Bado kuna wazazi wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili

Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiForums.

Ndugu zangu Watanzania;

Bado kuna watu wazima wanaendelea kuzaa hata baada ya mtoto wao wa kwanza kuolewa? Mtoto wa mwisho analingana na mjukuu wa kwanza? Huku ni kukosa maadili.

View attachment 1667340

Siku ya sherehe ya mwaka mpya nilikutana na dada mmoja anaitwa Veronica (hili sio jina lake halisi) ambaye nilimaliza naye shule ya msingi mwaka 1999.

Huyu dada nilikwisha kutana naye mwezi kama wa August maeneo ya Banana Ukonga huku Dar. Kwa kuwa tulikuwa hatujaonana miaka takribani 15 tulipiga story nyingi sana za zamani.

Sasa nilipokutana naye tena Ijumaa ya tarehe 01 January 2020 huku Kivule ninapokaa (kwa maana aliniambia anakaa Kata moja na mimi) nilimuona anaongozana na binti mdogo wa miaka kama 9 hivi.

Tena huyo binti wamefanana kweli kweli. Basi tulipoonana tulisalimiana tena kwa furaha sana. Baada ya story kadhaa nikamuuliza, huyu ndio mtoto wako wa kwanza? Akakataa. Akasema hapana, huyu sio mtoto wangu.

View attachment 1667350

Huyu ni mdogo wangu wa mwisho. Mtoto wangu ameenda kwa baba yake kusalimia atarudi shule zikifunguliwa. Sema ndio rafiki yake mkubwa sana huyu (mdogo wake wa mwisho) kwa maana wamepishana mwaka mmoja tu.

Mimi sikuwa na jambo lingine la kumwambia zaidi tu ya kumpa hongera lakini nikawa ninajisemea tu kimoyomoyo "ina maana haya masuala ya mtoto na mama kuzaa kwa pamoja bado yanaendelea katika karne hii ya 21?"

Hii issue nilikuwa ninaiona tu kwa wazee wa zamani ambapo unakuta mtu unakutambulisha "huyu ndio baba yangu mdogo/shangazi yangu tumbo moja na baba" au "huyu ndio mama yangu mdogo tumbo moja na mama" lakini ukijaribu kuwatazama actually wanalingana umri au wamepishana mwaka mmoja tu.

View attachment 1667352

Mimi ni moja kati ya watu wanaokerwa sana na lugha za hawa dada/mama zetu manesi lakini linapokuja suala la kukemea wamama/wababa wanaoendeleza utamaduni huu wa hovyo mimi ninawaunga mkono sana.

Kuna mtoto wa shangazi yangu mmoja yeye ni nurse huko Geita anakwambia mama mtu mzima wa design hii akija kujifungua (wanawafahamu sana kwa maana vijijini watu ni wachache) huwa wanawachamba kwa maneno na lugha chafu mbele ya waume zao.

Kuna mama mmoja aliwahi kufariki mwaka 2006 alipokuwa anajifungua wakati bado tunakaa kule Keko. Sasa wakati wa mazishi watu wamekusanyika na wageni wanataka kujua chanzo cha kifo chake ikawa sasa ni aibu kusema kuwa amekufa kwa sababu ya "complications" za uzazi ilhali binti yake mkubwa ana mtoto wa miaka 2 tayari.

View attachment 1667341

Mimi binafsi ninaona sio jambo la hekima wala busara kwa mama/baba kuendelea kuzaa watoto wengine wadogo ilhali wale "first born" wamekwisha kuwa wababa/wamama wanaokaribia ku-reproduce.

Sio vizuri mama kuonekana ana tumbo kubwa la ujauzito pindi wale "first borns" wanapokuwa wamepevuka akili.

Kwa maoni yako, ni sahihi mama na binti/mtoto kuendelea kuzaa kwa pamoja? Mtoto wa mwisho kulingana na mjukuu wa kwanza?

"HAPPY NEW YEAR 2021"

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Maoni ya wadau
=====
Mwaka 1999 ndio naanza shule, wewe unamaliza LA SABA 🤣🤣🤣🤣

Humu kuna vikongwe mnatupigia kelele sana
 
Watoto wengi wa uzeeni huwa wanakuwa mataahira na wana uwezekano mkubwa wa kupata mtindio wa ubongo.

Ndio shida ya jamii ya watu wenye elimu kiduchu.

Mkizaa mataahira mnaanza kuisumbua serikali na jamii kwa ujumla. Mnatengeneza matatizo yanayoweza kuepukwa.

Atii ooh mie ntazaa mpaka tone la mwisho! SO WHAT? ni sifa?

Mbegu bora za watoto ni za ujanani! Sio unazaa mataahira ya uzeeni halafu unajisifu!
Well said
 
Amri kutoka kwa mungu au ulevi wako tu na elimu kiduchu uliyonayo?

Haiwezekani zee lina miaka hamsini bado linazaa tu!

Mtoto wako anazaa na wewe unazaa! SHAMEFUL!

Mnakuwa kama familia ya masungura!
Wanakuwa wanajenga ukoo wa hovyo sana
 
Kwa hiyo mwanaume aliyeoa binti yako anakuja kumpa hongera mkeo (mama mkwe wake) kwa kujifungua mtoto mchanga (shemeji yake)?
Tatizo liko wapi Sasa akijakupongeza?

Unataka kumaanisha, mtoto wako akiolewa Basi unatakiwa kutengana vyumba na mkeo ili watu wajue huwa hamfanyi chochote?

Mama mkwe kuzaa kunaleta shida gani ndugu

Inamaana tatizo lenu ni kuonekana baba anafanya mapenzi na Mama wakati binti yao ameanza kufanya mapenzi?
 
nitaona kawaida, as long as kaipata kwenye mahusiano halali ya ndoa, yenye kueleweka, halafu,

ukiona hadi nina umri huo halafu maza bado kawa na uwezo wa kushika ujauzito maana yake alinizaa mapema sana, hivyo atakuwa sio mzee bali mwanamama tu, nitaona freshi tu, mradi mahusiano yake yawe ya kueleweka
Hakika dunia ni uwanja wa fujo
 
emoji23.png
emoji23.png
 
Binafsi hii kitu pia siipendi.Mama kuendelea kuzaa na watoto wake nao wanazaa.Kwa case ya kwamba alianza uzazi akiwa bado Mdogo inaeza ikawa Sawa.Lakini katika mazingira ya kawaida mama ana miaka50 anajifungua mtoto wa Saba huko,na mwanae anajifungua mtoto wa pili.Dah kwangu naona sio kitu kizuri Sana.Nani atamsaidia mwenzie kubembeleza mtoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom