Baba mzazi wa Lulu aibua mazito | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baba mzazi wa Lulu aibua mazito

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ketwas, Apr 13, 2012.

 1. ketwas

  ketwas JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 213
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Baba mzazi wa Lulu aibua mazito
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Thursday, 12 April 2012 21:36 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  [​IMG]BABA mzazi wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu,'

  ATAKA JAMII ISIMHUKUMU MWANAWE, HAKI ITENDEKE, AELEZA USHIRIKA WA LULU NA KANUMBA
  Daniel Mjema
  BABA mzazi wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu,' ameitaka jamii kutomhukumu mwanawe kutokana na kifo cha msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba, badala yake iache vyombo vya sheria vifanye kazi yake.

  Mzazi huyo, Michael Edward Kimemeta anayeishi mjini Moshi, amewaomba Watanzania kuiachia Mahakama iamue kama mtoto wao anahusika katika kifo hicho ama la.

  Kimemeta, ameeleza kuwa binti yake ana umri wa miaka 16 tofauti na inavyoelezwa kuwa ana miaka 18.

  Juzi Lulu alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.

  Kumekuwa na utata uliojitokeza kuhusu umri wa Lulu. Wakati mwenyewe akieleza kuwa ana miaka 17, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa umri wake ni miaka 18 na juzi Mahakama iliambiwa kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na baba yake akisema ana miaka 16.

  Kwa upande wake, mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, alisema tukio la kifo cha Kanumba na kukamatwa kwa binti yake Lulu, limempa mshituko mkubwa na kumsababishia maradhi ya kisaikolojia na kimwili.

  “Hayo yaliyotokea kwa kweli yamenifanya niumwe kabisa hapa sasa hivi nimelala naumwa…nimempa go ahead (ruksa), baba yake azungumze kwa sababu taarifa zote anazo. Naomba mimi mniache kwa sasa,”alisema.

  Kimemeta aliliambia Mwananchi jana kuwa mwanawe huyo alizaliwa Aprili 17 mwaka 1995 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

  “Nataka nikuambie (mwandishi) mwanangu atatimiza umri wa miaka 17 ifikapo Aprili 17 mwaka huu. Sasa ana umri wa miaka 16 na ni mtoto. Tunavyosikia Kanumba alikuwa mpenzi wake inatuuma sana,” alisema.

  Baba huyo alisema alizaa na mama yake Lulu lakini hawakuwahi kuishi pamoja. "Mwanamke huyo alikuwa akifanya kazi Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na muda wote Lulu alikuwa akiishi na mama yake jijini Dar es Salaam,"alisema Kimemeta.

  Ameomba familia ya marehemu Kanumba ikubali kupokea pole ya familia ya Lulu kupitia gazeti hili kutokana na mazingira kutoruhusu familia hizo kukutana.

  “Nasikitika mazingira ya tukio lenyewe mpaka sasa hayaruhusu familia yetu kwenda kutoa pole na kuifariji familia ya Kanumba kulingana na utamaduni wa mwafrika…tunaomba wapokee pole zetu kupitia njia hii,” alisema.

  Kwa mujibu wa Kimemeta, hivi sasa wanahofia maisha yao kutokana na jamii kujenga mtazamo hasi juu ya tukio hilo hata bila ya kusubiri vyombo vya sheria kusikiliza ushahidi wa tukio hilo na kutoa hukumu yake.

  Alisema kuwa jamii inapaswa ifahamu kuwa, kikatiba mtu yeyote anayeshitakiwa kwa kosa lolote haimaanishi tayari ni mkosaji, bali atahesabiwa kuwa mtuhumiwa hadi pale Mahakama itakapomtia hatiani.

  “Yanasemwa mengi mara ooh Kanumba ndio alianza kumpiga mwanangu mara ooh Kanumba alisukumwa …mimi nasema tuiache Mahakama hata sisi hatupendi mtu auawe, lakini Mahakama iachwe itende haki,”alisisitiza.

  Akizungumzia maisha ya mwanawe Lulu, Kimemeta alisema alipokuwa akitangaza Kipindi cha Watoto Televisheni ya ITV, walifarijika sana, lakini alipoanza kuingia kwenye sanaa ya filamu, walijua sasa wamempoteza.

  “Baada ya kuingia kwenye sanaa ya maigizo niliona kabisa tumempoteza mtoto na nilimweleza mama yake kuwa wale aliokuwa nao katika maigizo akiwamo Kanumba mwenyewe, nilikuwa siwaamini hata kidogo,” alisema.

  Kimemeta alidai kuwa siku moja mwanawe alimpigia simu akimwarifu kuwa alikuwa anakwenda jijini Arusha kurekodi filamu na Kanumba, yeye alipinga safari hiyo akitaka Kanumba amthibitishie usalama wa binti yake.

