Bado tunajiuliza nani alitudanganya kati ya Kamanda Sirro na Mwigulu Nchemba?

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Wakati Tundu Lissu kabla hajashambuliwa kwa risasi alikuwa analalamika kuwa kuna gari inamfuatilia. Sisi ambao siyo wanaintelijensia tulikaaa kimya kusubiri majibu ya wataalam na viongozi. Na haya yalinenwa na wakuu wetu:
  1. Waziri wa mambo ya ndani, wakati huo Mwigulu Nchemba, alisema kwamba gari yenye namba ambazo Tundu Lissu alidai inamfuatilia ilionekana Arusha. Akadai pia wamewahoji wahusika na wamejiridhisha kwamba gari hiyo haikuwahi kufika D'Salaam.
  2. Naye IGP Sirro alidai Lissu hakuwahi kutoa taarifa kituo cha polisi kuhusu kufuatiliwa. Vilevile IGP anadai polisi hawakuwa na taarifa zozote kuhusu Lissu kufuatiliwa na " watu wasiojulikana. "

    Sasa tunachojiuliza ni kuwa hawa wote walikuwa wizara moja, Je ni kuwa hakuna mawasiliano kati ya waziri na IGP , Je hao maafisa waliokwenda kufuatilia huko Arusha na kuwahoji wahusika na kujiridhisha kuwa hawajawahi kuwa Dsm walitoka kikosi gani au cha wizara gani kana kwamba IGP asifahamu?. Au Mh Waziri ana kikosi chake pia ambacho IGP hakifahamu?. Nachelea kuhoji hapa ni nani alitupotosha? Mtaalamu wa Intelijensia na Mambo ya kiusalama, Kamanda Sirro au Mwanasiasa na mwanauchumi Mh. Mwigulu Nchemba.​
Haya majibu yanafikirisha to the extent kuwa kwanini kusingekuwa na tume huru kuchunguza hilo tukio?
 
..Ninavyokumbuka pia Lissu alikamatwa na polisi kutokana na kauli za " kichochezi " alizozitoa ktk press conference aliyodai kuna gari ya " watu wasiojulikana " inamfuatilia.

..Vilevile msemaji wa serikali aliitisha press conference na kukanusha madai ya Tundu Lissu. Madai hayo yalihusu uhusika wa Jpm ktk suala la madai ya mkandarasi aliyeishitaki serikali.
 
Sasa tunachojiuliza ni kuwa hawa wote walikuwa wizara moja, Je ni kuwa hakuna mawasiliano kati ya waziri na IGP , Je hao maafisa waliokwenda kufuatilia huko Arusha na kuwahoji wahusika na kujiridhisha kuwa hawajawahi kuwa Dsm walitoka kikosi gani au cha wizara gani kana kwamba IGP asifahamu?. Au Mh Waziri ana kikosi chake pia ambacho IGP hakifahamu?.
waswahili wanasema ukiwa muongo usiwe msahaulifu
 
Wakati Tundu Lissu kabla hajashambuliwa kwa risasi alikuwa analalamika kuwa kuna gari inamfuatilia. Sisi ambao siyo wanaintelijensia tulikaaa kimya kusubiri majibu ya wataalam na viongozi. Na haya yalinenwa na wakuu wetu:
  1. Waziri wa mambo ya ndani, wakati huo Mwigulu Nchemba, alisema kwamba gari yenye namba ambazo Tundu Lissu alidai inamfuatilia ilionekana Arusha. Akadai pia wamewahoji wahusika na wamejiridhisha kwamba gari hiyo haikuwahi kufika D'Salaam.
  2. Naye IGP Sirro alidai Lissu hakuwahi kutoa taarifa kituo cha polisi kuhusu kufuatiliwa. Vilevile IGP anadai polisi hawakuwa na taarifa zozote kuhusu Lissu kufuatiliwa na " watu wasiojulikana. "

    Sasa tunachojiuliza ni kuwa hawa wote walikuwa wizara moja, Je ni kuwa hakuna mawasiliano kati ya waziri na IGP , Je hao maafisa waliokwenda kufuatilia huko Arusha na kuwahoji wahusika na kujiridhisha kuwa hawajawahi kuwa Dsm walitoka kikosi gani au cha wizara gani kana kwamba IGP asifahamu?. Au Mh Waziri ana kikosi chake pia ambacho IGP hakifahamu?. Nachelea kuhoji hapa ni nani alitupotosha? Mtaalamu wa Intelijensia na Mambo ya kiusalama, Kamanda Sirro au Mwanasiasa na mwanauchumi Mh. Mwigulu Nchemba.​
Haya majibu yanafikirisha to the extent kuwa kwanini kusingekuwa na tume huru kuchunguza hilo tukio?
Siro kaambulia aibu tena na uzee ule
 
Kufuatilia mambo ya wanasiasa ni heri ushike tu jembe ukalime...mwigulu ni mwanasiasa na lissu nae ni mwanasiasa .wote wana uongo ndani yake
 
Sasa tunachojiuliza ni kuwa hawa wote walikuwa wizara moja, Je ni kuwa hakuna mawasiliano kati ya waziri na IGP , Je hao maafisa waliokwenda kufuatilia huko Arusha na kuwahoji wahusika na kujiridhisha kuwa hawajawahi kuwa Dsm walitoka kikosi gani au cha wizara gani kana kwamba IGP asifahamu?. Au Mh Waziri ana kikosi chake pia ambacho IGP hakifahamu?.
waswahili wanasema ukiw amuongo usiwe msahaulifu
unatakiwa uwe consistent kwenye uoga wako
Wanasema Uongo ni mzigo mzito zaidi kuliko Ukweli
 
Back
Top Bottom