Bado najiuliza, uchaguzi tumefanya kwanini?

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,601
8,741
Inasikitisha sana kuona nchi yetu inapoenda kidemokrasia. Kama wewe ni Mtanzania unayependa nchi hii huwezi kufurahia hata kidogo kinachoendelea.

1. Kwanza jiulize kitu kimoja kunyang'anya Wapinzani nafasi walizoshinda kihalali au kuwazuia haki zao inasaidia vipi taifa letu? Kusaidia CCM sio kusaidia taifa!

2. Pili, je kuwa na wawakilishi sehemu nyingine ambao hawajachaguliwa na wananchi ni tatizo kwasababu watu bado wana mioyo yao na huwezi kubadilisha kwa kulazimisha.

3. Kwanini tunapoteza pesa, kuiabisha nchi, kuleta ugomvi mkubwa hivi kwa taifa badala ya kuungana na kuleta maendeleo?
 
Kumrahisishia jiwe na serikali yake kufanya maamuzi yanayowanufaisha wao binafsi. Miaka 60 baada ya uhuru tunaongozwa na chama kimoja na hamuoni kuwa hili ni tatizo.

Niligundua kuwa uhaba wa maji tiririka ni tatizo Tanzania wakati wa corona. Kila mahali kulikua na ndoo za maji kudhihirisha kuwa hakuna maji ya uhakika kwa watu kunawa mikono.
 
.Mimi najiuliza inakuwaje Wazanzibar wanapiga kura kumchagua Rais wa TANZANIA?
Screenshot_20201029-160159.jpg
 
"Kwisha"
"kwisha"
vitisho vya Armsatadam"kwisha"
mbwembwe za mikutano ya nyomi"kwisha"
vitisho vya The Haugue"kwisha"
kulala kwa Mwalimu Nyerere Butiama"kwisha"
Mzee Ponda na bagonza"kwisha"
mapicha mapicha ya mbwembwe"kwisha"
niyeyee tunajambo letu October"kwisha"
 
Kwani mlikuwa mnategemea nini?

Sisi wengine tumekuwa tukiwaambia kuwa hakuna haja ya kushiriki hiyo ‘charade’, lakini tunaishia kudhihakiwa tu.

Subirini 2025 mshiriki tena kuipa uhalali CCM.

Actually Mimi wala sijashangaa na wala sikuwa na mategemeo tofauti..
Ila nilifikiri watakuwa kama miaka mingine kuiba na kwingine kuacha .
This time wameiba kila jimbo
 
Hivi Kikwete kweli anajisikiaje kumwachia nchi huyu mtu mwovu asie haya kabisa!!

Na yeye udogo wake wa akili kutaka kumrithisha Membe ndio imetuletea janga, mkosi na aibu hii kimataifa! Hata kaheshima kadogo tulikokuwa nako kameisha kabisa!

Jiwe na makuwadi wenzie wanaweza jiona wameshinda lakini ukitafakari vizuri mwisho wa Ibilisi huyu utakuwa mbaya sana!
 
Kwani mlikuwa mnategemea nini?

Sisi wengine tumekuwa tukiwaambia kuwa hakuna haja ya kushiriki hiyo ‘charade’, lakini tunaishia kudhihakiwa tu.

Subirini 2025 mshiriki tena kuipa uhalali CCM.

Tazama watu waliojiandikisha halafu hawajapiga kura..ni zaidi ya nusu..
So msimamo wako ni almost ndo msimamo wa watanzania majority
 
Kama wewe ni Mtanzania unayependa nchi hii huwezi kufurahia hata kidogo kinachoendelea.
Yaan mpenda nchi achukie kuona wananchi wanachagua viongozi wao kwa demokrasia ya viwango vya juu kiasi hiki halafu asifurahie?
Ni mitazamo ya aina hii inawagharimu wapenzi wa jinsia moja...
 
Back
Top Bottom