Baba mzazi wa Lulu aibua mazito

wanaume nanyi mmezidi,mtoto wa miaka 18 hata mawazo ya maisha hana,unajizamisha,unategemea nini
Kwani kuna msichana anayetembea na birth certificate? au hujui ni yeye Lulu ndio alisema yeye siyo watoto show tena bali ni wakubwa show?
 
wazazi hapa tunapata somo zuri sana juu ya malezi. na ninafikiri ufke wakati sasa tuamue kuwa na nia ya dhati ya kuwalea wanetu katika maadili mema. hebu tofauti za sisi wazai tuzieke mbali wala tusiwe selfish katika kupata amani yetu na kusahau amani ya watoto.
 
ni aomba niandike mada hapa hapa mtanisamehe kama nitawaboa.

Hivi wazazi wanapogombana na kutengana je hapo huwa wanajali maisha ya watoto au wanajali maisha yao tu? na je hili laweza kutafsiriwa kama ubinafsi kwa hawa wazazi?
 
Kila thoery ina exception; wenyewe wataalamu wanatumia precision error. Ukweli unabaki pale pale wawili ni wawili tu. Mfano mimi na mume wangu wote hatupendi kuendekeza upuuzi katika malezi; lakini kuna kipindi najikuta nimechemka kwa sababu ya mapenzi yalopitiliza kwa wanangu; mwenzangu akiona niko blind anarekebisha; nakuja realize baadae jinsi nilivyo act kwa hisia na si objectivity. Same to my hubby. Kwa hiyo mkiwa wawili mnakosoana pale mmoja anapopitiwa na kutaka ku spoil mtoto.

Kulea mtoto si mchezo mara nyingi sana maamuzi yanahitaji second opinion; sasa kama uko peke yako no matter how tough you are kuna possibility ya ku fail.

nakupinga kabisaaaa..mimi nimelelewa singo parent tangu namiaka mitatu till leo sina upuuz huo,hiyo inadepend na ustrong wa mzazi katika malezi
 
Hatuwezi jibu kwa usahihi kama walo na hiyo experience. Ila mimi kama si watoto labda ningekuwa nsharudi kwenye u single maana nakumbuka ujana wangu nlikuwa si mtu wa msamaha. I hope wale wanao divorce wanakuwa wamefika point of no return otherwise yes they are very selfish.

ni aomba niandike mada hapa hapa mtanisamehe kama nitawaboa.

Hivi wazazi wanapogombana na kutengana je hapo huwa wanajali maisha ya watoto au wanajali maisha yao tu? na je hili laweza kutafsiriwa kama ubinafsi kwa hawa wazazi?
 
Kama Lulu yupo ktk minor age basi wazazi wana makosa makubwa kwa malezi yao mabaya.Wao walitakiwa wajue mtoto wao anafanya nini.Kuanza kujitetea kwasasa kunazidi kuonyesha mapungufu yao.Hili liwe funzo kwa wazazi wengine kwani ni muhimu sana sana mtoto kupata malezi ya baba na mama.Baba anataka kumwona rais kwasasa kwaajili ya nini?Alikuwa wapi kumtafuta rais kabla ya matatizo haya yote?Yeye mwenyewe malezi yamemshinda,atamshauri nini rais huyu?:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
 
Alisema angependa kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili azungumze naye kama rafiki yake na watafute suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.
Rais Kikwete kweli ana suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa? Just wondering

Mie nilichoshangaa ni hii habari ya kila kitu apelekewe rais, hii ofisi ya rais imeshushwa hadhi sana siku hizi. Itafikia ugomvi wa mke na mume watu wanataka kuupeleka kwa rais asuluhishe.
 
Huyo mzee ***** hana akili naona anataka umaarufu via this skendo ,kwani hii kauli ya kuwa Lulu anamiaka kumi na nane(18) aliitoa mwenyewe katika kipindi mikasi akihojiwa na mjanja wa maswali ya mitego Tanzania Salama J inawezekana unajuwa binti yako atafungwa ndo maana unaweweseka kama nakuona yaani unataka kukutan na Jk poole saanana
 
kesi ya wiz wakuku, machungwa, jiran kugombana, mme na mke kugombana, richmond, sakata la wizi wa mablion ya fedha benk kuu etc yote anapelekewa rais! hta hii ambayo inaonyesha dhahr kuwa wazaz wamefail ktk malezi ya mtoto wao, baba anadai anataka kuongea na rais kuhusu nn? je mwanae yacngemkuta hyo angetaka kumeet na rais? je iwapo mwanae atafanikiwa kutoka dhumun lke la kuonana na rais litakuwepo? hyo baba aache ujinga kilichobak wakubal tu wameshndwa ktk malez ya mtoto wao so waiachie jamii iwasaidie.
 
