Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Kuna dada alipishana na mke wa mwanaye mke wa mwanaye anaingia kujifungua naye anatoka haaa haaa alifunga na uzazi hapo hapo na alikuwa na watoto kama 10 hivi
Jamaaani, yani watoto wote hao alafu bado anajidhalilisha kwa waka mwana zake (in-laws)?
 
Sijambo zuri na linasikitisha sana, ila kuna baadhi mazingira yanapelekea swala hilo, mfano kuna watu wanabakwa wakiwa wadogo miaka 16 anajifungua, anaenda shule baada ya hapo anaolewa unategemea mtoto atakaye mzaa apishane na wabinti yake?, kwa nyongeza umesema mambo ya zamani hata hivo mtu wa1 999, umemeliza shule wewe kwasasa unaesabika kama wa zanani usasa unaanzia 2015...
Katika akina mama 200 wanaozaa sambamba na watoto wao, utakutana na kesi moja tu ya namna hii. Hao wengine 199 ni kukosa tu staha na maadili
 
ndio jamii zetu za kiafrika wengine tunazeeka mapema kwa kuwa huwa tunalazimika kupokea shikamoo za waliotuacha mbali kiumri yan jitu limekupita miaka kuanzia nane huko eti linakuamkia kisa baba yake mdogo au anko wake aaaaaah...... (tusichukulie kila kitu serious)
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
baba mdogo wa mwendokasi
 
NINA JAMAA YANGU BAADA YA BABA YAKE KUSUMBULIWA NA MARADHI NA VILE BABA YAKE ALIKUWA NA MTOTO MDOGO AKAAMUA KUCHUKUA MDOGO WAKE AKAE NAE.

CHANGAMOTO INAKUJA WATOTO WAKE WAKIMWITA JAMAA YANGU BABA NA MDOGO WAKE ANAMWITA BABA BADALA YA KAKA.
Wanamuita baba kwa sababu babu alikosea kuzaa uzeeni
 
Eti maadili wewe unajua maadili gani ?.Kuzaa ni kukosa maadili? Nchi inataka watu wewe unaongea upuuzi ? Mpaka binti anaolewa maana yake anakuwa anajua mama yake alifanya nini ndipo akazaliwa yeye sasa hapo ajabu kitu gani?. Usituletee tabia za huko kwenu ulaya. Afrika ambapo binti anazaa akiwa miaka14 anarudi shule anamaliza chuo kikuu anazaa wa pili halafu yule kwanza ameshapevuka na anaweza olewa na akazaa .Amka Afrika siyo Ulaya.Afrika unaweza kuwa na miaka 25 na bado unaye Baba Mdogo wa miaka 2.
Baba mdogo wa miaka miwili huyo ni mtoto wako wewe punguza ushamba
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Bado kuna watu wazima wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili.

View attachment 1667340

Siku ya sherehe ya mwaka mpya nilikutana na dada mmoja anaitwa Veronica (hili sio jina lake halisi) ambaye nilimaliza naye shule ya msingi mwaka 1999.

Huyu dada nilikwisha kutana naye mwezi kama wa August maeneo ya Banana Ukonga huku Dar. Kwa kuwa tulikuwa hatujaonana miaka takribani 15 tulipiga story nyingi sana za zamani.

Sasa nilipokutana naye tena Ijumaa ya tarehe 01 January 2020 huku Kivule ninapokaa (kwa maana aliniambia anakaa Kata moja na mimi) nilimuona anaongozana na binti mdogo wa miaka kama 9 hivi.

Tena huyo binti wamefanana kweli kweli. Basi tulipoonana tulisalimiana tena kwa furaha sana. Baada ya story kadhaa nikamuuliza, huyu ndio mtoto wako wa kwanza? Akakataa. Akasema hapana, huyu sio mtoto wangu.

View attachment 1667350

Huyu ni mdogo wangu wa mwisho. Mtoto wangu ameenda kwa baba yake kusalimia atarudi shule zikifunguliwa. Sema ndio rafiki yake mkubwa sana huyu (mdogo wake wa mwisho) kwa maana wamepishana mwaka mmoja tu.

Mimi sikuwa na jambo lingine la kumwambia zaidi tu ya kumpa hongera lakini nikawa ninajisemea tu kimoyomoyo "ina maana haya masuala ya mtoto na mama kuzaa kwa pamoja bado yanaendelea katika karne hii ya 21?"

Hii issue nilikuwa ninaiona tu kwa wazee wa zamani ambapo unakuta mtu unakutambulisha "huyu ndio baba yangu mdogo/shangazi yangu tumbo moja na baba" au "huyu ndio mama yangu mdogo tumbo moja na mama" lakini ukijaribu kuwatazama actually wanalingana umri au wamepishana mwaka mmoja tu.

View attachment 1667352

Mimi ni moja kati ya watu wanaokerwa sana na lugha za hawa dada/mama zetu manesi lakini linapokuja suala la kukemea wamama/wababa wanaoendeleza utamaduni huu wa hovyo mimi ninawaunga mkono sana.

Kuna mtoto wa shangazi yangu mmoja yeye ni nurse huko Geita anakwambia mama mtu mzima wa design hii akija kujifungua (wanawafahamu sana kwa maana vijijini watu ni wachache) huwa wanawachamba kwa maneno na lugha chafu mbele ya waume zao.

Kuna mama mmoja aliwahi kufariki mwaka 2006 alipokuwa anajifungua wakati bado tunakaa kule Keko. Sasa wakati wa mazishi watu wamekusanyika na wageni wanataka kujua chanzo cha kifo chake ikawa sasa ni aibu kusema kuwa amekufa kwa sababu ya "complications" za uzazi ilhali binti yake mkubwa ana mtoto wa miaka 2 tayari.

View attachment 1667341

Mimi binafsi ninaona sio jambo la hekima wala busara kwa mama/baba kuendelea kuzaa watoto wengine wadogo ilhali wale "first born" wamekwisha kuwa wababa/wamama wanaokaribia ku-reproduce.

Sio vizuri mama kuonekana ana tumbo kubwa la ujauzito pindi wale "first borns" wanapokuwa wamepevuka akili.

Kwa maoni yako, ni sahihi mama na binti/mtoto kuendelea kuzaa kwa pamoja? Mtoto wa mwisho kulingana na mjukuu wa kwanza?

"HAPPY NEW YEAR 2021"

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau
=====
Utakua bored

Wapi wameweka limit ya watu kuwa na watoto?
 
Mmenikumbusha marehemu babu yangu mzaa mama.

Mimi kwenye familia ni mtoto wamwisho ila nina mama zangu wadogo wawili ambao wananiamkia. Na hapo mama yangu sio mtoto wakwanza kwao. Yani mjukuu wakwanza wa marehemu babu amewazidi umri wajomba zake na mama zake wadogo wengi sana.
 
Kuna members wengi wajinga sana humu eti wanataka kunipangia kipi cha kuandika kana kwamba wananilipa pesa
Hujapangiwa bosi wala hakuna malipo

Hoja Tu imekua kituko

Unataka kuwapangia wazazi wazae lini lakini hutaki feedback ukipost kwenye public forum

I respect you a lot kamanda.... Ila Leo aisee
 
Back
Top Bottom