Baba mzazi wa Lulu aibua mazito

Umeona eeh. Baada ya miaka kuongezeka mwenzetu yake inarudi nyuma.
Nimekumbuka kuna jamaa nilipewa story alipofika muda wa kustaafu na kupewa barua yake eti kaja an affidavit inaonyesha ni mdogo kwa miaka mitano. Kha. Employers wana kazi kweli. Na hivi ilivyo easy kutengeneza vyeti Bongo kazi kweli kweli.

dah siku zinavyo kwenda lulu anazidi kupungua miaka
this story can make a good movie
 
Alifafanua kuwa hadi anafariki dunia, aliacha kiasi cha fedha
zaidi ya Sh 40 milioni katika Kampuni yake ya Kanumba The
Great. wadau mi nimeona hapa si tulikuw tunasoma jamaa tajiri wa 3 kwa wasanii baada ya hasheem thabeet na lady jd akiwa na utajir sio chni ya mill 150 kwe kampun...dah kweli wasanii MASABURI
 
Niliangalia clip ya mama Lulu nikasikia anasema mama Kanumba ni dada yake, sikumwelewa; kumbe wote ni "wa nyumbani". Lakini ndo hiyo hata kama mnatoka mkoa mmoja haya ni makubwa hayawezi kumalizwa kifamilia; ni mahakama tu itaamua.
 
Masaburi aka akili mgando.Ndio madhara ya mtoto kulelewa na mzazi mmoja wakati mzazi mwingine anakula good time.

Sio lazima awe anakula goodtime. There are millions of reasons why marriage break or never has been there . The point is single parenting is a calamity. Niliwahi kusoma utafiti mmoja na wakasema asilimia kubwa ya walioko magereza ni wale waliolelewa na mzazi mmoja. Worse ni wale waliolelewa na mama . Tz kesi za single pareting zinaongezeka na hili ndio tatizo tutakaloendelea kuliona on daily basis.
 
Manyani mengine yaliyokuwa yana mchezea mwanaye anayajua?
 
Alisema angependa kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili azungumze naye kama rafiki yake na watafute suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.
Rais Kikwete kweli ana suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa? Just wondering

Mzee Michael Kimemeta anahitaji ushauri kuhusu hili,Hiyo optional ni mbaya

Hata hivyo naunga mkono kwamba mahakama iachwe ifanye kazi yake.Lulu ana haki ya kupewa msaada wa kisheria.Tatizo tumegeuka taifa la kutoa hukumu kwa hisia.Hatuko objective zaidi ya ushabiki na mahaba tu
 
Mmmmh kumbe lulu ana baba? Alikuwa anamlea vipi sasa? Maana vituko vyake vilikuwa haviishi!!!!
 
Alisema angependa kukutana na Rais Jakaya Kikwete ili azungumze naye kama rafiki yake na watafute suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa na cha baadaye.
Rais Kikwete kweli ana suluhisho la maadili kwa kizazi cha sasa? Just wondering

Lulu akishaachiwa huru ataendelea na huo mkakati wake wa maadili kwa vizazi vijavyo?
Usanii mtupu!
 
mzee kapagawa! Kweli maadili ambayo msingi wake huanzia ngazi ya familia yeye anataka kuanzia ngazi ya taifa, anyway kikwete mwenyewe kaelemewa mbaya hajatimiza ahadi yoyote ile aliyoahidi wengi,ndio atatimiza ya huyo mzee mmoja,
kama anataka akaongee na JK amsaidie atoke halafu ajilipe hapo sawa,
pia kuna taarifa nilizipata kuwa kuna majambazi 6 yaliuawa mmoja wao akiwa binti wa jk pande za morogoro hivi wakiwa wamevamia benki, walikuwa na gari la usalama wa taifa,mwenye taarifa zaid zenye ukweli wa hili

Labda Mzazi anasaka u'mkwe,manake Mkuu naye........
 
yote tisa kumi ni hilo la kuonana na rais kumjadili Lulu, hebu ngoja au rais ndo huyo kigogo aliyempigia Lulu simu?
 