  “Kwa sababu nilikuwa sipendezwi na hayo mambo nilimwambia mama yake azungumze na Kanumba na akatuhakikishia atamlinda na kambi yake ina maadili, lakini kumbe huo ndio ukawa mwanzo wa mwanaye kugeuzwa mpenzi wa msanii huyo,”alidai.

  [​IMG]Elizabeth Michael 'Lulu,'

  Baba huyo mzazi alidai kutofanya vizuri darasani kwa mtoto wake huyo, kulichangiwa na hatua ya kuingia katika sanaa ya uigizaji.


  “Lulu alikuwa mtoto mwenye tabia nzuri sana hata alipokuwa ITV kwa kweli alitutia moyo wazazi wake kwa jinsi ITV walivyokuwa wakimlea, lakini alipojiingiza tu kwenye uingizaji hapo ndipo mambo yalipoharibika,” alisema.

  Alikanusha madai kuwa mwanawe hakumaliza kidato cha nne na kusisitiza kuwa Lulu alisoma Shule ya Kimataifa ya St Mary's na baadaye alihamia Shule ya Sekondari ya Midway High School na kumaliza kidato cha nne mwaka jana.

  Alisisitiza kuwa katika mambo yaliyokuwa yakiwaumiza mioyo, ni namna mtoto huyo alivyozidi kuharibika kwa kuingia katika fani ya uigizaji filamu.

  Alisema angependa kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili azungumze naye kama rafiki yake na watafute suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.

  Alisema tayari ameanza mchakato wa kuonana na Rais Kikwete ili amweleze siri aliyodai ni ‘nzito’ na kudai tayari ametafuta wazee watatu wenye busara wa kumsindikiza, endapo Rais atakubali ombi lake.

  Pia ameziomba taasisi zinazojishughulisha na masuala ya haki za binadamu na msaada wa kisheria, kujitokeza na kumsaidia mwanawe.

  Lulu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi na kusomewa shitaka la kumuua
  Kanumba, tukio lililotokea Aprili 7 mwaka huu eneo la Sinza Vatican.

  Msanii huyo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina
  mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mauaji na hivyo alipelekwa rumande Gegeza la Segerea hadi Aprili 23 mwaka wakati kesi hiyo itakapotajwa.

  Kifo cha msanii huyo kimetikisa nchi kutokana na umaarufu wake, akiwa ameigiza filamu 40 zilikuwa zikirushwa katika vituo mbalimbali vya
  televisheni ndani na nje ya nchi.


  Kanumba alipanga kujenga shule

  Katika hatua nyingine, Fidelis Butahe na Pamela Chilongola wanaripoti kuwa mchaguaji maeneo ya kupigia picha za filamu za msanii Kanumba, Rahim Khatib alisema marehemu Kanumba alinunua eneo la ekari 15 huko Mpiji mkoani Pwani kwa ajili ya ujenzi wa shule yake ya sekondari.

  Khatib alisema Kanumba alikuwa na mpango huo muda mrefu na kwamba lengo lake lilikuwa kuwasaidia wanafunzi wa eneo hilo ambao hutembea muda mrefu kutokana na shule kuwa mbali na eneo hilo.

  “Kanumba alikuwa na mipango mizuri katika maisha yake, kuna eneo kubwa alilonunua Mpiji ili ajenge shule ya sekondari,” alisema Khatib.

  Alifafanua kuwa hadi anafariki dunia, aliacha kiasi cha fedha zaidi ya Sh 40 milioni katika Kampuni yake ya Kanumba The Great.

  “Marehemu ameacha fedha zaidi ya Sh 40 katika kampuni yake, magari matatu na hivi karibuni alinunua jingine aina ya Toyota Land Cruiser, ”alisema Khatib.

  Katika hatua nyingine Khatib alisema kifo cha Kanumba ni pigo kwa watu waliokuwa wakifanya naye kazi akiwemo yeye mwenyewe kwa kuwa walikuwa wakimtegemea kwa kiwango kikubwa.

  Sintah naye alonga

  Kwa upande wake msanii maarufu wa filamu nchini, Christina Manongi maarufu kama Sintah ambaye alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kufika nyumbani kwa marehemu Kanumba muda mfupi baada ya msanii huyo kuanguka, alisema kuwa siku tano kabla ya Kanumba kufariki, alikuwa na hasira tofauti na alivyomzoea.

  Sintah ambaye alikuwa na msanii huyo katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Jumapili ya Aprili mosi pamoja na mwigizaji mwingine, Steve Nyerere alisema kuwa kila alichokuwa akimuuliza Kanumba, alimjibu kwa ukali.

