Shujaa Mwendazake
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 3,751
- 6,342
Wakati Tundu Lissu kabla hajashambuliwa kwa risasi alikuwa analalamika kuwa kuna gari inamfuatilia. Sisi ambao siyo wanaintelijensia tulikaaa kimya kusubiri majibu ya wataalam na viongozi. Na haya yalinenwa na wakuu wetu:
- Waziri wa mambo ya ndani, wakati huo Mwigulu Nchemba, alisema kwamba gari yenye namba ambazo Tundu Lissu alidai inamfuatilia ilionekana Arusha. Akadai pia wamewahoji wahusika na wamejiridhisha kwamba gari hiyo haikuwahi kufika D'Salaam.
- Naye IGP Sirro alidai Lissu hakuwahi kutoa taarifa kituo cha polisi kuhusu kufuatiliwa. Vilevile IGP anadai polisi hawakuwa na taarifa zozote kuhusu Lissu kufuatiliwa na " watu wasiojulikana. "
Sasa tunachojiuliza ni kuwa hawa wote walikuwa wizara moja, Je ni kuwa hakuna mawasiliano kati ya waziri na IGP , Je hao maafisa waliokwenda kufuatilia huko Arusha na kuwahoji wahusika na kujiridhisha kuwa hawajawahi kuwa Dsm walitoka kikosi gani au cha wizara gani kana kwamba IGP asifahamu?. Au Mh Waziri ana kikosi chake pia ambacho IGP hakifahamu?. Nachelea kuhoji hapa ni nani alitupotosha? Mtaalamu wa Intelijensia na Mambo ya kiusalama, Kamanda Sirro au Mwanasiasa na mwanauchumi Mh. Mwigulu Nchemba.