Baba yako Shuleni alikuwa anashika namba ngapi darasani ??

Duduwasha

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
5,703
3,653
Nakumbuka Baba yangu alinihadithia kuwa yeye alikuwa anashika nafasi ya kwanza kwenye mitihani yake na kuna siku alishika nafasi ya pili akalia sana mitihani iliyofuata akawa wa kwanza tu ...

je Baba yako alikuwa wa ngapi maana shuleni niliwahi hadithia kuhusu mdingi wangu na wao wakasema baba zao pia walikuwa wa kwanza tu je mdingi wako na wewe alishika nafasi gani? au kuna wengine baba zao ndio walikuwa wa Mwisho Darasani?
 
Baba yangu mie shule hakwenda, lakini ngumbaro alihitimu.
So kusoma, kuandika alifahamu, na muamala wowote uhusianao na issue za transactions alikua mahiri sana.
Alifariki kaniachia nyumba 6, na zote ziko kwenye miji mikubwa ya kibiashara.
Wewe Babako anamiliki nyumba ngapi ?
 
baba yangu alikua na mtiani mmoja wa mafunzo ya police, mtiani huo alikua amepata 98,sasa basi kila siku nikifanya mtiani anauleta kulinganisha na wangu.da! Ilikua ngumu kuufikia huo wake.
 
Mdingi anasema alikuwa around namba 3 lakini namuamini sababu kuna BA Econ & Statistics First Class inaning'inia chumbani kwake.
 
Namba sio kitu. . zipo hata za kubahatisha na za kukariri. Muhimu ni kujifunza na kutumia mtu anachojifunza.
Hivi kuna ulazima wa kujibu tread hata kama huna cha kuandika? umeulizwa babako alikuwa anashika namba ngapi? wewe unasema namba sio kitu....if so....hii sio thraed unayopashwa kuchangia....
 
Hivi kuna ulazima wa kujibu tread hata kama huna cha kuandika? umeulizwa babako alikuwa anashika namba ngapi? wewe unasema namba sio kitu....if so....hii sio thraed unayopashwa kuchangia....
Wewe UNAPASHWA?
 
Sijui alikua anashika namba ngapi ila ni mwanafunzi pekee alichaguliwa kwenda sekondari,alitoka kijijini kabisa wilaya fulani mkoani Mbeya akaenda Galanos Tanga,
Then 5&6 Azania na kwenda Oxford for his Bachelor Degree Education,then MA Economics, UDSM.
Nashangaa mie hiki kichwa sijui cha mama!
Inawezekana alikua anashika no 9 lakini ndio hivyo.
 
Kushika namba si hoja!

Mimi ningependa kujua wale wavumbuzi wa ndege walikuwa wakishika namba ngapi darasani kwao wakati wanasoma.
 
Alisomeshwa na kijiji, akaishia darasa la 8, mungu akamjaalia akaenda mpaka Cuba katika mafunzo ya kijeshi, akashika nafasi mbalimbali za uongozi, Zaidi ni mmoja wa wazee waliofundishwa uadilifu na kulitumikia taifa kwa moyo wa kizalendo. Akafa hana kitu.

Kweli JK Nyerere alikuwa na viongozi waliojituma na sio viongozi maslahi wa JK Kikwete.
 
Wazee wetu wakiwa wanataka watoto wao wawe na bidii ya kusoma.. Pole Sana Afrodenzi naogopa kukuuliza zaidi jamani
 
eti anasema ya kwanza, namuuliza mbona kila mzazi anasema ya kwanza? anasema hajui ila yeye ndo alikuwa kinara darasani, hakuendelea coz mzee wake alitaka achunge ng'ombe huko lushoto.
 
Back
Top Bottom