Bado najiuliza, uchaguzi tumefanya kwanini?

Bado najiuliza, uchaguzi tumefanya kwanini?

Broad daylight robbery.
Halafu utasikia wanajiita wacha Mungu, wanyenyekevu... kumbe ni madhulumati na dhalimu kabisa.
 
Actually Mimi wala sijashangaa na wala sikuwa na mategemeo tofauti..
Ila nilifikiri watakuwa kama miaka mingine kuiba na kwingine kuacha .
This time wameiba kila jimbo
Yup!

Ndo hivyo.

Na 2025 mambo hayatokuwa tofauti sana.

Mimi siwezi kupoteza muda wangu na nishati yangu kupiga kura kwenye mazingira kama haya ya kwetu.

Ni uwendawazimu wa juu kabisa.
 
Tazama watu waliojiandikisha halafu hawajapiga kura..ni zaidi ya nusu..
So msimamo wako ni almost ndo msimamo wa watanzania majority
And guess what....

Kama vyama vikubwa vya kisiasa vingesusia, hiyo idadi ya wapiga kura ingeweza kushuka zaidi na kuifanya CCM ionekane ni kituko tu mbele ya jamii na hata jumuia ya kimataifa!

Sasa hivi hao wapinzani hawana uhalali wa kulalamika.
 
Inasikitisha sana kuona nchi yetu inapoenda kidemokrasia. Kama wewe ni Mtanzania unayependa nchi hii huwezi kufurahia hata kidogo kinachoendelea.

1. Kwanza jiulize kitu kimoja kunyanganya wapinzani nafasi walizoshinda kihalali au kuwazuia haki zao inasaidia vipi taifa letu? Kusaidia CCM sio kusaidia taifa!

2. Pili, je kuwa na waakilishi sehemu nyingine ambao hawajachaguliwa na wananchi ni tatizo kwasababu watu bado wana mioyo yao na huwezi kubadilisha kwa kulazimisha.

3. Kwanini tunapoteza pesa, kuiabisha nchi, kuleta ugomvi mkubwa hivi kwa taifa badala ya kuungana na kuleta maendeleo?
Kamundu, point no3. labda watawala wa CCM watakujibu punde si punde... waulize kwa herufi kubwa...
 
@Kamundu,kwa kukujibu swali lako. Tumefanya uchaguzi kwa sababu uongozi uliopo ulikuwa unamaliza muda wake na kwamba kulikuwa na wagombea wa vyama mbalimbali!
 
Nikiwaambia wapinzani wasusie chaguzi, hawataki. Hawanielewi.

Endeleeni tu kushiriki.

Wasiposhiriki mnawaambia wameogopa kukataliwa kwenye box la kura, mara ukisusa sisi twala!
...all in all wote hao waliopita hakuna hata mmoja atakayekwenda nyumbani kwa mwananchi wake na kumsongea ugali au kumchemshia chai!
 
I hate CCM, i hate Magufuli
Very sorry it doesn't help nor change anything many of patriotic Tanzanians love him and that's enough..

Congratulations in advance President Magufuli
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
"Kwisha"
"kwisha"
vitisho vya Armsatadam"kwisha"
mbwembwe za mikutano ya nyomi"kwisha"
vitisho vya The Haugue"kwisha"
kulala kwa Mwalimu Nyerere Butiama"kwisha"
Mzee Ponda na bagonza"kwisha"
mapicha mapicha ya mbwembwe"kwisha"
niyeyee tunajambo letu October"kwisha"
Hivi Ponda na Bagonza wapo kweli?? Naona kimyaaaaaaaaa wanasikilizia matokeo
 
Wasiposhiriki mnawaambia wameogopa kukataliwa kwenye box la kura, mara ukisusa sisi twala!
...all in all wote hao waliopita hakuna hata mmoja atakayekwenda nyumbani kwa mwananchi wake na kumsongea ugali au kumchemshia chai!
Nope!

Unasusa kwa sababu ya principle.
 
Ulikuwa uchaguzi wa kukamilisha ratiba kikatiba, kwamba baada ya miaka mitano muhula umekwisha tunachagua viongozi wa muhula unafuata. Sasa mnalalamika mlitaka kiongozi yupi wa upinzani achaguliwe? Kwani kuna sheria kuwa lazima kila bunge lazima upinzani wawepo? Mimi naona poa tu, wacha wapambane CCM tupu huu muhula tuone wapi wanatupeleka, upinzani nao wajitafakari kama kweli wanastahili kuwepo, badala ya kulalamika kuibiwa. Wajipange vizuri ili wawe na nguvu 2o25.