Wewe unaongelea wafanyakazi na professional sex workers wakati hapa point ni mtoto mdogo under 18. Angekuwa na kazi ofisini au profesional sex worker sidhani hata wazazi wake wangepata jeuri ya kuzungumza. Wanaongea kwa point kuwa ni mtoto mdogo; that is why nasema kama ni mtoto wao wameplay part gani kumfunza a behave kulingana na umri wake???

Hata wangemfunza vipi yule alishaharibikiwa.
 
Huyu baba hana adabu hata kidogo, eti wamemruhusu kwenda location baada ya kuhahakishiwa kuwa kikundi kina maadili. Kwanini asifatana nae kama mzazi huko location? wakati huyo ni mtoto mdogo. Kwani alikuwa hajui kuwa mwanae ni kicheche?

Halafu bado eti akaongee na Rais. Ndio iweje? anafikiri kuwa Rais ataiamuru mahakama imwachie? avune alichopanda, aiache mahakama ifanye kazi yake.
 
Baba mzazi wa Lulu aibua mazito Send to a friend
Thursday, 12 April 2012 21:36
0digg

kimemeta-michael.jpg
BABA mzazi wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu,'

ATAKA JAMII ISIMHUKUMU MWANAWE, HAKI ITENDEKE, AELEZA USHIRIKA WA LULU NA KANUMBA
Daniel Mjema
BABA mzazi wa msanii wa filamu, Elizabeth Michael 'Lulu,' ameitaka jamii kutomhukumu mwanawe kutokana na kifo cha msanii mwenzake marehemu Steven Kanumba, badala yake iache vyombo vya sheria vifanye kazi yake.

Mzazi huyo, Michael Edward Kimemeta anayeishi mjini Moshi, amewaomba Watanzania kuiachia Mahakama iamue kama mtoto wao anahusika katika kifo hicho ama la.

Kimemeta, ameeleza kuwa binti yake ana umri wa miaka 16 tofauti na inavyoelezwa kuwa ana miaka 18.

Juzi Lulu alifikishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Kanumba.

Kumekuwa na utata uliojitokeza kuhusu umri wa Lulu. Wakati mwenyewe akieleza kuwa ana miaka 17, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa umri wake ni miaka 18 na juzi Mahakama iliambiwa kuwa msanii huyo ana umri wa miaka 17 na baba yake akisema ana miaka 16.

Kwa upande wake, mama mzazi wa Lulu Lucresia Karugila, alisema tukio la kifo cha Kanumba na kukamatwa kwa binti yake Lulu, limempa mshituko mkubwa na kumsababishia maradhi ya kisaikolojia na kimwili.

"Hayo yaliyotokea kwa kweli yamenifanya niumwe kabisa hapa sasa hivi nimelala naumwa…nimempa go ahead (ruksa), baba yake azungumze kwa sababu taarifa zote anazo. Naomba mimi mniache kwa sasa,"alisema.

Kimemeta aliliambia Mwananchi jana kuwa mwanawe huyo alizaliwa Aprili 17 mwaka 1995 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

"Nataka nikuambie (mwandishi) mwanangu atatimiza umri wa miaka 17 ifikapo Aprili 17 mwaka huu. Sasa ana umri wa miaka 16 na ni mtoto. Tunavyosikia Kanumba alikuwa mpenzi wake inatuuma sana," alisema.

Baba huyo alisema alizaa na mama yake Lulu lakini hawakuwahi kuishi pamoja. "Mwanamke huyo alikuwa akifanya kazi Shirika la Ndege Tanzania (ATC) na muda wote Lulu alikuwa akiishi na mama yake jijini Dar es Salaam,"alisema Kimemeta.

Ameomba familia ya marehemu Kanumba ikubali kupokea pole ya familia ya Lulu kupitia gazeti hili kutokana na mazingira kutoruhusu familia hizo kukutana.

"Nasikitika mazingira ya tukio lenyewe mpaka sasa hayaruhusu familia yetu kwenda kutoa pole na kuifariji familia ya Kanumba kulingana na utamaduni wa mwafrika…tunaomba wapokee pole zetu kupitia njia hii," alisema.