  “Ni tofauti na nilivyomzoea, siku ile ya Jumapili tulikaa pale Leaders Club mpaka usiku sana na kila jambo nililokuwa nikizungumza naye alinijibu kwa mkato na ukali kweli, ilinishangaza,” alisema Sintah

  Alifafanua kuwa moja ya mambo waliyokuwa wakizungumza na Kanumba ni pamoja na yeye kutaka kuacha uigizaji, suala ambalo marehemu Kanumba hakuliunga mkono na kumjibu kwa ukali kuwa asijitoe katika uigizaji.

  source mwananchi

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Alisema angependa kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili azungumze naye kama rafiki yake na watafute suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.
  Rais Kikwete kweli ana suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa? Just wondering
   
 3. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Wizi mtupu!
   
 4. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Yeye mwenyewe hana maadili,
   
 5. S

  SI unit JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 1,938
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kwanza amuulize binti yake kwa nini alisema ana miaka 18..
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Suluhisho unalo wewe inavyoelekea, tupe maelekezo ya suluhisho lako.
   
 7. Shagiguku

  Shagiguku JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 400
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  sawa sawa waungwana, tusubirie haki ya mahakama itatenda kazi yake....!
   
 8. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Wazazi kama hawa ingebidi wachunguzwe na ustawi wa jamii ikigundulika wana play part kwenye kuharibika kwa binti yao wafungwe hata mwaka mmoja. Lulu amekuwa ashikiki utadhani hana wazazi? Kama ni below 18 na walisikia kuwa anajengewa sijui ameshajengewa nyumba na kigogo kwa nini hawakufuatilia huyo fataki ashitakiwe? Akileta fedha mnachekelea leo anashitakiwa kuuwa eti under 18; under 18 my foot. Eti tulimkabidhi Kanumba mtoto wetu amlee; are you serious???; utampaje mfupa fisi akulindie? Utampaje kijana lijali uangalizi wa mwanao wa kike??? Ili liwe funzo kwa wazazi wanaoshangilia either explicitly or implicitly uchafu wa binti zao.
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  That's the Spirit.
  You don't reject your own flesh, no matter what.
   
 10. Brown ad

  Brown ad JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 347
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Huyo sintah nae akakojoe akalale kanumba na alimjua kama yeye ni mnafki ndio maana alikuwa anamjibu vibaya
  na kumbe sikujua kumbe mtu akikasirika ni dalili ya kukalibia kufa,
   
 11. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Utamlinganisha Lulu na Professional sex workers maeneo ya Ambiance na popote hapa Dar?

  Hata kama alipinda, alikuwa na kazi yake.

  Kuna wafanyakazi wengi tu maofisini wamewekwa vinyumba na kujengewa na mafataki.

   
 12. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Wewe unaongelea wafanyakazi na professional sex workers wakati hapa point ni mtoto mdogo under 18. Angekuwa na kazi ofisini au profesional sex worker sidhani hata wazazi wake wangepata jeuri ya kuzungumza. Wanaongea kwa point kuwa ni mtoto mdogo; that is why nasema kama ni mtoto wao wameplay part gani kumfunza a behave kulingana na umri wake???

   
 13. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mzee kapagawa! Kweli maadili ambayo msingi wake huanzia ngazi ya familia yeye anataka kuanzia ngazi ya taifa, anyway kikwete mwenyewe kaelemewa mbaya hajatimiza ahadi yoyote ile aliyoahidi wengi,ndio atatimiza ya huyo mzee mmoja,
  kama anataka akaongee na JK amsaidie atoke halafu ajilipe hapo sawa,
  pia kuna taarifa nilizipata kuwa kuna majambazi 6 yaliuawa mmoja wao akiwa binti wa jk pande za morogoro hivi wakiwa wamevamia benki, walikuwa na gari la usalama wa taifa,mwenye taarifa zaid zenye ukweli wa hili
   
 14. Nicksixyo

  Nicksixyo JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 949
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Masaburi aka akili mgando.Ndio madhara ya mtoto kulelewa na mzazi mmoja wakati mzazi mwingine anakula good time.
   
 15. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  panahusika sana hapo kwenye RED
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  May be yes/may be no.

  Industry ya entertainment karibu sehemu zote wanafanya kazi katika mazingira magumu hasa upande wa mahusiano iwe above 18 au under 18. Lulu hana exception, maana hata walioanza wakiwa wakubwa wameshajipindia tu.

  So wazazi labda walaumiwe kwa kumruhusu mtoto wao kuwa mwigizaji.
  Siwezi walaumu wazazi wake moja kwa moja. Hapa kuna factors zingine za kuangalia.

