Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,155
- 137,168
Hayawi hayawi yanakuja kuwa.
Zimebaki siku tatu tu siku ya siku kuwadia.
Wachache wetu tuliwaambia kuwa mnajipa matumaini hewa tu.
JWTZ kamwe haliwezi kuipindua serikali ya CCM kwa sababu:
1. JWTZ ni majuha.
Hakuna lolote wanalolielewa kuhusu mambo yanayoendelea nchini. Hawajui chochote kuhusu ubovu wa katiba, utawala mbovu, n.k.
Mfano wa ujuha wa JWTZ: kuna siku nilimuuliza afisa mmoja wa hilo jeshi kuhusu aircraft carriers. Nikamwuliza Tanzania tunazo ngapi? Akasema ‘blaza’ hizo zipo kwenye maeneo yote ya mipakani mwa nchi 😂😂.
Nilimwuliza hilo swali kwa sababu alikuwa anazisifia sana silaha za jeshi. Alikuwa anadai JWTZ ina silaha hatari sana.
Mimi nikajaribu ku reason naye kwa kumwuliza kuhusu bajeti yetu ya ulinzi, kuhusu silaha zinazotengenezwa Tanzania kwa kutumia viwanda na wataalamu wa Kitanzania, na kadhalika.
Badala ya kunijibu maswali yangu, ambayo sidhani kama aliyaelewa, yeye akawa anazungumzia uhatari wa silaha walizonazo [ambazo ni za kizamani].
Dunia inakoelekea sasa hivi binadamu watakuwa hawaendi vitani tena. Yatakuwa maroboti huko kwenye medani za kivita. Madege yasiyo na rubani, nyambizi zisizo na wanamaji, ufyatuzi wa makombora yanayoweza kufika popote pale duniani na yakapiga shabaha kwa usahihi wa hali ya juu, na kadhalika.
Sasa unaweza kusema, ‘Ngabu, huyo ni mtu mmoja tu umeongea naye kuhusu hayo mambo yanayoendelea nchini kijeshi. Wote hawako hivyo’.
Ni kweli kabisa. Wote hawako hivyo. Huyo niliyeongea naye ndo mwenye nafuu. Hao wengine hata kuongea nao mambo ya maana haiwezekani.
2. Hao wachache waliobaki wenye ‘below average IQ’, wameshaonjeshwa asali ya ufisadi.
Hawawezi kufanya wala kusema chochote. Hawawezi wakaukata mkono unaowalisha.
Bila ya kuwa jeshini, hawana uwezo mwingine wowote ule ambao ungewapa fursa ya kushamiri.
3. Kwa kuzingatia hayo niliyoyasema kwenye 1 na 2, nadhani naweza kusema kwa uhakika mkubwa kabisa kuwa sisi hatuna jeshi la wananchi.
Lililopo ni jeshi la kulinda maslahi ya viongozi wa CCM na serikali yao.
Hivyo, kutegemea msaada kutoka kwenye jeshi la kulinda na kutetea maslahi ya CCM, ni kupotoka.
Huo ndo ukweli, hata kama ni mchungu kuukubali.
Btw, Kapteni Tesha kaja akapita tu kama upepo na akapotea mazima 😂.
Au bado mna matumaini kuwa atarudi?