Babie Kabae na Udini Clouds Tv

Kwani uislamu una ubaya gani?!!.......acha ujinga kijana!
sijui umemuelewa mtoa mada "... maudhui ya kipindi sio kuongelea habari za kidini MA ndio maana kikawa na wafuatiliaji wa dini tofauti "... hizo habari za masuala ya dini anazozileta zitakuja kuua kipindi " kwa sababu kila mfuatiliaje na yeye atataka aanze kusikia dini yake ikiongelewa vyema
 
Mbona waziri kabudi huwa anapenda kutoa reference za verse za Bible kila risala zake lazima adokoze na anatuongoza Atheists ,islam,christians na dini nyinginezo na hata ukifuatilia bunge kuna wabunge ambao ni public figures hufanya hivyo pande zote 2 na watu hupotezea na huchukulia kawaida

Mimi naona hizi minor issues kuzifanya mjadala na kuumia ni ujuha tu na si za kutilia maanani..

Badala muumie freedom of press,utawala bora,ufisadi,rushwa lakini mnakaa vijiweni mnamlalamikia kababy tena umesema vijiwe vingi..wacha mh Rais awapeleke puta kwa watu wa aina hii
 
Mbona mchungaji Masanja mkandamizaji jumatatu alikuwa kwenye kipindi hicho hicho akihubiri Injili au haujamuona!!......acha kuwapangia bhana.
Huyo kama alikuwepo alikuwa mwalikwa na walimwalika wakijua kuwa ni mchungaji, hapa tunaongelea mtangazaji mwajiliwa anayetakiwa kuwa neutral
 
"Asalaam aleykum" ndio inayokuuma ww! Ndio salaam kuu kwa sasa maeneo yote ya mijini, hii salamu wala haijakaa kidini, inamtakia amani kila mwanadamu/haijambagua mtu,

"Tumsifu yesu kristo" hii salamu imeshawatenga wangapi? Imekaa kidini dini/kibaguzi sana,
 
Kwanini usiseme AMANI KWAKO?
 
Asubuhi yote hiyo unakaa kwenye vijiwe vya kahawa? Halafu Magufuli anasema Watanzania wanachapa kazi uchumi umekuwa???

Hapa haitaji Elimu ya Economic kujua hali ya Tanzania kiuchumi ipo je......
 
Ninajua kinachokusumbua ni elimu yako ndogo katika mahusiano na watu walio na imani tofauti na wewe.

1. Nani asiyejua salamu hiyo ulioitaja inatumiwa na ninyi

2. Nani asiyejua kuwa hayo ni maneno ya kiarabu yenye maana ya amani iwe nawe?

3. Sasa umeeleza salamu ya wakristo lakini nikuhakikishie hakuna mkristo anayemsalimia mtu ambaye sii wa imani yake kwa salamu hiyo

4. Hata maneno yake yawe mazuri vipi , kwa kitendo cha kuwa ndio salamu rasmi ya dini fulani ni makosa makubwa sana kulazimisha kumsalimia mtu wa imani tofauti kwa salamu ile

5. Salamu maana yake unamtakia heri na yule anayesalimiwa anatakiwa afurahi kwa maneno uliomtamkia, kinyume na hapo ukinisalimia kwa salamu inayotumika kwenye dini yako naona zaidi u nanikebehi zaidi ya kunisalimia na umeshaniaribia siku hapo, maaana ninaanza kukuchambua sababu ya wewe kunisalimia salamu hiyo huku ukijua fika ni wa imani nyingine.

6. Kwa taarifa yako hata wakatoliki uliowataja wana salamu ya kilantini yenye maana kama hiyo "Pax vobiscum" lakini hawaitumii kwa watu wa imani nyingine kwa sababu kilatini ni lugha rasmi ya kanisa katoliki , kama ilivyo kiarabu lugha rasmi ya dini yenu. Ukishslijua hilo ili kuendelea kuishi kwa mahusiano mazori ya kuonyesha kuto kudharau imani za watu wengine ni vyema kama kuna salamu ya lugha ya kigeni mnayotumia miongoni mwa waamini wa imani fulani muendelee kuitumia ninyi kwa ninyi, na mnapokutana na mtu wa i mani nyingine, tumia salamu ya kawaida ya lugha ya taifa hata kama haina tafsiri nzuri kama unavyotaka, hata kama imetoholewa kwenye lugha nyingine sii kitu. Ni vyema kutokunisalimia kabisa kuliko kunisalimia kwa salamu ambayo itanikera. Haya kama mkatoliki akikomaa sasa naye awe anakusalimia "Pax vobiscum" wewe utajibu nini ama utafurahi? Hata kama anajua namna ya kujibu ama unajua maana yake si utaamini anataka kuiona salamu ya dini yake ni suprime over oll other?
 

Sidhani kama ni Mdini kihivyo ila ninachojua tu ni kwamba hupenda kufanya ' references ' za mambo na matukio mbalimbali kupitia Imani yake ya Kiislamu na sijaona tatizo hapo. Kwa kukusaidia tu hapo hapo ni kwamba wapo Watangazaji wengine ( siyo Waislamu ) na Wao wakiwa katika Vipindi vyao mbalimbali hupenda mara kwa mara kufanya ' references ' za Kidini ( tena za Kikristo ) kama Mwanadada Maria Edward Mzurikwao wa Magic fm.

Hata hivyo nadhani Wewe jukumu lako Kubwa hapo linatakiwa Kusikiliza tu kile ambacho unakiona Kwako ni bora / sahihi na hayo mengine yanayokukwaza unaweza ukaachana nayo au ukayapuuza na hakuna kitakachoharibika. Hivi ukiwa unakula Wali wao Nyumbani na bahati mbaya ukakutana na Mawe kadhaa utaacha Kula kwakuwa umeyakuta hayo Mawe au utayapangua tu hayo Mawe na kuendelea zako Kutiririka na Kuserereka na Kula?

Wengi wetu hasa ( tunaoabudu ) Makanisani na Misikitini mara kwa mara hasa katika Mafundisho / Injili za Viongozi Wetu kuna muda utakuta ama wanaongea tu Pumba au wanakugusa ( mnaita wanagonga Ikulu ) je ina maana hali ikishakuwa hivyo basi unatakiwa uchukie na uondoke au unatakiwa tu kuvumilia na kuyapokea yote?

Na sidhani kama huyo Mtangazaji ' Genius ' Babie Kabae ana Kiwango hicho cha Udini ( Uislamu ) kama usemavyo japo Mimi ni Mkristo tena Mkatoliki wa Kutukuka kabisa. Na kwa maelezo yako yote unaonekana nyuma ya Pazia hoja yako hapa siyo Udini ( Uislamu ) wake bali naona kama vile una Kisununu / Husuda tu dhidi ya huyu Mwanamke. Hakuna Mtangazaji ninayemkubali, ninayemuheshimu, Mwerevu na makini kama Babie Kabae wa 360 Cloudstv.
 
Mbona uwa hulalamiki kuwa kila siku clouds redio wanapiga nyimbo za gospel za akina goodlucky gosbert na wengine kweny vipidi ambavyo siyo vya dini? Au huo si udini? Tuahce ***** ***** maana laiti zingekuwa zinapigwa Qaswida pasingekalika
 
ok
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…