Kwa mujibu wa Kimemeta, hivi sasa wanahofia maisha yao kutokana na jamii kujenga mtazamo hasi juu ya tukio hilo hata bila ya kusubiri vyombo vya sheria kusikiliza ushahidi wa tukio hilo na kutoa hukumu yake.

Alisema kuwa jamii inapaswa ifahamu kuwa, kikatiba mtu yeyote anayeshitakiwa kwa kosa lolote haimaanishi tayari ni mkosaji, bali atahesabiwa kuwa mtuhumiwa hadi pale Mahakama itakapomtia hatiani.

"Yanasemwa mengi mara ooh Kanumba ndio alianza kumpiga mwanangu mara ooh Kanumba alisukumwa …mimi nasema tuiache Mahakama hata sisi hatupendi mtu auawe, lakini Mahakama iachwe itende haki,"alisisitiza.

Akizungumzia maisha ya mwanawe Lulu, Kimemeta alisema alipokuwa akitangaza Kipindi cha Watoto Televisheni ya ITV, walifarijika sana, lakini alipoanza kuingia kwenye sanaa ya filamu, walijua sasa wamempoteza.

"Baada ya kuingia kwenye sanaa ya maigizo niliona kabisa tumempoteza mtoto na nilimweleza mama yake kuwa wale aliokuwa nao katika maigizo akiwamo Kanumba mwenyewe, nilikuwa siwaamini hata kidogo," alisema.

Kimemeta alidai kuwa siku moja mwanawe alimpigia simu akimwarifu kuwa alikuwa anakwenda jijini Arusha kurekodi filamu na Kanumba, yeye alipinga safari hiyo akitaka Kanumba amthibitishie usalama wa binti yake.

"Kwa sababu nilikuwa sipendezwi na hayo mambo nilimwambia mama yake azungumze na Kanumba na akatuhakikishia atamlinda na kambi yake ina maadili, lakini kumbe huo ndio ukawa mwanzo wa mwanaye kugeuzwa mpenzi wa msanii huyo,"alidai.

lulu-top.jpg
Elizabeth Michael 'Lulu,'

Baba huyo mzazi alidai kutofanya vizuri darasani kwa mtoto wake huyo, kulichangiwa na hatua ya kuingia katika sanaa ya uigizaji.


"Lulu alikuwa mtoto mwenye tabia nzuri sana hata alipokuwa ITV kwa kweli alitutia moyo wazazi wake kwa jinsi ITV walivyokuwa wakimlea, lakini alipojiingiza tu kwenye uingizaji hapo ndipo mambo yalipoharibika," alisema.

Alikanusha madai kuwa mwanawe hakumaliza kidato cha nne na kusisitiza kuwa Lulu alisoma Shule ya Kimataifa ya St Mary's na baadaye alihamia Shule ya Sekondari ya Midway High School na kumaliza kidato cha nne mwaka jana.

Alisisitiza kuwa katika mambo yaliyokuwa yakiwaumiza mioyo, ni namna mtoto huyo alivyozidi kuharibika kwa kuingia katika fani ya uigizaji filamu.

Alisema angependa kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili azungumze naye kama rafiki yake na watafute suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.

Alisema tayari ameanza mchakato wa kuonana na Rais Kikwete ili amweleze siri aliyodai ni ‘nzito' na kudai tayari ametafuta wazee watatu wenye busara wa kumsindikiza, endapo Rais atakubali ombi lake.

Pia ameziomba taasisi zinazojishughulisha na masuala ya haki za binadamu na msaada wa kisheria, kujitokeza na kumsaidia mwanawe.

Lulu alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi na kusomewa shitaka la kumuua
Kanumba, tukio lililotokea Aprili 7 mwaka huu eneo la Sinza Vatican.

Msanii huyo hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa Mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza mashauri ya mauaji na hivyo alipelekwa rumande Gegeza la Segerea hadi Aprili 23 mwaka wakati kesi hiyo itakapotajwa.

Kifo cha msanii huyo kimetikisa nchi kutokana na umaarufu wake, akiwa ameigiza filamu 40 zilikuwa zikirushwa katika vituo mbalimbali vya
televisheni ndani na nje ya nchi.


Kanumba alipanga kujenga shule

Katika hatua nyingine, Fidelis Butahe na Pamela Chilongola wanaripoti kuwa mchaguaji maeneo ya kupigia picha za filamu za msanii Kanumba, Rahim Khatib alisema marehemu Kanumba alinunua eneo la ekari 15 huko Mpiji mkoani Pwani kwa ajili ya ujenzi wa shule yake ya sekondari.