Wazazi kama hawa ingebidi wachunguzwe na ustawi wa jamii ikigundulika wana play part kwenye kuharibika kwa binti yao wafungwe hata mwaka mmoja. Lulu amekuwa ashikiki utadhani hana wazazi? Kama ni below 18 na walisikia kuwa anajengewa sijui ameshajengewa nyumba na kigogo kwa nini hawakufuatilia huyo fataki ashitakiwe? Akileta fedha mnachekelea leo anashitakiwa kuuwa eti under 18; under 18 my foot. Eti tulimkabidhi Kanumba mtoto wetu amlee; are you serious???; utampaje mfupa fisi akulindie? Utampaje kijana lijali uangalizi wa mwanao wa kike??? Ili liwe funzo kwa wazazi wanaoshangilia either explicitly or implicitly uchafu wa binti zao.

hapo umenena.
 
Lulu akishaachiwa huru ataendelea na huo mkakati wake wa maadili kwa vizazi vijavyo?
Usanii mtupu!

Hana mkakati wowote fix tu. Kama kweli anao angeanza kuu implement kwa mwanae alipoona anapotoka.
 
Sio lazima awe anakula goodtime. There are millions of reasons why marriage break or never has been there . The point is single parenting is a calamity. Niliwahi kusoma utafiti mmoja na wakasema asilimia kubwa ya walioko magereza ni wale waliolelewa na mzazi mmoja. Worse ni wale waliolelewa na mama . Tz kesi za single pareting zinaongezeka na hili ndio tatizo tutakaloendelea kuliona on daily basis.

Ni wababa wachache sana wanaolelea watoto wao peke yao wengi huwa wanaoa wake wengine ambao ndio step mothers, so dont blame single women
 
Mtoto ameharibika mikononi mwa mama yake, alianza kwenda disko usiku mwaka 2009 ukiangalia vizuri utakuta alikuwa na umri wa miaka 14, kama aliwahi shule na miaka 7 ndio kwanza alikuwa form two . Umri hatarishi, kidato cha kupevuka. Inawezekana nguvu ya pesa ilitumika kumtumia vibaya mtoto. Tungependa kujua mama mzazi anashughulika na nini mpaka hivi leo? je wasanii mbalimbali hawafiki nyumbani kwa muhusika na kukutana na mama yake? Mama alikuwa anachukulia vipi mahusiano anayoyaona kwenye filamu? Nguo anazovaa mwanae alichukuliaje?
 
Mtoto ameharibika mikononi mwa mama yake, alianza kwenda disko usiku mwaka 2009 ukiangalia vizuri utakuta alikuwa na umri wa miaka 14, kama aliwahi shule na miaka 7 ndio kwanza alikuwa form two . Umri hatarishi, kidato cha kupevuka. Inawezekana nguvu ya pesa ilitumika kumtumia vibaya mtoto. Tungependa kujua mama mzazi anashughulika na nini mpaka hivi leo? je wasanii mbalimbali hawafiki nyumbani kwa muhusika na kukutana na mama yake? Mama alikuwa anachukulia vipi mahusiano anayoyaona kwenye filamu? Nguo anazovaa mwanae alichukuliaje?


......Kuna wabunge wamesema Lulu alikuwa tegemezi la familia, hivyo wanaomba wananchi kuchangia pesa kwa ajili ya familia ya Lulu.

Kama alikuwa tegemezi la familia, basi mama yake alikuwa hawezi kumuonya chochote huyo mtoto sababu anajua ndio pato lake la pesa linatokea hapo.

Watoto wengi wanaolelewa na mzazi mmoja huwa wanaharibikiwa, mtoto wa miaka 17 kuwa nje saa 6 za usiku mzazi upo wapi? Mie hadi nilipokuwa na umri wa miaka 20 sikuruhusiwa na wazazi kuwa nje ya nyumbani baada ya saa 2 usiku.

