Mtu afadhali unaweza kusema kuwa kabla ya ujio wa Lowassa kwamba watu walijua wanasimamia nini na wanasimama wapi.

Lakini leo hii nani anayejua wanachokisimamia? Nani anajua wanaposimama?

Walishindwa hata kuwashawishi wapinzani wenzao kuwaunga mkono ki hali na ki mali kwenye huo UKUTA wao. Wengine wakadiriki hadi kuwatakia kila la kheri na kuwaahidi kuchangia damu endapo wangehitaji baada ya kupokea kichapo cha vijana wa Ngosha.

Matokeo yake tingatinga limepita na kuusambaratishia mbali.

Wanahitaji uongozi mpya wenye maono mapya la sivyo wataenda bye bye for good.
no wonder DT is going to be president in that country. weird bunch of people!

I would have played it a bit smarter if I were you.....I would go online polling. what about that for litmus, huh?
 
no wonder DT is going to be president in that country. weird bunch of people!

I would be smarter if I were you.....I would go online polling (litmus, isn't it?).

Donald Trump hawezi kuwa rais wa USA wewe.

Kama vipi tuweke dau hapa....dola 1,000.

Are you game?
 
Mambo ya Obama ya nini hapa?

Tunaweka dau, hatuweki?
hamna cha dau hapa.

ili mshike adabu and you guys come back down to earth, I pray that DT ashinde (oh yeah, atashinda).

oh boy, the dude will kick a.s.s freaking big time!!
 
hamna cha dau hapa.

ili mshike adabu and you guys come back down to earth, I pray that DT ashinde (oh yeah, atashinda).

oh boy, the dude will kick a.s.s freaking big time!!

We waombee Magu na mwenzie Ali Kiba.

Trump hawi rais wa Marekani.
 
alipokelewa Lowassa baada ya tuhuma na matusi nchi nzima kwa miaka kadhaa na ghafla akatangazwa 'mtakatifu'!
sio kitu kigumu kupata waamini kwenye mazingira kama haya...unahitaji mashabiki tu ambao wako tayari kuamini lolote utakalowaambia na kuwashawishi,hata kama ni kukana majina,jinsia na kabila zao,watu ambao 'wanakula chochote toka mdomoni mwa bwana zao,watu ambao kwasababu zao binafsi hawataki kujaribu kupambanua mambo na kwa makusudi wanafumbia macho udhaifu wa imani zao ili tu kutii kiu yao ya kuwa wao 'hawawez kukosea'!
watakuwepo wenye kuwaamini naamini...ila mimi niliacha kuwaamini na kuwapa heshima siku waliyompokea Edo chamani..
 
Mie nampenda Nyani Ngabu kwa kuwa anasema ya ukweli na ya kutoka moyoni, sasa nyie mnaomshambulia sijui mna maana gani! Haendeshwi kwa kufuata mkumbo. Akisema CCM imekosea anakuwa ana hoja na hali kadhalika kwa vyama vingine. Hongera sana mtoto wa Marekani. Nitafutie na mie kanafasi huko japo nije hata kuwaosha wagonjwa wa akili na wazee nipumzike na hii minyoo na taifodi za hapa nyumbani kwetu
 
Mie nampenda Nyani Ngabu kwa kuwa anasema ya ukweli na ya kutoka moyoni, sasa nyie mnaomshambulia sijui mna maana gani! Haendeshwi kwa kufuata mkumbo. Akisema CCM imekosea anakuwa ana hoja na hali kadhalika kwa vyama vingine. Hongera sana mtoto wa Marekani. Nitafutie na mie kanafasi huko japo nije hata kuwaosha wagonjwa wa akili na wazee nipumzike na hii minyoo na taifodi za hapa nyumbani kwetu
Wee ni mtu poa sana. Ukija utafikia kwenye hii crib yangu iliyopo kwenye leafy suburb

1472707561916.jpg
 
"Chadema kwisha malegea" ukweli mchungu na siku zote ndivyo ulivyo. sisi wengine tuliwaelezaga wakati wanamtukana Dr. Slaa. CHADEMA bila Dr. Slaa haipo na itakufilia mbali wakatuona tumenunuliwa. Dhambi ya kumtukana Dr. Slaa itawatafuna daima.
 
Niliwahi kuweka thread iliyowashauri CHADEMA wabadilishe uongozi wa juu kabisa licha ya kuweza kuongeza idadi ya wabunge. Walipata wabunge wengi kwa sababu Lowassa has a very powerful personality and not because Mbowe is a capable leader, that is all.
CHADEMA needs new blood at the very top, otherwise siwaoni wakiongeza idadi ya wabunge, come 2020.
 
Naaminika Sana. Sijawahi kubadili gia angani Kama Mbowe. Jana kabadili gia ardhini. Poleni Sana.
Vitu vingine vinahitaji uelewa mpana sana ili kuvielewa. Wewe ni wa kulishwa maneno hivyo itakuchukua mda mrefu sana kuvielewa.
 
Kijana kukaa ukishabikia CDM ni kupoteza mda wako bure.
Japo tunaona serikali imekuwa ikivunja katiba hadharani lakini bado dioni haja ya kushabikia CDM, bora kukaa bila kusapoti upande wowote, kama wameshindwa kwenda kumtoa kiongozi mwenzao Salum Mwalimu hadi leo anasota lupango wakati viongozi kina mbowe ndio waliompa hio kazi na walaaniwe viongozi wote wa CDM.
Tazama leo tena wameufyata na UKUTA wao, kazi kupiga kelele tu wachumia tumbo wakubwa.
Chama kikubwa cha siasa huwa hakina usaliti. Ukiona chama cha siasa kinazo tabia za kuzungukana na kusalitiana, basi hata kama kina umri wa miaka 100 bado ni kichanga sana kuweza kupewa dhamana ya kuongoza nchi.
 
Back
Top Bottom