TANZIA Baba yake Young Dee, Brigedia Jenerali Dr. Robinson Mboli Mwanjela, afariki Dunia

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
1672246240742.png

20221227_211309-jpg.2461124


Elimu: >> source pdf page 90 <<

  • Degree ya udaktari, MD- Doctor of Medicine- UDSM
  • Masters ya udaktari, MMed - Masters of Medicine - UDSM
  • Masters ya jeshini, MSS - Master in Security and Strategies - Chuo cha taifa cha ulinzi - NDC.

Kazi

Tarehe 20 Januari 2014, Rais mstaafu Jakaya Kikwete ambaye pia alikuwa Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama alimpandisha cheo kutoka kanali kwenda kuwa Brigedia Jenerali >> source 2 <<

Kabla ya kustaafu, aliwahi kuhudumu kama mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Tiba - Lugalo.

Aliwahi kuwa mkufunzi / lecturer chuo cha IMTU idara ya internal medicine (taarifa ipo source 1 )

.....................................

Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na mtoto wake David almaaruufu Young Dee aliepost msiba huo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa instagram, jana tarehe 27-12-2022 mida ya jioni.

images (24).jpeg


Updates;

Brig General Robinson Mboli Mwanjela ameagwa leo, asubuhi saa tatu pale Lugalo, na saa saba baada ya misa katika kanisa la Wazo Hill KKKT.

Pale Lugalo zilitolewa heshima zote za kumuaga kijeshi, na procession ya kuutoa mwili mortuary ilikuwa very touching.

Kule Wazo Hill Majenerali wamemmwagia sifa za kazi yake kama Ofisa wa ngazi za juu aliyekuwa muadilifu katika utendaji wake kulitumikia jeshi la wananchi (JWTZ)
 
View attachment 2461001

Brigedia Jenerali (Dokta) Robinson Mboni Mwanjela aliwahi kuhudumu kama mkuu wa Chuo cha Kijeshi cha Tiba - Lugalo.

Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na mtoto wake David almaaruufu Young Dee alipost msiba huo kwenye ukurasa wake wa instagram.
Hili jina nilisikia mara ya mwisho wakati wa Kampeni za Uchaguzi kanda za juu kusini? Au nimechanganya majina?

R.I.P bregadia
 
Sio kila mwa ni wanyaki, kuna Kina mwa wabena, wahehe, wasangu, wasafwa, wandali, n.k. nikicheki katika hao waliojazana jeshini ni wanyalukolo, hivyo kuna uwezekano mkubwa ni mnyalu,

Pia ingekuwa ni mnyaki basi wangekuwa wamesafirisha kyela ama tukuyu maana ni nadra sana mnyaki kuzikwa nje ya Mbeya.
Huyu mnyaki mdgo wangu dgo Young D kwao Mbeya Hilo jina la katikati wengi ni wanyaki
 
huyu wa mbeya kabisa kule rungwe juu milimani karibu na shule ya rungwe boyz
Majina ya Mwa--- yanatumika sana kwa wanyakyusa lakini haimaanishi kila Mwa--- ni mmyaki. Haya majina ya Mwa--- yapo pia makabila mengine ya mikoa ya Mbeya, Njombe na Iiringa.

chifu mkwawa alikuwa na jina la Mwamuyinga lakini ni mhehe,

Mwanshinga ni jina la chifu wa wasafwa, pia wapo wasafwa kina mwaihoyo, mwantinda, mwandele, mwanzanga, mwasote, n.k.

Nilikuwa na rafiki baba yake yupo jeshini anaitwa Mwamanga lakini alikuwa mbena, pia wapo wabena wengine kina mwajombe, mwandulami, n.k

Wapo kina Mwakipande ni wakinga,

, n.k.

Point yangu kuu ni kwamba tusiwe na haraka kufanya hitimisho
 
Tunaendelea kupata uthibitisho.. hilo jina la Mwa--- limesambaa kwa makabila ya kanda za juu kusini. Mike tee jina lake ni Mwakatundu lakini ni mhehe, Nilikuwa na rafiki baba yake yupo jeshini anaitwa Mwamanga lakini alikuwa mbena, kuna wengine wanaitwa kina Mwakipande ni wakinga, wapo wanaitwa kina mwashinga ni wasafwa, n.k.
Shida sio majina hayo yakianzia na mwa hila linakuwa maana kabisa Kwa kinyakyusa huwezi kusema mwashinga ni mnyakyusa hapa kuna maana linaleta huyo mshua ata ukimuangalia Kwa Sura mnyaki huyo wanyambara wa Mbeya tunajuana Kwa sura
 
Shida sio majina hayo yakianzia na mwa hila linakuwa maana kabisa Kwa kinyakyusa huwezi kusema mwashinga ni mnyakyusa hapa kuna maana linaleta huyo mshua ata ukimuangalia Kwa Sura mnyaki huyo wanyambara wa Mbeya tunajuana Kwa sura
Tuishie hapa!! Kwa faida ya uzi huu acha tufanye iwe hivyo ili tusiyarefushe mabishano ya majina ya kikabila, ni jambo la busara tujikite kwenye maombolezo.

Apumzike kwa amani Kamanda
 
Back
Top Bottom