Bado kuna wanaopigana sababu ya mapenzi?

black abdu

Senior Member
Dec 2, 2022
152
208
Siku moja kuna jamaa, si rafiki yangu lakini tulikuwa tu afahamiana nae, amekuja na story kuwa alikuwa amevutiwa na msichana niliyekuwa natoka nae. Sikufahamu dhamira yake ila nilimjibu tu, "ongeza jitihada, unaweza kumpata"! Upande mmoja nawaza labda nilikosea, ningemwambia aache fikra zake kwa kuwa yule alikuwa mtu wangu, au ningegombana nae, au ningeanza kufatilia kama wana chochote kati yao na alikuja tu kunipima!

Upande mwingine nawaza kuwa nilifanya sahihi, kwa sababu ikiwa huyu ni msichana huru, timamu wa akili na ufahamu, anahitaji kutumia akili yake kufanya maamuzi yake badala mimi kumfanyia.

Vipi nagombana au kuwekeana chuki na mtu na kumbe msichana mwenyewe kaniegesha tu moyoni? Ningeumia kichwa changu bila sababu.

Si kuwa sikumpenda au sikujali kumpoteza ila napenda zaidi mtu akae na mimi kwa sababu moyo wake unanihitaji kama ninavyomuhitaji, na kama ni hivyo basi atasimama kumkataa kila mwanaume anayejitokeza kumtaka.

Ukweli huwa nashangaa kusikia watu wamegombana kwa sababu ya kuchukuliana wapenzi. Zamani nilikuwa naona hizo, unasikia wadada wameviziana njia ya kwenda sokoni, wakapigana sababu mmoja ameenda na mtu wa mwenzie... na ukute hapo wote ni michepuko wasiojijua.

Naongelea zamani wakati "mchepuko" haukuwa umeingia kwenye misamiati bado.... watu walikuwa hata kugombana na kupigana ni kistaarabu, tofauti na tuliyoyaona baada ya kuzuka kwa mitandao ya kijamii, tunaona video za kufaniana na watu kufanyiwa vitu vya ajabu, utasikia msichana kaungana na wenzie wamemvamia "mwizi" wake na wanamchukua video kuwa iwe funzo kwa wengine.

Au jamaa kafanyiwa ufirauni na kundi la "njemba" kwa sababu katembea na mtu wa mwingine.

Je, hayo uthibitisho wa mapenzi ya kweli?

Natambua kweli moyo unaopenda huumia sana lakini je, kupigana na kudhalilishana ndio suluhisho?

Mi nikijua msichana wangu ametembea na mtu mwingine kwanza nitamuuliza kama ni kweli, na anitajie sababu ni zipi, kama kanichoka au kule anapata asivyopata kwangu ni bora niuguze moyo kuliko kuhatarisha maisha yangu kwa msongo wa mawazo.

Kwa nini nitaongea nae na kutaka awe mkweli, kwa sababu kama yeye ameshamfia huyo mwingine, hawezi kumwacha, anaweza kufanya kwa siri na matokeo yake kuniletea maradhi. Bado ninaamini kama ananihitaji atapata namna ya kutunza huba letu.

Naelewa kuna kuteleza, kwa vile si wakamilifu lakini si hadi mzinga umechongwa na asali inarinwa kila siku.

Naogopa sana maradhi!

Sasa siku hizi kumekuja visa vipya kwa jina la "wivu wa kimapenzi". Tunasikia mtu amekatwa nyeti, Mama kwe na mwanae wauliwa risasi, jamaa kachomewa nyumba na vitu vote, na wengine kujidhuru, kisa? Wivu wa kimapenzi.

Mi naomba tu nionekane fisi au "boya" ila bora nikae ndani nilie kuliko kwenda kufanya mambo ya ajabu.

Kuna dada mmoja, yeye alihisi nyendo za mumewe hazikuwa sawa, akahoji lakini jamaa akakataa. Dada wa watu akafanya upelelezi wake kimya kimya, akapata vithibitisho vyote alivyovihitaji kisha kimya kimya akajiondoa. Hadi hii lei jamaa anambembeleza ila dada hakubali.

Hivi kwanza katika dunia kama hii iliyojaa magonjwa inakuwaje msichana anakubali kurubuniwa na mwanaume mwingine? Hadi anaenda kutembea nae? Heshima na utu wake viko wapi?

Pagumu ni hapa kwa sisi wanaume, kutamani kila tunachokiona. Kwani hakuna dawa? Au kuna ulazima wa kufanyia kazi kila hamu tunayoihisi? Hapo tunakuwa watumwa wa nafsi/Manamanio.

Kuna kijana mwenye busara alinifundisha kuwa kupata matamanio ni kitu kimoja, huna kosa hapo kwa sababu moyo huwa mkorofi.....ila kuyafanyia kazi hayo matamanio ndio hugomba na ndipo ibilisi na washkaji zake walipo.

Ndio maana, zinaa imepigiwa marufuku kwenye dini zote; kuran inasema hata usiikaribie.

Nikirudi kwenye nukta yangu ni kuwa siafikiani na tunayoyqona yanatokea kwa jina la Wivu wa Kimapenzi, kuna namna bora ya kukabiliana na uhalisia kuliko kufanya yanayofanyika.
 
Inategemeana na NTU na NTU!...kama mtu amewekezaga kila kitu kwa mwenzie then ikatokea cheating,hapo ngumi zitarushwa tu hakuna namna!!Lakini mimi naona ni uzuzu kumwamini binadamu mwenzako hadi kufikia hatua ya kupigana 7bu ya maamuz yake,damn,LET IT GO!
 
Tatizo makala ndefu sana sijui umeandika Nini lakini kama ni hicho hicho kilichopo kwenye heading basi nikujibu tu hao watu Bado wapo sana na tunaishi nao

Wapo wanaopigana kugombea mwanamke, wapo wanaopigana kugombea mwanaume, na wapo wanaopigana kwa ugomvi wao wenyewe ndani ya mahusiano/ndoa Yao

Ishi vizuri na viongozi wa ngazi za chini, wanakumbana nao sana hao
 
Back
Top Bottom