Khatib alisema Kanumba alikuwa na mpango huo muda mrefu na kwamba lengo lake lilikuwa kuwasaidia wanafunzi wa eneo hilo ambao hutembea muda mrefu kutokana na shule kuwa mbali na eneo hilo.

"Kanumba alikuwa na mipango mizuri katika maisha yake, kuna eneo kubwa alilonunua Mpiji ili ajenge shule ya sekondari," alisema Khatib.

Alifafanua kuwa hadi anafariki dunia, aliacha kiasi cha fedha zaidi ya Sh 40 milioni katika Kampuni yake ya Kanumba The Great.

"Marehemu ameacha fedha zaidi ya Sh 40 katika kampuni yake, magari matatu na hivi karibuni alinunua jingine aina ya Toyota Land Cruiser, "alisema Khatib.

Katika hatua nyingine Khatib alisema kifo cha Kanumba ni pigo kwa watu waliokuwa wakifanya naye kazi akiwemo yeye mwenyewe kwa kuwa walikuwa wakimtegemea kwa kiwango kikubwa.

Sintah naye alonga

Kwa upande wake msanii maarufu wa filamu nchini, Christina Manongi maarufu kama Sintah ambaye alikuwa mmoja wa wasanii wa kwanza kufika nyumbani kwa marehemu Kanumba muda mfupi baada ya msanii huyo kuanguka, alisema kuwa siku tano kabla ya Kanumba kufariki, alikuwa na hasira tofauti na alivyomzoea.

Sintah ambaye alikuwa na msanii huyo katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam Jumapili ya Aprili mosi pamoja na mwigizaji mwingine, Steve Nyerere alisema kuwa kila alichokuwa akimuuliza Kanumba, alimjibu kwa ukali.

"Ni tofauti na nilivyomzoea, siku ile ya Jumapili tulikaa pale Leaders Club mpaka usiku sana na kila jambo nililokuwa nikizungumza naye alinijibu kwa mkato na ukali kweli, ilinishangaza," alisema Sintah

Alifafanua kuwa moja ya mambo waliyokuwa wakizungumza na Kanumba ni pamoja na yeye kutaka kuacha uigizaji, suala ambalo marehemu Kanumba hakuliunga mkono na kumjibu kwa ukali kuwa asijitoe katika uigizaji.

source mwananchi


Bwana Kimemeta, kama ni masuala ya maadili mazuri kwa kizazi cha sasa na kijacho, ni vizuri kama yakianzia kwako.
Mtu mwenye umri wa miaka 49 bado ni kizazi cha sasa. Kuzaa nje ya ndoa ni upotofu mkubwa wa maadili. Licha ya hayo, kuzaa na mwanamke, kisha kuendelea na maisha yako, ukimwacha mtoto akue mwenyewe, huo ni sawa na uhayawani.

Mheshimiwa Rais Kikwete, kuonana na wewe itakuwa kujivunjia heshima aliyojijengea katika kipindi kifupi.

Pamoja na utata wa umri wa mtoto wako, bado anaonekana na sura ya kitoto. Licha ya hayo, hata kama angekuwa na miaka 20, bado akili yake haijakomaa.

Mimi binafsi ningekuwa mmoja wa "mkondo wa sheria", ningekukamata wewe pamoja na mzee Kanumba nikawafungilia jela kwa kushindwa kutoa malezi bora kwa watoto wenu, mpaka inafikia hatua ya Marehemu Kanumba kumkana baba yake.
 
huyu babake nae hamnazo kwelii... huenda kasingiziwa au alimkanaga from the begining. Yani baada ya kifo cha Kanumba ndo ameona binti yake anapotea kimaadili.. alikuwa wapi siku zote na skendo zoooote alizonazo lulu na tupicha twa uchi daily kwenye udaku. Najutaaaaa mwananchi kupata nafasi ya kumhoji lol
 
Mi naona hili lizee limechiz! Yeye anadhani kuonana na Rais ni sifa!
Suluhisho la kimaadili kwa watoto wote liko mikononi mwa wazazi kwanza na jamii kwa ujumla,eti Rais,amechanganyikiwa?mtoto wake alivyokinukisha ndio anakumbuka hilo?Kanumba na yeye aliishiwa,kuchukua kidemu kibaya kama kile?
 
Back
Top Bottom