Kwa namna moja au nyingine wazazi walichangia kuharibika kwa huyo binti........acha afunzwe na ulimwengu sasa!
 
jamani sasa najihisi kizunguzungu maskini LULU.Mungu akutie nguvu na kukutumia msaada toka pattakatifu pake. Jamani kwa waliofuatilia comments zangu nyingi juu ya huyu binti mtagundua kuwa nimekuwa nikiwalaumu sana wazazi wake kuliko kumlaumu Lulu. sasa nimethibitisha kuwa lawama zangu ni sahihi kabisa kwenda kwa wazazi wake. Miaka ya 2004 nikiwa mwanafunzi wa shahada ya ualimu UDSM NILISOMA KOZI MOJA ILIYOITWA CHILD HOOD PSYCHOLOGY. Kozi hii ilifundishwa na Dr Sima kweli nimegundua kuwa nilijifunza kitu pale.

siwez kueka nondo zote hapa lakini ngoja nisummarize kwa haya machache:

kwanini nawatuhumu wazazi
1) kuwa single parented kid tena mikononi mwa mama peke yake kulimpa uhuru wa manyani kwani mama alikuwa lazy affair.
2) baba kuwepo mbali siyo sababu ya kushindwa kufuatilia mwenendo wa mwanae hasa alipoona ameanza kubadilika. Baba ana influence kubwa sana katika malezi na ndio mana huwa akisema mara moja tu inatosha kwa mtoto kutii.
3) kumuachia mtoto ajimiliki mwenyewe kosa sana kisheria kwani angeweza hata kufa akiwa kwenye kumbi za starehe. kwa mtot wa miaka 16 bado anatakiwa awe strictly under parents observation tena enzi zetu hata disco tukienda ni disco toto.
4)upendo kwa wazazi haukuwep na ni kama vile baba alimwachia mama ahangaike naye kwani alijua mtoto mwenye hekima ni fahari ya babaye bali mpumbavu ni mzigo wa mama ye.
5) siingilii mambo ya familia yao lakini ugomvi wa wazazi au kutokuwa na msimamo kati ya wazazi ni mateso kwa mtoto sana. manake hakuna aliyejali lulu analala saa ngapi, anatembea na nani ili apate nini au hata afya yake inaendeleje. labda niwaullize wazazi wake mara ya mwisho kumnunulia Lulu nguo ni lini? na je kwanini tusishawish mahakama iwafungulie hawa wazazi mashtaka kwa kushindwa kulea?
6)hivi wanafikiri ni sifa kwa mtoto wa miaka 16 kuwa ameshaujua utu uzima kiasi cha kuzini bila mpangilio, na kukesha kwenye kumbi za starehe? binafsi nimekasirishwa sana na tabia yao hii. poor parents.


kwa wale waliobahatika kuwa katika ndoa haya ndiyo madhara ya kuzaa nje ya ndoa.
 
Inawezekana kuna ukweli kuna tatizo katika single parenting. Nina dada yangu ni mjane; last born wake kashindikana ila sote tunajua tatizo ni malezi. Binti under 18 anarudi home usiku wa manane eti anatoka disco na mama yake anafungua mlango. Hiyo tulikuja jua baada ya yeye (sister) na mwanae kwenda kumsalimia baba yetu (babu wa mtoto) na baba to his suprise alishuhudia sister anaamka kumfungulia mtoto wake mlango usiku wa manane. Akafoka kesho yake sister anasema kama hataki wawe wanamtembelea aseme. Kwani anaona naye ameungana na wengine (sie) kumchukia mwanae.
Huyu sister ukitaka undugu uishe ongelea vibaya kuhusu binti yake. Yani tumebaki tunasubiri afunzwe na dunia.
nakupinga kabisaaaa..mimi nimelelewa singo parent tangu namiaka mitatu till leo sina upuuz huo,hiyo inadepend na ustrong wa mzazi katika malezi
 
wanaume nanyi mmezidi,mtoto wa miaka 18 hata mawazo ya maisha hana,unajizamisha,unategemea nini
 
Back
Top Bottom