Nahisi Magufuli ataendelea tena kuwa Rais kwa miaka mingi, hawa watu watabadilisha katiba, wapo wenyewe tu.

Upinzani ule wa rasmi utakufa tu, hasa kama atazuia tena mikutano ya kisiasa kwa miaka mingine mitano. Ngoja tuone hii changamoto ya chama kimoja bungeni kama italeta tija. Mwenyewe anadai connection ndio itakuwa nzuri. Ngoja tuone.

Bila katiba mpya hali hii itakuwepo mpaka mwaka 3000 na sioni dalili ya kutokea katiba mpya, inawabeba wenye mamlaka.
 
Nikiwaambia wapinzani wasusie chaguzi, hawataki. Hawanielewi.

Endeleeni tu kushiriki.
Mkuu mbona ule uchaguzi mdogo wa serekali za mitaa walisusia upinzani. Na sisiem ikajinoma taratibu kwa furaha keki ya nchi.
 
Inasikitisha sana kuona nchi yetu inapoenda kidemokrasia. Kama wewe ni Mtanzania unayependa nchi hii huwezi kufurahia hata kidogo kinachoendelea.

1. Kwanza jiulize kitu kimoja kunyanganya wapinzani nafasi walizoshinda kihalali au kuwazuia haki zao inasaidia vipi taifa letu? Kusaidia CCM sio kusaidia taifa!

2. Pili, je kuwa na waakilishi sehemu nyingine ambao hawajachaguliwa na wananchi ni tatizo kwasababu watu bado wana mioyo yao na huwezi kubadilisha kwa kulazimisha.

3. Kwanini tunapoteza pesa, kuiabisha nchi, kuleta ugomvi mkubwa hivi kwa taifa badala ya kuungana na kuleta maendeleo?
Swali lako mkuu Kila mmoja anajiuliza, ila nafikiri uchaguzi huu umetusaidia kujua mengi,
 
Inasikitisha sana kuona nchi yetu inapoenda kidemokrasia. Kama wewe ni Mtanzania unayependa nchi hii huwezi kufurahia hata kidogo kinachoendelea.

1. Kwanza jiulize kitu kimoja kunyanganya wapinzani nafasi walizoshinda kihalali au kuwazuia haki zao inasaidia vipi taifa letu? Kusaidia CCM sio kusaidia taifa!

2. Pili, je kuwa na waakilishi sehemu nyingine ambao hawajachaguliwa na wananchi ni tatizo kwasababu watu bado wana mioyo yao na huwezi kubadilisha kwa kulazimisha.

3. Kwanini tunapoteza pesa, kuiabisha nchi, kuleta ugomvi mkubwa hivi kwa taifa badala ya kuungana na kuleta maendeleo?
Swali lako mkuu Kila mmoja anajiuliza, ila nafikili uchaguzi huu umetusaidia kujua mengi,
 
2025 msije sema wapinzani wametucheleweshea maendeleo kapigeni kazi wenye nchi.

Mmesikia ? sema
Ndiooooo hamna hapana mwaka huu
 
Sema hii ya wabunge wengi wa chama kimoja inaweza waweka katika wakati mgumu hapo baadae maana kuna baadhi wanaweza bweteka na ushindi wasifanye yale tarajiwa kwa wananchi, ngoja tuone.
 
Mkuu mbona ule uchaguzi mdogo wa serekali za mitaa walisusia upinzani. Na sisiem ikajinoma taratibu kwa furaha keki ya nchi.
Uchaguzi wa serikali za mitaa si sawa na uchaguzi mkuu.

Vyovyote vile, sijali tena kuhusu upinzani.

Ni wajinga na ni wapumbavu.

Wajipange tena kushiriki kuisindikiza CCM 2025.
 
Hivi ponda na bagonza wapo kweli?? Naona kimyaaaaaaaaa wanasikilizia matokeo
wapo ila wamezimika kama"mshumaa"
wamebaki"wanashangaa"
wameshakata"tamaa"
wanaulizana ni kipi"kilichotokea"
mpaka Sugu"amepotea"
Halima"amepotea"
Mbowe analia msumali"ameukalia"
Gwajima na Akson oi,oi"wanashangilia"
 
Back
Top Bottom