  Upande mwingine, hata kama wasingemruhusu kuwa mwigizaji, bado kuna watoto wanauza na wako under 18, na wanajitegemea kwa kazi hiyo hiyo.  Angalia akina mifano watu walioingia kwenye fani ya usanii wakiwa wadogo hata nchi zilizoendelea wanakoishia.
   
 17. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kuna ukweli kuna tatizo katika single parenting. Nina dada yangu ni mjane; last born wake kashindikana ila sote tunajua tatizo ni malezi. Binti under 18 anarudi home usiku wa manane eti anatoka disco na mama yake anafungua mlango. Hiyo tulikuja jua baada ya yeye (sister) na mwanae kwenda kumsalimia baba yetu (babu wa mtoto) na baba to his suprise alishuhudia sister anaamka kumfungulia mtoto wake mlango usiku wa manane. Akafoka kesho yake sister anasema kama hataki wawe wanamtembelea aseme. Kwani anaona naye ameungana na wengine (sie) kumchukia mwanae.
  Huyu sister ukitaka undugu uishe ongelea vibaya kuhusu binti yake. Yani tumebaki tunasubiri afunzwe na dunia.

   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,945
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  jamani sasa najihisi kizunguzungu maskini LULU.Mungu akutie nguvu na kukutumia msaada toka pattakatifu pake. Jamani kwa waliofuatilia comments zangu nyingi juu ya huyu binti mtagundua kuwa nimekuwa nikiwalaumu sana wazazi wake kuliko kumlaumu Lulu. sasa nimethibitisha kuwa lawama zangu ni sahihi kabisa kwenda kwa wazazi wake. Miaka ya 2004 nikiwa mwanafunzi wa shahada ya ualimu UDSM NILISOMA KOZI MOJA ILIYOITWA CHILD HOOD PSYCHOLOGY. Kozi hii ilifundishwa na Dr Sima kweli nimegundua kuwa nilijifunza kitu pale.

  siwez kueka nondo zote hapa lakini ngoja nisummarize kwa haya machache:

  kwanini nawatuhumu wazazi
  1) kuwa single parented kid tena mikononi mwa mama peke yake kulimpa uhuru wa manyani kwani mama alikuwa lazy affair.
  2) baba kuwepo mbali siyo sababu ya kushindwa kufuatilia mwenendo wa mwanae hasa alipoona ameanza kubadilika. Baba ana influence kubwa sana katika malezi na ndio mana huwa akisema mara moja tu inatosha kwa mtoto kutii.
  3) kumuachia mtoto ajimiliki mwenyewe kosa sana kisheria kwani angeweza hata kufa akiwa kwenye kumbi za starehe. kwa mtot wa miaka 16 bado anatakiwa awe strictly under parents observation tena enzi zetu hata disco tukienda ni disco toto.
  4)upendo kwa wazazi haukuwep na ni kama vile baba alimwachia mama ahangaike naye kwani alijua mtoto mwenye hekima ni fahari ya babaye bali mpumbavu ni mzigo wa mama ye.
  5) siingilii mambo ya familia yao lakini ugomvi wa wazazi au kutokuwa na msimamo kati ya wazazi ni mateso kwa mtoto sana. manake hakuna aliyejali lulu analala saa ngapi, anatembea na nani ili apate nini au hata afya yake inaendeleje. labda niwaullize wazazi wake mara ya mwisho kumnunulia Lulu nguo ni lini? na je kwanini tusishawish mahakama iwafungulie hawa wazazi mashtaka kwa kushindwa kulea?
  6)hivi wanafikiri ni sifa kwa mtoto wa miaka 16 kuwa ameshaujua utu uzima kiasi cha kuzini bila mpangilio, na kukesha kwenye kumbi za starehe? binafsi nimekasirishwa sana na tabia yao hii. poor parents.
   
 19. Blaine

  Blaine JF-Expert Member

  #19
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 11, 2012
  Messages: 2,285
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  the parents were irresponsible! if lulu is a minor, then they shouldn't have allowed her to go away for acting. its their duty to raise her not Kanumba's drama camp or any1 else. there is nothing wrong with acting as long as the parent can watch over the child and it doesn't interfere with their schooling, friends e.t.c. Its funny that now he wants to talk to raisi and offer solutions to moral failings among the youth while yeye mwenyewe kashindwa na mwanae.
   
 20. nyumba kubwa

  nyumba kubwa JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 10,278
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Hawa wazazi sijuhi tu sheria inasemaje; lakini wangefungwa japo miezi mitatu liwe funzo kwa other irresponsible parents.
  Huyo Lulu naweza sema amefanya alofanya kwa sababu ya kuwa na wazazi wasojua majukumu yao.

   
Loading...