Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,991
- 156,280
Ukiusikia usemi wa watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa basi sasa ndio amini kuwa usemi huo upo na unafanya kazi.
Jumapili iliyopita nilimsindikiza mpwa wangu ( mtoto wa dada yangu yangu) kwenda kujitambulisha na kupangiwa mahari huko kijijini kwa binti (Bibi harusi mtarajiwa)
Kwa kweli mapokezi yalikuwa baridi sana, na tukadhania huenda tungeitiwa wezi. Binti alifichwa na hatukuwa na mwenyeji hata mmoja.
Wenyeji walitupokea, wakatukaribisha chini ya mti na kutuacha kwa zaidi ya masaa manner, huku wao wakiwa ndani wakiendelea na kikao chao.
Baada ya masaa manne kupita hatimaye wakaja tulipo na kuanza kutuuliza maswali ya kebehi sana kuhusu imani yetu.
Wakatuambia wao ni Mashahidi wa Yehova, kwanini tumeenda kumposa binti yao tusitafute binti wa dhehebu letu?
Tukajibu kuwa sisi wote ni Wakristo, lakini hawakuridhishwa na jibu hilo. Dhihaka na kebehi zikaendelea.
Hatukupewa chakula wala maji hadi tunaondoka, tulaambiwa majibu yetu yatafuata kwa barua.
Leo jioni mshenga katuletea barua yenye jibu la ombi letu. Tunatakiwa kupeleka magovi matano ya wanaume watu wazima.
Isome mwenyewe hiyo barua.
Wito wangu kwenu wazazi, kama hamtaki binti yenu aolewe na mtu msiye mtaka, muwe wawazi, sio mnaleta mambo ya ajabu ajabu.